Vita Dhidi ya Dawa Za Kulevya: Makonda Anapaswa Kuhojiwa!

HIVI kama mtuhumiwa ni msambazaji na muuzaji tu, yaani yeye hatumii akienda kwa Mkemia mkuu wa serikali watapima nini?????

hiii movie imishaharibika waagizaji wataachwa na badala yake watakamata watazamaji tu (yaani watumiaji wa madawa)

wanayanunua wapi?
 
Biashara yako imeharibiwa kwa kiasi gani??

maana majuzi hapa, mlijificha kila kona, mkahama mji..... le mnajifanya eti Makonda katibua tibua

kwani siku zote mlikua wapi?

halafu unajua sana hayo mambo
I am sorry, naomba nikupuuze tafadhali!!!
 
HIVI kama mtuhumiwa ni msambazaji na muuzaji tu, yaani yeye hatumii akienda kwa Mkemia mkuu wa serikali watapima nini?????

hiii movie imishaharibika waagizaji wataachwa na badala yake watakamata watazamaji tu (yaani watumiaji wa madawa)
Na hao wapo kibao tu... wao ni wauzaji lakini hata kuonja hawaonji! Sana sana wanakuwa na testers!!
 
Pole sana kama unaona yote sawa!!! Kama unadhani kutoa taarifa kwa media wakati mtu ameshakamatwa ni sawa na kuitisha press conference with live tv coverage wakati mtu mwenyewe hujui hata ni wapi alipo basi itoshe tu kusema kwamba una kazi kubwa ya kutetea ujinga!!
Watu wengi hawafahamu kuwa nadharia husikika vizuri lakini hali halisi inataka uzoefu! Uzoefu umeonyesha kuwa kukamatana kimya kimya huishia kuachiana kimya kimya! Drug dealers hawaogopi kufahamika maana tayari wanafahamika! Wanachoogopa ni kutajwa hadharani! Ndio maana baada ya zoezi la kuwataja kusitishwa sasa wanaweza kupata usingizi! Na huo ndo mwisho wa effective war on drugs!
 
Samahani kwa hilo, sasa unataka tuelewe ambcho hukukiandika hapo awali? Hebu rudia ulicho andika hapo awali na hiki nilichokoti sasa. Vina fanana?

Na washawasha!
Na ndio maana nikakumbia huelewi!! Ninataka uelewe ambacho sikuandika wakati tangu mwanzo nimeandika:
Mwaka 2013 kuna "Mchungaji" alikamatwa na 40 kg za heroine kule Tegeta lakini Nzowa aligoma kabisa kumtaja kwa kile alichosema ingeharibu uchunguzi!!! "Mchungaji” huyo alikamatwa na raia wawili wa kigeni.
Sijaandika hapo kwamba "ALIKAMATWA?!!" Angalia post #2 ambayo MWALLA ameni-quote kama hujaona hilo neno "alikamatwa...!" Kuonesha kwamba lipo tangu mwanzo ili usije kusema nime-edit!!

Yaani, ingawaje tayari alikuwa ameshakamatwa lakini bado Nzowa aligoma kutaja ni nani amekamatwa contrary na sasa ambapo kabla wahusika hawajatiwa nguvuni; wanaanza kupiga mayowe kwamba XYZ wanahusika na dawa za kulevya as a result wakienda hawakuti kitu!!!
 
Watu wengi hawafahamu kuwa nadharia husikika vizuri lakini hali halisi inataka uzoefu! Uzoefu umeonyesha kuwa kukamatana kimya kimya huishia kuachiana kimya kimya! Drug dealers hawaogopi kufahamika maana tayari wanafahamika! Wanachoogopa ni kutajwa hadharani! Ndio maana baada ya zoezi la kuwataja kusitishwa sasa wanaweza kupata usingizi! Na huo ndo mwisho wa effective war on drugs!
Miongoni mwa wale waliotajwa ni wangapi unawafahamu?! Eti wanaogopa kutajwa!!! Hivi kwa akili yako huko mitaani kwao ambako ndiko hasa wanafahamika unadhani hawafahamu kwamba hao ni drug dealers au unadhani wenyewe hawafahamu kwamba watu wanaowafahamu wanafahamu kwamba wao ni drug dealers!!

