Vita Dhidi ya Ufisadi: Mwaga Mboga, Nimwage Ugali, Kaazi Kweli Kweli! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vita Dhidi ya Ufisadi: Mwaga Mboga, Nimwage Ugali, Kaazi Kweli Kweli!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Buchanan, Nov 1, 2009.

 1. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #1
  Nov 1, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kuna baadhi ya kauli za viongozi wetu huwa zinatia wasiwasi kama kweli wana nia ya dhati ya kupambana na uovu ukiwemo ufisadi! Kauli ya Ole Sendeka kwamba atamharibia Rais Kikwete kwa kuanika maovu ya Serikali endapo hataacha kuwafuatilia wabunge kwa tuhuma za kulipwa posho mara mbili kwa kazi moja! Kauli nyingine ni ya Dkt Mwakyembe alipoitoa mara baada ya kutoa Ripoti ya Richmond kwa wale ambao walikuwa wanachokonoa kiaina mambo ya Richmond kwamba Kamati yake ingetoa hata yale ambayo hawayakusema kwa kuwa waliogopa kuiumbua Serikali! Sakata linaloendelea sasa hivi la posho mbili kwa kazi moja nako limekuwa na timing kali sana mpaka limeleta mkanganyiko mkubwa! Kauli nyingine ni ya Mh Zitto Kabwe aliyoitoa humu kwamba anawajua waheshimiwa wabunge wanaofoji tiketi za mabasi! Sina hakika kama Mh Zitto na yeye kama ameweka silaha kibindoni ili na yeye akilipuliwa amlipue mtu au amefikisha taarifa hiyo kwenye vyombo vinavyohusika! Observation yangu nyingine ni kuhusu Kesi ya Zombe ambaye alidai kwamba ETI amegundua kwamba Jeshi la Polisi linabambikizia watu kesi! Iweje huyu bwana Zombe "agundue" ubambikiziaji huo baada ya yeye kuwa na kesi huku akijua kwamba malalamiko ya ubambikiziaji kesi ni ya siku nyingi? Baada ya kutoa hayo machache nionavyo mimi upambanaji dhidi ya maovu kwa TZ utachukua muda mrefu kwa sababu "wapambanaji" wanapambana ili kujijenga wao binafsi zaidi kuliko kupambana na uovu kama ulivyo! The theory behind: "mwaga mboga nimwage ugali!" Huu ndio ukweli, kwa hali ilivyo sasa! Rais mwenyewe ana orodha ya wabwia/wauzaji wa madawa ya kulevya, anasubiri wakimchokonoa pabaya ana-single out (anam-shortlist, if you like) jina la mbaya wake na kumzima kiulaini! Hii ni TZ bwana, acha mchezo!
   
 2. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #2
  Nov 1, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Wadau mnasemaje hapo? Kuna upambanaji kweli au ni mawazo yangu tu?
   
 3. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #3
  Nov 1, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Huo si Upambanaji ni Uviziaji
   
 4. Companero

  Companero Platinum Member

  #4
  Nov 1, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Aah umesahau zile ngumi za utotoni...nianze uone cha mtema kuni...anza wewe uone kilichomfanya kanga asiwe na manyoya shingoni...
   
 5. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #5
  Nov 1, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Sure!
   
 6. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #6
  Nov 1, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Kauli zote hizi hazitoki kwa manufaa ya wapiga kura wao majimboni hapanani kwa sababu wameguswa wao kwenye ulaji wao direct ndiyo kisa. Nashawishika kusema kwamba Serikali ina uchafu mwingi ambao hata wapambanaji wanaujua ila wamekua wakipambana mkono uende kinywani na kuacha watanzania wanaumia .
   
 7. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #7
  Nov 1, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kauli hizi huwa zinakuwa much disturbing hasa pale ambapo jamii ilipoanza kujenga imani kwa "mpambanaji" kisha all of a sudden analewa sifa na kuanza kutema pumba!
   
 8. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #8
  Nov 1, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,578
  Likes Received: 3,881
  Trophy Points: 280
  hamna kitu pale Buchanan hesabu maumivu, si Mwakyembe wala nani CCM
   
 9. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #9
  Nov 2, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Kwa mtazamo wangu wote ni WAIGIZAJI, na kwa system ya serekali ya TZ ilivyo wote hawawezi kuchukuliwa sheri, kwana INAONEKANA wana siasa wa Tanzania wote woko juu ya sheria, utakumbuka ya kina marehemu DITOPILE, CHENGE(mzee wa vijicent) watuhumiwa wa EPA.. nakadhalika kibao.. wote ni MASTERLING na STERLING kwenye cinema sikuzote hauwawi mpaka mwisho wa sinema, kwa hiyo kwenye cinema hii inayoendelea bongo, masterlingi wote wa EPA, RICHMOND, KAGODA nakadhalika kibao, hawata dhurika kabisaaa sana sana watapata vijeraha vidogovidogo tu (kama kujiuzulu au kustaafishwa) na hiyo inakua ndio end of stori. Nafikiri mpaka hapo mmenisoma vizuri
   
 10. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #10
  Nov 2, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Nimeipenda notion ya "starring hauawi, anapata vijeraha vidogo vidogo!"
   
 11. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #11
  Nov 2, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,545
  Likes Received: 81,981
  Trophy Points: 280
  Kwa kifupi Serikali tuliyokuwa nayo yote ni bomu na masterling wote wanajua uozo mwingi wa Serikali iliyokuwa madarakani na si ajabu wameshatoa vitisho dhidi ya Serikali hiyo kwamba wakiguswa tu katika ufisadi unaowahusu basi wataamua kuanika uozo wote wa Serikali sasa Serikali inawaogopa kama ukoma kwa kutotata kuwagusa kabisa na huku Watanzania tukiishinikiza Serikali kila kukicha mbona masterling bado wanapeta tu!? Kulikoni? ingekuwa enzi za Watanzania wa mwaka 47 haya yote yangeshasahaulika sasa lakini Watanzania wa leo wameanza kuamka na kuhoji mambo mengi ambayo hayaingii akilini tena tunayahoji hadharani.
   
 12. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #12
  Nov 2, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Namkumbuka saana hayati Baba wa Taifa Mwl JK Nyerere wakati akipambana na wahujumu uchumi aliwakamata wahalifu miaka ya 1983 kisha akatunga sheria ambayo ilikuwa na retrospective effect ili kuwaadhibu! Samahani wanaharakati za Haki za Binadamu kwa hili, sometimes it helps by doing impossible actions in extraordinary circumstances!
   
 13. Al Zagawi

  Al Zagawi JF-Expert Member

  #13
  Nov 2, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,717
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  napenda kumnukuu mtu fulani hapa JF kujibu swali lako, 'Tanzania ni zaidi ya uijuavyo'
   
Loading...