Vita dhidi ya dawa za kulevya vs uhakiki

Mfalme Daud

Senior Member
Feb 3, 2012
170
125
Nimekuwa nikipitia maandiko mengi humu kuhusiana na mambo haya mawili. Wapo wanaosema kuwa;

1. Wanaohoji uhalali wa vyeti/majina ya mkuu wa mkoa ni wauzaji/watumiaji dawa za kulevya na wanataka kututoa kwenye hoja ya msingi ambayo ni VITA DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA

2. Wapo wanaosema uhakiki hauna uhusiano na vita hii.

Kimsingi, mimi binafsi naunga mkono juhudi zote za kupambana na matumizi na uuzwaji wa dawa za kulevya. Katika kujibu hoja hizo hapo juu nitatoa maelezo kwa upana katika kila hoja.

HOJA YA KWANZA.
Ili hoja hii iwe na mashiko lazima mambo haya yawe yamezingatiwa au maswali yafuatayo yawe yamejibika.
1. Je, tuhuma dhidi yake ni za kubuni, na hazina ukweli?
2. Kama ni uzushi, kwa nini anakuwa mgumu kuonesha vielelezo kufuta uzushi huo?
3. Kama aliweza kuwataja hawa watu wabaya hadharani jambo alilosema linaweka maisha yake rehani, kwa nini anakuwa mgumu kuweka vielelezo vitakavyookoa kazi yake na reputation (hadhi) yake?
4. Je, tuelewe kwamba vielelezo anavyovibana ndiyo vinahatarisha kazi yake?
5. Kama ni tuhuma za kweli, Je, Hawa wauza madawa ya kulevya walimfelisha mitihani? Walimnunulia cheti? Maana ukihusianisha haya mambo, ni kama unataka kusema kwamba, hawa wauzaji walikuwa wamemwandaa huyu mtu kukaa kwenye hiyo nafasi ikiwa ni pamoja na kumtafutia cheti bandia ili aje awasaidie.

Kwamba walijua na kumfahamu tangu akiwa mtoto, wakampeleka kuchoma mkaa, wakamfanya utingo, wakamshawishi na aliyemteua amteue ili awalinde... Na wameamua kumwaibisha kwa sababu kazi waliyomtuma ya kuwalinda ameshindwa.

6. Wanaohoji wanasema, kwa nini suala hili limekuja wakati huu. Kwani mtu akifumaniwa mnauliza kwa nini afumaniwe siku ya 50 na sio siku ile ya kwanza? Kufumaniwa ni kufumaniwa, iwe baada ya miaka elfu au siku ya kwanza.
Labda sijui tunachukuliaje uhakiki, kwani kuonesha cheti si suala la dakika moja tu linaisha na mambo mengine yanaendelea? Kwamba mnazungumzia suala la muda kama kuonesha vyeti kunaweza kuchukua miaka 5

7. Tena wanaongezea kuwa tuhuma za UHAKIKI zina lengo la kututoa kwenye hoja ya msingi ya dawa za kulevya. Swali ni hili, Je, mtuhumiwa yupo kwenye kamisheni ya kupambana na dawa za kulevya? Kama tayari kuna kamisheni, kwa nini wahangaike na huyu ambaye mle hayumo?

Kama suala ni majina, yeye si alipewa? Na waliompa si watayapeleka kwenye kamisheni husika? Sasa kwa nini wahusika wasipambane na kamishna au kamisheni husika wapambane na asiyehusika? Maana kama lengo huyu asiwepo, je kamisheni itashindwa kufanya kazi?

HOJA YA PILI.
Ili hoja hii iwe na mashiko lazima kuzingatia mambo yafuatayo.
1. Je, uhakiki na vita dhidi ya dawa za kulevya nini kilianza?
2. Kama uhakiki ndio ulioanza, nini kilichotutoa kwenye hoja ya uhakiki kama si vita hii?
3. Kama uhakiki ulianza na mtuhumiwa HAKUHAKIKIWA kama mtumishi anayelipwa kwa kodi za umma, nadhani
Sasa yeye ndiye alitutoa kwenye uhakiki sisi tunamrudisha huko. Kwamba tumalize moja ndipo tuhamie pengine.
4. Ingekuwa mmoja wa ile kamisheni au kamishna mwenyewe anatuhumiwa basi tungehusianisha kwamba hawa waso na haya wanataka kuivunja nguvu tume hii. Sasa huyu hata hahusiki, hayumo kwenye tume, hivi mnamhusishaje? Au uhusiano ni neno lenye tafsiri ipi labda?

5. Mtasema kawataja, je alikuwa ameshawamaliza wote ndio useme sasa wamemlipizia, au kuna ambao hata kwenye list hawajafika? Je kama kawamaliza kamisheni ina kazi gani? Kwa nini vita isingeishia pale badala yake wakakabidhiwa wahusika?
6. UHAKIKI ulinuia KUBORESHA utumishi wa umma, kwamba mhusika wa nafasi fulani awepo kihalali. Uhalali wake katika nafasi hiyo unampa nguvu ya kutekeleza majukumu yake. Hivyo vita ya dawa za kulevya inapaswa kufanywa na wale walioko kihalali kwa maana ya nafasi zao kiutumishi, ndio maana ya kuwepo kwa kamisheni iliyo halali kisheria na kiutendaji.

Labda niishie hapa. Kama kuna hojaji nyingine tuzione.
UHAKIKI NI HOJA YA KWANZA KUBORESHA UTUMISHI WA UMMA. VITA DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA INAENDELEA NDIO MAANA KUNA KAMISHENI. VITA HAIJAISHA! NA UHAKIKI VILE VILE HAUJAISHA.

(Cop & paste)
 
Maneno meeengi... sisi tunataka vyeti tu.

Mnataka uongozi na hamna vyeti??.... What do you expect??
 
Back
Top Bottom