Vita havijaribiwi, Ila silaha zinajaribiwa

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,883
VITA HAVIJARIBIWI, SILAHA NDIZO ZINAJARIBIWA.

Anaandika, Robert Heriel.

Vita ni sumu. Sumu haionjwi.
Vita ni mkondo wa MTO wenye maji, kamwe usitie miguu kupima kina cha maji.
Vita havijaribiwi, ukivi-beep vinakupigia pasipo tafadhali.
Maisha ni vita, maisha hatajaribiwi, maisha hayachezewi kamari. Ingawaje maisha ni bahati lakini kuishi ni makusudi, tulizaliwa Kwa bahati lakini tunaishi makusudi kabisa.

Maisha ni vita ya maslahi ya viumbe kila mmoja akipigania Uhai wake, wenye nguvu hushinda wadhaifu, wenye akili hushinda wajinga. Ndivyo ilivyo. Kila mmoja hutafuta faida yake mwenyewe, yeye na awapendao.

Hakuna anayeishi Kwa ajili ya mtu mwingine, ingawaje tunategemeana. Kila mmoja ni muhimu kuishi lakini wapo ambao kuishi ni lazima kwao. Hao ndio wenye kuishinda vita.

Vita haijaribiwi Ila silaha zinajaribiwa.
Vita havina ubora Ila silaha zinaubora.
Vita havina macho Kwa maana wapiganao ni vipofu, naam ndio maana niliandika kuwa Maisha ni safari isiyo na macho, nao waishio ni vipofu, hawajui lilolombele Yao litakalowapata, na Yale waliyonayo hawajui yataondoka lini.

Unapopima kina cha maji mtoni usiingize mguu wako, Bali chukua ufito au jiti refu ulitumie Kama kipimo; ili Kama litabebwa kutokana na maji kuwa mengi yenye Kasi basi libebwe jiti na sio wewe.

Hivyo ndivyo vita inavyopigwana
Iwe vita ya maisha au vita ya mabomu na mikuki.

Huwezi kujitoa kafara kwenye vita ingali vita ni changa, kafara hutolewa dakika za majeruhi, dakika za lalasalama ili kuokoa jahazi na kulazimisha ushindi.
Mtu hujitoa mhanga/kafara Kwa kuokoa wengine sio kujitoa mhanga wa kipuuzi na kipumbavu ambao mtu hupoteza Uhai wake na bado ushindi usipatikane na kuwadharimu wengine.

Vita huanza Kwa silaha laini laini kabla ya silaha nzito na complicated.
Kwenye vita wanatangulizwa Kwanza wenye umuhimu mdogo na uwezo mdogo WA mapigano kabla ya kuhitimishwa na kiongozi Mkubwa.

Kumtanguliza Kiongozi mkubwa mbele kabisa Mwanzoni mwa vita ni kutaka mpigwe Technical Knockout (TKO) kwani atakapopigwa na kuuawa kiongozi Mkuu basi vita hiyo imeisha.

Katika Siasa, vita vya Kisiasa hutumia zaidi vibaraka na wafuasi kufanya mashambulizi huku viongozi Wakuu na wahusika nyeti wakijificha na pengine wasijulikane kabisa.

KAZI Viongozi hawa wakubwa ni kuratibu, kudhamini na kutoa misaada Kwa wafuasi na vibaraka wao wadogo katika mashambulizi ya kisiasa.

Ni kosa la kiufundi Kwa Kiongozi mkubwa wa Kisiasa au mfanyabiashara mkubwa kutoka Front kupigana kama mwendawazimu, kwani Kwa kufanya hivi atapigwa mapema na kuimaliza vita mapema.

Kiongozi kuharakisha kujitokeza front kwenye vita hi kuharakisha vita Kuisha.

Kiongozi mkubwa hushauriwa kutoka mafichoni mara ya kuona uelekeo wa vita kuwa wanashinda kwani Asilimia zaidi ya 80% wamewagaragaza vibaya mahasimu wao.

Kanuni ya kutuma vikosi vitangulie kabla ya mhusika Mkuu imefanywa na watu na wapiganaji wote wenye akili njema na wenye Sayansi na Sanaa ya vita. Yakobo na wanawaisrael waliitumia Sana mbinu hii.

Hata sasa majeshi mengi Duniani hutumia kanuni hii.

Ukiwaangalia hata Waasi au magaidi huwezi mkuta Kiongozi wao akiwa Front Kama Mpumbavu. Yeye hujificha mafichoni na kazi yake ni kuratibu na kuhakikisha mambo yanaenda Sawa.

Sasa Ndugu yangu Ndugai atakuwa mfano Bora katika Uzi wangu huu.
Vita haijaribiwi. Ukiingia uwe umejidhatiti Kwa kila Hali.

Hata hivyo hata Kama Ndugai alikuwa na agenda ya Siri labda ya maslahi ya 2025 basi Kwa vile yeye ni Kiongozi mkubwa hakupaswa kujitokeza hivi kizembe,hakujua yeye ni Kigogo mkubwa. Na Kama akipigwa yeye atagharimu kundi lake na watu wenye mtazamo Kama yeye.

Ndugai angepaswa awatumie Vijana au vibaraka wadogo wadogo huku yeye akihakikisha haijulikani ni yeye aliyenyuma ya mashambulizi hayo.

Hii hata wangekamatwa hao Vijana, bado mapambano yangeendelea Kwa sababu Mkuu wao yupo ni swala tuu la kusajili Vijana wengine.

Lakini Kuruhusu kujtokeza na kupigwa KO pasipo kuomba maji kutaleta athari mbaya upande wake na Kundi lake kwani wafuasi wake watajiuliza Kama mkubwa wetu kapigwa KO bila hata kumaliza Raundi sembuse wao wakina apeche alolo.

Mwisho, vita haijaribiwi, Ila silaha ndizo zajaribiwa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
1641555534197.png
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom