Vita dhidi ya ufisadi: Serikali kufuta leseni za wahasibu wote? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vita dhidi ya ufisadi: Serikali kufuta leseni za wahasibu wote?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mzee Mwanakijiji, Jan 24, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jan 24, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,376
  Trophy Points: 280
  Je kwa mtindo wa kufutia waganga wote wa jadi leseni zao za kufanya kazi ya ujuzi wao katika kile ambacho kinaitwa 'kupambana na vita dhidi ya mauaji ya Albino) kuna uwezekano wa siku chache zijazo kwa Waziri Mkuu kutangaza kufutia leseni wahasibu wote wa serikali kwa sababu ya wachache ambao wanajihusisha na vitendo vya kifisadi?

  Nini/nani atamzuia?
   
 2. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #2
  Jan 24, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Sio lazima afanye hivyo kwa kila jambo....
   
 3. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #3
  Jan 24, 2009
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  unnecessary criticism.. or rather ill targeted.. watu wengine mna hila.. badala yakulaumu jamii zaidi ambayo ndio inatenda haya. watu wana laumu serikali, kwa mtu yeyote anaejua jinsi tanzania ilivyo atajua ni jinsi gani nivigumu kuzuia kitu kama hicho bila kucompromise the rule of law.
   
 4. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #4
  Jan 24, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  MMKJJ,
  Kwa hili la kufuta leseni za waganga namuunga mkono waziri mkuu maana hawa watu ni wauaji na wamepoteza sifa za kazi zao.
  Ninaamini wanafahamiana ni nani hasa ambaye ana deal na ujinga huu wa kuua wenzao na hawataki kukemeana.
  Nashauri isiwe tu kwa kufunga leseni bali kuwapiga marufuku kufanya uchawi wao huo! Maana wanaleta maafa kila leo.
  Najua wengi ni followers wao, lakini hawa si watu wa ku support hata kidogo.
  Leo wanahitaji viungo vya albino. Kesho watataka viungo vya mtu mweusi tiiiiiiiiiiiii.
  Si watu wa kukumbatia hawa.
   
 5. G

  Ghwakukajha Senior Member

  #5
  Jan 24, 2009
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 172
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Two sides of different coins!
  Wahasibu ni professionals,they have gone to school before they acquire that title.Kwa hawa "waganga" the issue ni kuwa huo uganga wanajibatiza wenyewe tu.So kwangu mimi sioni kama PM or whoever anaweza kuwafutia leseni wahasibu hao.May be their professional bodies,maana wao ndio huwaqualify/kuwa_award as certified public accountants.Hapo hakuna siasa,and no one exactly no one can disqualify em for political reasons.
   
 6. Haki.tupu

  Haki.tupu JF-Expert Member

  #6
  Jan 24, 2009
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kwa hili la kufuta leseni za waganga nadhani serikali isilaumiwe. Ni katika kuhakiksha kila kinachowezekana kinafanyika! Ni lazima wajitahidi kufanya kila linalowezekana kuokoa maisha ya watu! Na hili nadhani limetokana na mapendekezo ya wananchi wa mikoa ya kanda ya ziwa. Sidhani kama kuamka na kuilaumu serikali kwa kila jambo ndio kuisaidia. Labda tuwaambie tu na huku EPA na Richmund wawasikilize wananchi tu. Tukiilaumu serikali kwa kila jambo tutapoteza maana.
   
 7. N

  Nurujamii JF-Expert Member

  #7
  Jan 24, 2009
  Joined: Jun 14, 2007
  Messages: 414
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Sio kufutiwa tu leseni bali waganga wote wa ndumba wakamatwe. Wanajuana hawa. Chimbuko la haya mauaji ni waganga wa kienyeji. Hata kama hakuna ushaidi wa kutosha bado lakini tunaweza kuwakamata kwa ushahidi wa kimazingira.

  Hivi kweli kama mganga anadai anazo dawa za kuondoa mikosi na hasara katika biashara kwa nini aachwe huyu? Wakamatwe waulizwe mbele ya media kama ni kweli hizo dawa zao zinafanya kazi au ni ulaghai then wachukuliwe hatua za kutapeli umma na kuchochea mauaji!!

  Nina hasira nao hawa watu mie. Mauaji ya vikongwe ni wao, maalbino ni wao, ubakaji ni wao.........arrrgggggghh!
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  Jan 24, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,392
  Likes Received: 81,412
  Trophy Points: 280
  Wahasibu wenyewe tunao wangapi hadi Serikali iwe na ubavu wa kuwafuta wengine!? Inanikumbusha gazeti moja nilinunua wakati Mzee Rukhsa akiwa Rais kulikuwa na kichwa cha habari "Rais apata ajali" basi nikasema nilinunue ili nijue kulikoni. Habari yenyewe iliwekwa kwa ndani ya gazeti kumbe Rais mwenyewe aliyepata ajali ni Emanuel Mlundwa aliyekuwa Rais wa chama cha masumbwi. Kufutia leseni waganga wa jadi na wahasibu wapi na wapi!!!
   
 9. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #9
  Jan 25, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Hapa kwa mtazamo wangu ni kwamba huyu PM kakurupuka, tena karupuka kutoa agizo hili. Cha kujiuliza hapa ni je hiyo serikali inajua ni waganga wa jadi wangapi wana leseni za kazi yao? Na je wana zi renew wapi hizo leseni? na wanalipa kodi kiasi gani katika mapato yao? haya yakiwekwa wazi basi tujadili kuwafutia leseni.

  1. Nijuavyo mimi kule vijijini ndanindani ambako Hospitali zipo Km 150 kutoka katika makazi yao wengi hutumia mitishamba katika kujitibu na miti hiyo hupendekezwa na waganga hao hao wa jadi ambao wengine hata leseni hawaijui ni kitu gani.

  2. Kabla ya kutoa tamko hili PM angehakikisha kwanza serikali inajenga hospitali kwa wastani wa umbali wa KM 3 nchi nzima kwanza. Hapo ndipo angeweza kutoa Tamko lake hilo. Hili linanikumbusha enzi za Sumaye alipotoa agizo la kwamba akikuta wauza mchicha wa magomeni michicha yao ya kijani wamueleze maji wanatoa wapi wakati kuna shida ya maji Dar, baada ya kupiga marufuku umwagiliaji wa mchicha (Akapachikwa nickname: ZERO).

  3. 99.9% ya wanasiasa ni wateja wakubwa wa waganga wa kienyeji hasa katika kusaka vyeo na ushindi. Sasa kuwapiga marufuku kufanya kazi zao hadharani ni kuwatia mjaribuni waheshimiwa na Pinda akiwa mmoja wapo. Nani asiyejua Bunge likianza pale Dodoma mji hujazwa na hawa wataalam wa Science ya kuruka kwa ungo?.

  4. Serikali pamoja na kuwa na vyombo vya dola vyenye wataalam waliosomea pale CCP na kwingineko wameshindwa kutengeneza network ya kuwanasa hawa wauaji wa Albino?, mbona ni aibu sana kwa Nchi? ina maana hawa wauaji wanatechnolojia kubwa kuwazidi polisi? au Polisi wanaogopa nao kushushwa mishipa?, na kama wanaogopa je wale watakaoendelea kufanya shughuli zao za kiganga watakuwa na ubavu wa kuwakamata?.

  5. Serikali imeshindwa kazi na kuwatupia mpira wananchi kwa kisingizio cha kufuta vibali vya waganga wa jadi na kuwataka wananchi wawaangalie waganga je, waheshimiwa kuanzia Rais, PM mawaziri wabunge na viongozi wote nao wapo tayari kuwataja waganga wao wa Jadi?. Basi waanze kutoa mfano wao kwa kuwaanika kabla wananchi nao hawajafuata mkondo. vinginevyo hii ni Ze Komedi.


  Hoja ya mwanakijiji nilivyoielewa ni kwamba kama suluhisho la kupiga vita wauaji wa albino ni kufuta leseni za waganga wote kwa sababu miongoni mwao wapo wanaelekeza mauaji basi ni kweli na Wahasibu nao wafutiwe kwa sababu miongoni mwao wapo wanaoendekeza UFISADI, Nafikri hapo PM na washauri wake wameenda "Chaka" au wamekula "Kasa".
   
 10. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #10
  Jan 25, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,866
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Je mnajua ratio ya MD to Mganga wa kienyeji Tz? ni 1:50,000 versus 1:350!

  Kwa Tz ina maana ktk kila watu 350 yupo mganga 1.

  Hawa waganga wapo hila mahali. Hizi ni data zimechapishwa kisayansi..and this is average..sehemu zingine may be kila mtu ni mganga!

  Uganga is an institution ..has been been there 1000 years or so..so it does not just vanish kwa kuwa Pinda hawapendi!

  sasa kama huduma afya vijijini hakuna na watu wanaugua kila siku unategemea nini??

  Let us argue beyond the box!
   
 11. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #11
  Jan 25, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0

  Unaweza toa link au source ya mahali ambapo hizo data zimechapishwa nami nikajisomee?
   
 12. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #12
  Jan 25, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,866
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Usipende kutafuniwa kila kitu ..tafuta ulkkwama PM me.
  Ahsante!
   
 13. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #13
  Jan 25, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Huu ni uwanja wa jamii, ukiweka data weka nzima nzima wasomaji waelewe. Unaleta vipisi ili uandikiwe PM?
   
 14. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #14
  Jan 25, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,866
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  JF sii uwanja kutafuniwa kila kitu..kama ni kujifunza it does not take 3 min kupata data kama hii! I had expected you to builb a counter argement! Jaribu angalia references hizi chachehapa chini.

  1. Cunningham AB: African Medicinal Plants: setting priorities at the interface between conservation and primary health care. Working paper 1. UNESCO, Paris; 1993.
  2. Courtright P, Chirambo M, Lewallen S, Chana H, Kanjaloti S: Collaboration with African Traditional Healers for the prevention of Blindness. World Scientific Publishing Co; Singapore; 2000.
  3. Emmanuel A Makundi , Hamisi M Malebo , Paulo Mhame , Andrew Y Kitua and Marian Warsame: Role of traditional healers in the management of severe malaria among children below five years of age: the case of Kilosa and Handeni Districts, Tanzania. Malaria Journal July 2006.
   
Loading...