Kinyume chake, ukimtangaza ni nani atakayemfahamu zaidi ya wale wanaowafahamu tangia zamani?! Ukichukua ile orodha ya episode 2; ni wangapi uliwafahamu baada ya kuwa wametajwa kama si kwamba umewafahamu wale ambao ni public figures ambao imeonesha sio drug dealers?!

By the way, pamoja na kupiga kelele kila mahali tena kwa kutumia live coverage; ni wangapi walikamatwa na bado wameachiwa?! Hiyo ya kusema wanaachiwa kimya kimya is your assumption na wala ushahidi huna lakini kuna ushahidi kwa 800% kwamba hata hao waliotajwa kwa mayowe, wapo walioachiwa na wengine wengi wataendelea kuachiwa kwa sababu hakuna ushahidi!!

But on top of that; si mnatuambia kwamba serikali ya sasa haitaki ujinga ujinga?! Sasa kwanini wahofie watu kuachiwa?! Kulikuwa na sababu gani ya ku-risk ushahidi wakati wanajua wao kama wao si watu wa mchezo mchezo na katu kuachiwa kimya kimya hakutakuwepo?!!!
 
Watu wengi hawafahamu kuwa nadharia husikika vizuri lakini hali halisi inataka uzoefu! Uzoefu umeonyesha kuwa kukamatana kimya kimya huishia kuachiana kimya kimya! Drug dealers hawaogopi kufahamika maana tayari wanafahamika! Wanachoogopa ni kutajwa hadharani! Ndio maana baada ya zoezi la kuwataja kusitishwa sasa wanaweza kupata usingizi! Na huo ndo mwisho wa effective war on drugs!

wengi hawajui hili

hao polisi wanawajua, wabunge wanawajua na kila siku wanakaa nao na wanapewa hela za uchaguzi

dawa yao ilikuwa ni ile sindano tu! Tangaza, ni operation ukiwa msafi rudi nyumbani kama mchafu unabaki

kuwa wataficha, wanaficha hata zoezi likiwa la kimya kimya, wataficha tu

kuwa kuna watu wanaonewa, sawa sawa, hali ni mbaya na tunaswaga waliokuwemo na wasiokuwemo!!

madawa ni sumu, sijaona ustaarabu wa ku deal na mtu mwenye sumu!!
 
Hakuna Alie Msafi % kubwa hata wale walio lisimamia hili swala kidete Huenda wakawa wanahusika kwa njia moja au nyingine! Ila kwakua Mpini wameshika wao Inabidi wengine wawewapole tu..!
LISEMWALO LIPO.. NA KAMA HALIPO BASI LAJA..!
 
Rehab rehab rehab...chidi njoo umchukue mwenzio huku
Ignored.png
 
msaada jamani...inakuwa worst feeling kama unamfahamu, mkuu haunijui sikujui, how is that feeling becomes worst to me!

nani kakupa laptop, una misuse resources mkuu,

kuna rehab iko kigamboni, uko wapi nije kukubeba? kiroho safi mkuu, nitagharamia
Ignored.png
 
Let’s dump all cra'ps and get down to the nitty-gritty!! Paul Makonda amevurunda kwa kiasi kikubwa issue ya mihadarati!

Tuweke kwanza pembeni masuala ya bangi na tujikite kwenye cocaine na heroine!

Jana Kamanda Simon Sirrro ameripotiwa akisema waliokamatwa hadi hivi sasa ni watu 349 na pipi 601 za heroine na cocaine zimekamatwa!!

Endapo hizo pipi zingekamatwa toka kwa Punda wanaomeza mzigo; pipi 601 ni almost 6 kg zinazoweza kubebwa na punda 6 pekee... maximum 10 unless kama unatumia amateurs!!

Remember, Punda wanaomeza mzigo wanawafanyia kazi SME Drug Dealers kwa maana ndio wanatumia hiyo njia!! Drug Dealers wa ukweli washaachana na hivi vipipi ambavyo vinaongeza risk kwa sababu, ONLY 50 Kg utahitaji angalau Punda 50 kama utataka kusafirisha kwa mara moja!!

