Vita dhidi ya dawa za kulevya inapogeuka uchochoro wa kuwapa watu umaarufu

Uncle Jei Jei

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
1,684
2,157
Nami naomba nitie neno katika vita dhidi ya kutokomeza dawa za kulevya

Ki uhalisia hakuna mtu mwenye mapenzi mema na jamii inayomzunguka anayeweza kukubaliana na uuzaji wa dawa hizi hatari

DSM ndio kitovu cha nchi hii kiasi kwamba kwa asilimia kubwa kila kitu, kiwe kizuri au kibaya kinaanzia dsm ndio maana sishangai moto wa vita hii kukolezwa kuanzia dsm na leo tunaona mikoa mingine inafuata japo kwa namna tofauti.

Kinachonishangaza mimi kama uncle Jei Jei, ni kitendo cha kuwapa watu umaarufu katika vitu haramu hivyo vita nzima kugeuka kichekesho na kuonekana kuwa watu wazima wanafanya masikhara katika mambo ya hatari

Tangu wiki iliyopita vyombo vingi vya habari vinamtaja Makonda, tukisema lengo lake lilikuwa kujiongezea umaarufu tutakuwa tumekosea!?

Ni kweli kuwa hajui kama hana mamlaka ya kuwataja watu hadharani bila vidhibiti!?

Ni kweli kuwa hajui kama hana mamlaka ya kumuita mtu polisi!?

Sasa tukisema alikuwa anatafuta kuendelea kutajwa na vyombo vya habari kwa sababu siku chache nyuma hadi watu walimmisi!?

Leo hadi Gwajima naye aliyekuwa kimya kwa muda kaibuka, Manji ambaye huenda watu walikuwa hawamsemi semi naye kajaa midomoni mwa watu, huku sio kutafuta umaarufu kweli!?

Leo kina TID hawaishi kumtembelea na kumtaja brother Makonda, hatuoni kweli kwamba alihisi umaarufu unashuka!?

Wasaidizi wake wa karibu ni wakuu wa wilaya, cha ajabu katika vita hii hatuwaoni luningani!!

Vita ya muhimu kama hii hutakiwi kuingiza mzaha kama wa brother Makonda!?!... Eti Rose wa Tabata, Uledi wa Mwananyamala, Makomeo,... Kweli Tabata nzima Kuna Rose mmoja tu!?

Huu ni mzaha na katika mzaha huu wenyewe wenye madawa yao wanaicheka nchi kwa kukubali kuchezeshwa shele na huyu kijana!! Yangu ni hayo!!
 
Nampongeza Makonda kwa uthubutu. Uthubutu wake umesababisha kuteuliwa kwa mhusika. Sasa naingojea orodha namba 3! Orodha hiyo huenda ikawakumba na wale waliodhani operation za Makonda zingewaacha salama.
 
Ushauri wako sasa
 
U

Ushauri wako sasa
Mamlaka husika (kikosi kazi cha kupambana na dawa za kulevya) kimpige stop huyu anayefanya mzaha kwa mambo serious kwani ki ukweli anavuruga vita halisi.

Baada ya hapo taasisi hiyo ipewe bajeti ya kutosha na kikosi kingine cha siri kiundwe kufuatilia kazi za kikosi kazi hicho
 
Sio vizuri kutafuta umaarufu kwa kuwachafua watu na kupoteza lengo la kutokomeza dawa levya
Siyo vizuri ndiyo,ila hiyo vizuri isiyoambatana na umaarufu ni ipi?Kuwa mwanafunzi bora,kuwa mchapakazi,kuwa mtiifu,mbunifu,nk vinaambatana na umaarufu.Hata ukiwa mlevi bora,mzinzi bora,mvuvi hodari,mkulima,yaani anything better itakupa umaarufu tu hata kama hupendi.
 
Nampongeza Makonda kwa uthubutu. Uthubutu wake umesababisha kuteuliwa kwa mhusika. Sasa naingojea orodha namba 3! Orodha hiyo huenda ikawakumba na wale waliodhani operation za Makonda zingewaacha salama.

udhubutu upi na wewe! umetoka usingizini nini? kuna madawa yaliyoripotiwa kukamatwa toka zoezi lenu lianze? muone ulivyokaa kishabiki eti nangoja orodha ya 3! hivi una akili wewe, waliotajwa wenyewe 90% hawajaripoti wewe bado unataka kutujazia watuhumiwa hewa.
 
Unahisi utatajwa kwenye orodha namba 3? Usiwe na wasiwasi, leo kazi inapata professional. Hiyo namba 3 na nyingine zijazo watashughulikiwa kimya kimya!
 
Back
Top Bottom