Iliwahi kusikika kauli kutoka kwa mkuu wa nchi katika "kuwakemea" wahusika wakubwa wa madawa ya kulevya. Kauli za viongozi wa kitaifa siyo rahisi kupotei kwenye historia. Kwa upande mwingine, madhara ya hii biashara ni ya wazi kwa maisha ya wananchi na taifa kwa ujumla.
Mheshimiwa rais wa awamu ya nne JMK, aliwaasa wafanyabiashara wakubwa kwinye hii biashara, kwamba waache, kwani anayo orodha ya majina yao.
Tafakari;
Je kulikuwa na mashaka au ugumu gani ya kiongozi kutoruhusu hatua za kisheria zichukuliwe?
Je, huyu kiongozi aolikuwa anatambua madhara ya kauli yake? kwamba hakuhitaji kuwachukulia hatua, na ni wazi hakufuatilia kama kauli yake ilizingatiwa na pengine kupunguza athari za hii kitu.
Na mwisho, je, mkuu huyu anatambua ni jinsi gani wananchi wasiyo hatia wanavyodharirika utu wao, na kupoteza nguvu kazi ya taifa; Je, alikuwa na nia ya dhati ya kupambana na watanzania hawa wachache ili kulinda na kutetea utu, haki na matakwa ya kikatiba?
Sina habari ya mwitikio wa mataifa rafiki au ya magharibi, punde walivyosikia kauli ya mkuu huyu, kama ilisikika. kumbuka mataifa haya yanapambana kwa kufa na kupona na hii vita isiyoisha.