Kinyume chake, wana-opt kusafirisha mzigo mzima mara moja... wakikamatwa; wamekamatwa na wakitoboa wanakuwa wametoboa kweli kweli!

Kwahiyo ni kichekesho kama sio kiroja kutamba huku na kule kwamba vita dhidi ya dawa za kulevya imepamba moto wakati mihadarati iliyokamatwa ni equivalent to Punda 6!!

Punda 6 wanaweza kupatikana kwenye kata moja tu ya Wilaya ya Temeke ambayo ni chamtoto mbele ya Kinondoni linapokuja suala la idadi ya Punda! Kwa Magomeni, Punda 6 unaweza kuwapata kwenye mtaa mmoja tu!!

Mwaka 2012 Maureen Lyumba alikamatwa na 210 kg za heroine! 210 kg ni equivalent to Punda 200 waliokamatwa na mzigo red-handed compared na equivalent to Punda 6 waliokamatwa hivi sasa!!

Hapo hapo kwa Maureen, uchunguzi ulionesha Drug Baron anayehusika na mzigo ni Shikuba... watu hawakupiga makelele!!!

Ingawaje Shikuba alichoropoka na kukimbilia Afrika Kusini lakini waliendelea kumuwinda kimya kimya hadi walipomdaka miaka 2 baadae pale airport (Dar) wakati akitokea SA!!

Bila shaka kwa staili hii ya Makonda, angeitisha Press Conference na kuanza "Yulee drug baron anayefahamika hadi na serikali ya Marekani tumepata taarifa anakuja kutokea South Afrika! Tumeshawaambia Uhamiaji na askari wa airport ili akitia pua tu; akamatwe!!!"

Hicho ndicho alifanya kwenye episode 1 !! Makonda alitangaza hadharani kwamba kuna mtu wanamlia mingo pale airport na anatokea China na mzigo wa kutosha!!

Ni mpumbavu gani angeendelea na saafari hata baada ya kuwa ameambiwa tunakusubiri airport?!!!

Mwaka 2013 kuna "Mchungaji" alikamatwa na 40 kg za heroine kule Tegeta lakini Nzowa aligoma kabisa kumtaja kwa kile alichosema ingeharibu uchunguzi!!! "Mchungaji” huyo alikamatwa na raia wawili wa kigeni.

Hata hao raia wawili, Nzowa aligoma kuwataja!!!

Mwaka juzi (Early november 2015) wakati watu wapo kwenye shamra shamra na wengine kwenye maumivu ya uchaguzi mkuu; kuna Mchungaji raia wa Nigeria alihukumiwa kwenda jela miaka 30 na faini sh. 9 billion! Pamoja nae, kulikuwa na raia mwingine wa SA na mwingine wa Pakistani!

Huyu ilidaiwa alikamatwa Kunduchi kwa kukutwa na 80kg za heroine.... compare from 40 kg above!!

Now look... yule "Mchungaji" ambae Nzowa aligoma kumtaja mwaka 2013 alitokea Tegeta, alikuwa na raia wengine wa kigeni 2, alikutwa na 40 kg!!

Na yule aliyehukumiwa 2015 nae alikuwa ni "mchungaji", anatokea Kunduchi, alikuwa na raia 2 wa kigeni na mzigo 80 kg!!!

Ukiunganisha dots hapo utagundua kwamba yule ambae Nzowa aligoma kumtaja mwaka 2013 ndie yule yule aliehukumiwa 30 years mwaka 2015!!!

What if wangepiga kelele kwenye live tv coverage kwamba wamemkatama mchungaji so and so!!! Unadhani hizo additional 40 kg zingepatikana?!

Hapa si kwamba naupongeza uongozi wa Nzowa... hata nae alikuwa ni failure!! Lakini pamoja na yote hayo bado utaona ni namna gani pamoja na failure ya Nzowa lakini matukio yake machache yalikuwa na impact kubwa kuliko haya tunayoambiwa eti vita imepamba moto!!!

