Vita dhidi ya mabepari wa madini inahitaji umoja, ilimshinda Dr Williamson wa Mwadui na Mwl Nyerere

Huwa na washangaaga sana Watu wakiwasifia awa viongozi wawili......

Ni watu ambao huwa nikiwafikiria mpaka na sisimka....

Ila Watanzania bado tuna umbumbu sijui ndo ulofa kama tulivyoambiwaga na ye mwenyewe, utashanga mtu msomi kabisa lakin anakwambia bora enzi ya Mkap, ajui mkapa alikua anapata fedha kwa kuuza Rasilimali zetu, kwa kuuza mashirika yetu ya Umma tena kea bei za Kipuuzi, uyu mtu ndo alisababisha upigaji mkubwa mpaka awamu iliyofuata.... Tunamatatizo sana nchi hii! Mungu atuuhurumie tu atusaidie kwa Mapenzi yake

Mwafrika Mpe Mswaki kisha Mng'oe Jino...
Yani hadi unajiuliza ni kwanini umezaliwa ndani ya bongo hii?
Ni wapumbavu sana sisi Waafrika kwa kukosa upeo wa maisha ya vizazi vyetu vijavyo kama JPM

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Renogoatiate? You wish it was easy that way. Hawa jamaa just know they can afford best lawyers and financial advisors anywhere in the world. Ndo maana vinchi vyetu vya kimasikini tuna vikwazo vingi sana kwenye Safari ya kujikwamua kiuchumi. Hata wale wasomi wachache tulionao Kama lawyers akina Mkono au mama Majaar...ndo hao wana gang up na hao the so called investors. Muwekezaji akipata mgodi wa 2 billion usd akampa mkono 10 million usd ashughulikie kila kitu serikalini....shida iko wapi? Ndo maana unakuta akina Mkono et al wanagombea ubunge. They want easy access to the decision makers. In reality. Nchi zetu tunaibiwa na wale tuliowaamini. Sasa kwa sababu ya umasikini wetu...everyone in the country has a price! Unavyosikia elites wanapiga kelele JPM ameua uchumi....unafikiri in uchumi upi unaliliwa? Vita hii in kubwa mno.

Bro...mtandao wa wapigaji in mkubwa mno! JPM amejilipua...Haya maji kina in kirefu. I wish him well.
Daaah Kaka umenena kwa uchungu sana hadi nimejikuta nikitaka kububujikwa na machozi.

Mungu nakuomba tupatie uvumilivu sisi Wa-TZ tumpatie Raisi wetu umoja wa pekee sana ili tujikwamue na hii vita ya Mabeberu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"......Report ya pili ya Kamati ya Rais juu ya maboso(mchanga wa madini)inaenda kufungua ukurasa mpya wa "vita" ya moja kwa moja kati ya Rais wa Tanzania yeye binafsi dhidi ya wafanyabiashara wakubwa wa madini duniani.Tumuunge mkono Rais,kwa kumuelekeza vizuri na kwa staha pale anapokosea,na pia kwa kumpongeza kwa kiasi pale anapopatia mikakati katika mapambano haya.Tunaenda kuanza "vita" rasmi na "wamiliki" wa madini wa dunia,tusikate tamaa...Aluta Continua
barafu wa Jf toka Toronto-Canada

Mkuu barafu, mi nadhani adui yetu nambari moja ni aina ya sheria tulizo/tunazojitungia kuhusu sekta hii ya madini na usimamizi mbovu wa jinsi ya kupata kodi ya serikali. Kwangu mimi haijalishi NANI anamiliki mgodi wa Mwadui. Au globally anamiliki migodi mingapi. Muhimu ni yeye kutulipa CHETU. Wala sidhani dawa ni serikali kutaifisha migodi hii. Dawa ni Serikali KUJUA kodi yake stahiki ni IPI. Pili serikali iweke sheria rafiki kwenye kuuziana madini. Tatizo la ubovu wa sheria zetu uko hivi Mkuu, kesho ukisafiri na wenzio kutoka Shinyanga kwenda Bariadi, mkiokota ALMASI, mtagundua kuwa ili muiuze kuna mlolongo mrefu wa sheria zitazowaandama kiasi kuwa mwishoni mtatafuta nani awape chenu muishie bila bughdha. Hii vita ya mabepari haipaswi hata kidogo kutuacha tukiwa maskini kama tunajua kodi yetu ni pi.
 
Daaah Kaka umenena kwa uchungu sana hadi nimejikuta nikitaka kububujikwa na machozi.

Mungu nakuomba tupatie uvumilivu sisi Wa-TZ tumpatie Raisi wetu umoja wa pekee sana ili tujikwamue na hii vita ya Mabeberu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Bila shaka sasa safari rasmi tumeianza,leo Rais kashuhudia makubaliano ya 16% na 50% ya faida.Tungoje na tuone,yajayo yanafurahisha
 
One fact that will never change is: Despite all his shortcomings President Magufuli was very right about the extent of foreign banditry and extortion of our natural resources.
 
Mkuu barafu, mi nadhani adui yetu nambari moja ni aina ya sheria tulizo/tunazojitungia kuhusu sekta hii ya madini na usimamizi mbovu wa jinsi ya kupata kodi ya serikali. Kwangu mimi haijalishi NANI anamiliki mgodi wa Mwadui. Au globally anamiliki migodi mingapi. Muhimu ni yeye kutulipa CHETU. Wala sidhani dawa ni serikali kutaifisha migodi hii. Dawa ni Serikali KUJUA kodi yake stahiki ni IPI. Pili serikali iweke sheria rafiki kwenye kuuziana madini. Tatizo la ubovu wa sheria zetu uko hivi Mkuu, kesho ukisafiri na wenzio kutoka Shinyanga kwenda Bariadi, mkiokota ALMASI, mtagundua kuwa ili muiuze kuna mlolongo mrefu wa sheria zitazowaandama kiasi kuwa mwishoni mtatafuta nani awape chenu muishie bila bughdha. Hii vita ya mabepari haipaswi hata kidogo kutuacha tukiwa maskini kama tunajua kodi yetu ni pi.

Umesema kweli tupu nami nakuunga mkono 100%

Kwa sababu mtu unajiuliza kama unataka kumnyang'anya mwenye uwezo wa kuzalisha madini haya ili iweje mwisho wake maana wewe huna utaalamu wala uwezo wa kimtaji kuendesha biashara hii...?

Hizi rasrimali tumepewa na Mungu ili tuzivune, tuzitumie na kumnufaisha kila mtu...

Kama kuna mtu ana uwezo wa kuchimba madini, aandaliwe mazingira ya kuivuna rasrimali hiyo na serikali ipate kilicho chake ili ikitumie kwa ustawi wa wananchi wote..

Hii dhana ya kuwa "kama hatuna uwezo wa kitaalamu na kimtaji, hakuna haja ya kuruhusu wengine kuvuna rasrimali hii, na kwamba, bora tukae nayo hivi hivi mpaka tutakapokuwa na uwezo...", ni dhana potofu.

Leo ukienda pale Mwadui, kumechakaa na sifa zote za eneo hili kama alivyoeleza Barafu hazipo na mtu akisoma sasa na akaenda kutazama atasema kuwa Barafu anadanganya...

Sababu ya yote haya ni kwa serikali kutokuwa na consistency ktk SERA na SHERIA za nchi yetu. Kila kiongozi huja na hisia na matamanio yake binafsi na matokeo yake ni kuharibu tu kwa kwenda hatua 10 mbele na badae 20 nyuma na ndiyo yanakuwa maisha yetu...
 
Back
Top Bottom