Vita dhidi ya Malaria ni kupoteza Muda

Regia Mtema

R I P
Nov 21, 2009
2,970
864
Nimekuwa nikistajabishwa na hili tangazo la kwenye luninga ambalo lina waonyesha katuni wakizungumzia jinsi ya kujikinga na Malaria kwa kutumia chandarua chenye dawa.Kinachonishangaza ni kuwa tangazo hili liko kwa lugha ya kingereza wakati tunatambua kabisa kwamba zaidi ya asilimia 60 ya watanzania hawafahamu lugha hii.Na kimsingi wasiofahamu lugha hii ndio wale wasiofahamu jinsi ya kujikinga na Malaria,nikiassume kwamba hawajaenda shule hivyo hawafahamu kabisa jinsi ya kujikinga na Malaria.Hivi hili tangazo limemlenga nani hasa?Kwa mwendo huu hii vita ya Malaria itaisha kweli?na je rasilimali katika vita hii zinatumika ipasavyo?
 
Hivi Vyandarua vyenye dawa ndiyo njia kuu ya Kupambana na Malaria? Mbona ndiyo inayotangazwa Zaidi? Isije ni Matangazo ya Biasahara ya Net! How about kutokomeza Mazalia ya Mbu?

Tukienda Bar twende na Vyandarua, tukiwa tunakula tujifune Vyandarua? Na je tukiwa tunajisomea Usiku tujifunike vyandarua?
 
Kwanza, hii approach ya kupambana na malaria kwa msisitizo wa chandarua ina walakin. Sioni utawezaje kumaliza malaria sehemu Tandale kwa msisitizo wa chandarua. Waweke emphasis kwenye kutengeneza mifumo ya maji machafu, usafi kwa ujumla, serekali kupuliza dawa mitaani, nk.
 
Ndio maana nikasema hii vita nikupoteza muda..Imekuwa yakibiashara zaidi.Vyanzo vya mbu haviguswi kabisa..
 
Hivi Vyandarua vyenye dawa ndiyo njia kuu ya Kupambana na Malaria? Mbona ndiyo inayotangazwa Zaidi? Isije ni Matangazo ya Biasahara ya Net! How about kutokomeza Mazalia ya Mbu?

Tukienda Bar twende na Vyandarua, tukiwa tunakula tujifune Vyandarua? Na je tukiwa tunajisomea Usiku tujifunike vyandarua?

Nakuunga mkono mkuu hapo kwenye nyekundu Mkuu. Kama hakukuwa na kampeni ya usafi ili kuhakikisha mbu hawana sehemu za kuzaliana hii kampeni itakuwa ni usanii tu mwingine wa hali ya juu na haitakuwa na mafanikio yoyote.
 
Na mbaya zaidi Rais amejitokeza front..
 
Hivi Vyandarua vyenye dawa ndiyo njia kuu ya Kupambana na Malaria? Mbona ndiyo inayotangazwa Zaidi? Isije ni Matangazo ya Biasahara ya Net! How about kutokomeza Mazalia ya Mbu?

Tukienda Bar twende na Vyandarua, tukiwa tunakula tujifune Vyandarua? Na je tukiwa tunajisomea Usiku tujifunike vyandarua?

hawachoki kutufanya wajinga au hawajaridhika kutufanya wajinga...........
 
Na mbaya zaidi Rais amejitokeza front..

Yaani ni vitu vya kustaajabisha sana. Haihitaji kuwa na Phd ili kufahamu kwamba katika kampeni za kupambana na malaria matumizi ya vyandarua inabidi yaende sambamba na kupambana na hali ya uchafu wa kutisha katika miji yetu mbali mbali ili kuondoa kabisa sehemu ambazo mbu wanaweza kuzaliana, lakini hili la usafi limeminywa kabisa.
 
hawachoki kutufanya wajinga au hawajaridhika kutufanya wajinga...........

Dada/Kaka hawa watu nawafananisha na Kupe watatunyonya mpaka tuwe weupe kwa kukosa Damu!

Ndiyo tatizo la kuingiza Siasa hata katika Mambo yanayohitaji Utaalamu! Mazalia ya Mbu yapo yanaonekana lakini hakuna Jitihada zozote kuyatokomeza!
 
It is purely politics,hivi uwepo wa Rais kwenye matangazo mbalimbali ya operesheni zinduka unaimpact gani kwenye hii vita?kwani akiwepo yeye ndio wananchi watapambana na Malaria?
 
Back
Top Bottom