Hapa let's call a spade a spade!! Makonda ameharibu moja kwa moja what's so called vita dhidi ya dawa za kulevya!!! Na ninavyoona, anastahili kabisa kukamatwa na kuhojiwa ili kufahamu ikiwa alichofanya si kwamba alikusudia kutoa tahadhali kwa real drug barons ili wafiche ushahidi!!!

Na ni kutokana na hatua hii ya Makonda ndio maana Kamanda Sirro hana namna zaidi ya kwenda kuwapima watuhumiwa kwa Mkemia Mkuu! Anachukua huo uamuzi kwa sababu anafahamu hawatakuwa na kesi yenye ushahidi dhidi yao baada ya kuwa walishapewa muda wa kupoteza kabisa ushahidi!

Hivyo, ni bora kwa Kamishina Sirro awapate japo na kesi ya kutumia dawa za kulevya ili ionekane vita vinapamba kasi kuliko kuwaachia mamoja!!!!

Na hapa utaona kwamba wale wanaomuunga mkono Makonda wanatetea wauza mihadarati wakubwa kwa sababu wanafahamu kwa staili yake hii hawatapatikana na hatia kinyume na wanavyotaka tuamini!!
Well said. Pia napenda kuuluza hivi mtu anaetumia madawa ya kulevya anabanwa na sheria gani? kama hivo kwanini enzi za baba yetu JK alimpokea Ray c na kumsaidia ili aokoke na madawa ya kulevya? kama alikuwa amefanya makosa kisheria kwanini hakufunguliwa mashtaka kama ambavyo sasa hivi inafanyika?
 
Well said. Pia napenda kuuluza hivi mtu anaetumia madawa ya kulevya anabanwa na sheria gani? kama hivo kwanini enzi za baba yetu JK alimpokea Ray c na kumsaidia ili aokoke na madawa ya kulevya? kama alikuwa amefanya makosa kisheria kwanini hakufunguliwa mashtaka kama ambavyo sasa hivi inafanyika?
Dah! Sijaipitai sheria ya mwaka 2015 lakini ambayo ilikuwa inatamalaki mtumiaji nae anayo hatia!

First scenario ni pale mtu anakamatwa kabisa na dawa za kulevya lakini kutokana na udogo wa kiasi kilichokamatwa, inashawishi kuamini kwamba hicho ni kwa matumizi binafsi na sio kuuza! Wakati mwingine sheria inaweza kukutaka uthibitishe kwamba unatumia mwenyewe!

Katika mazingira kama hayo, mtuhumiwa anaweza kuhukumiwa kwenda jela (nadhani 5 years) au faini ya vilaki kadhaa!!!

Kwa upande mwingine, kutokana na vile Hakimu anavyomuona mtuhimiwa; anaweza kuamua kwamba huyu badala ya kufungwa basi apelekwe sober house ili akapate tiba na sio kumfunga! Kwa mfano, yule Chid Benzi wa sasa hata ukimpiga faini ya laki 3 sidhani kama anaweza kulipa! Lakini kutokana na jinsi alivyoathirika sana, kushindwa kwake kulipa hakuwezi kumfanya hakimu ampeleke jela bali anaweza ku-opt apelekwe sober house!!!! Hapo ndipo linapoingia suala mtu kama Ray C wa JK! Yule hata kama angekuwa amefikishwa mahakamani, bado kuna uwezekano hakimu akitoa hukumu ya yeye kupelekwa sober house.
 
Vita hii ushindi wake haupimwi kwa punda waliokamatwa. Vita hii ushindi wake ni kitimtim na kimuyemuye wanachopata wauza unga. Hao mapapa kwa kipindi hiki hawatapitisha mzigo.
Mimi binasfi sikufurahishwa na kukatwa kwa spidi ya Makonda. Kuweka mambo hadharani kuliwatoa sana upepo madila wa unga.
Sasa huyu Sianga sioni chochote atakachofanya ambacho hakijafanywa miaka ya nyuma bila ya mafanikio.
 
Back
Top Bottom