Vita dhidi ya madawa na viroba ni vyema ijumuishwe na kupiga vita mikorogo

Bornventure

JF-Expert Member
Jan 29, 2017
529
523
Habari wanajamii. Nimejaribu kuwaza juu ya haya majanga yanayowapata wa Tanzania kutokana na matumizi ya madawa ya kulevya na viroba na naipongeza serikali kwa hilo.

Sambamba na hilo nadhani ni muda muafaka kwa serikali kuona madhara makubwa yanayowapata vijana hasa wa kike kutokana na kutumia mikorogo na madawa makali kujichubua sura zao na kuchukua hatua madhubuti kupiga vita.

Ushauri wangu nikwamba kwa kutumia strategies zilezile kama kudhibiti madawa pia nivyema Police wakaanza kuwakamata wadada wote (kuanzia askari wa kike hasa trafiki waliojichubua) na kuwataka wataje hiyo mikorogo walikoipata finally kuwakamata waingizaji wakubwa.

Nadhani kwa kufanya hivyo tutasaidia kurejesha afya ya ngozi na uzuri wa Dada zetu wa kitanzania.
 
Mmhhh.... Izo za kuwadaka waingiza mikorogo umeniacha hoi..... Ila wengine wanatengeneza mikorogo yao wenyewe majumbani.......
Lakini hii mikorogo imepigwa vita kitambo sana huoni kila mara TFDA inaagiza kuchoma vipodozi vyenye viambata vya sumu
 
Mmhhh.... Izo za kuwadaka waingiza mikorogo umeniacha hoi..... Ila wengine wanatengeneza mikorogo yao wenyewe majumbani.......
Lakini hii mikorogo imepigwa vita kitambo sana huoni kila mara TFDA inaagiza kuchoma vipodozi vyenye viambata vya sumu
Hawako serious hata hao TFDA because hivyo vitu ni vingi saana vipo tu madukan na wao wengi tu hutumia
 
Kuna waziri mmoja huko serikalini yule anatumia kabisa mkorogo aisee unataka afanane na remy wakizuia mikorogo? Hebu acha watu wafanye mambo yao bwana.
 
Back
Top Bottom