Vita dhidi ya COVID-19 tusitengeneze mashujaa ambao hakuna ulazima wa kufanya hivyo

Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
11,324
17,829
Hii habari ya yule wakili maarufu kwenye kesi zenye uhusiano na sanaa kuitwa kujieleza na pengine kufikishwa ubaoni kwa Pilato linaweza kutengeneza shujaa asiyetegemewa akageuka kuwa cheche ya moto (spark of fire) inayo subiriwa na wabaya wa wenye dhamana.

Kuna washindani wenu au watu wasiokubali jinsi mnavyotekeleza majukumu flani (hapo naomba ieleweke haimaanishi wasiokubali wapo sahihi), Hawa wapinzani wenu ambao nisingependa tuwaite adui wenu wanaweza kuwa wanasubiri kwa hamu kubwa itokee cheche moja muhimu kulipua moto mkubwa wa ghasia, hii niite cheche ya kuanzisha moto mbaya sana kuliko ule ulioteketeza na kuangamiza kabisa mji wa Roma (The Great Fire of Rome) enzi za mfalme (mtawala) Nero tarehe Julai 9, Mwaka wa 64 baada ya Daudi (July 9, 64 A.D).

Kwa historia maeneo yale anakotokea huyu mwanasheria na aliko fanya mazungumzo yaliyo pelekea kuitwa kuhojiwa ni sehemu ambayo siyo tulivu (unstable) sana kisiasa, kuna hitaji mtu mmoja tu wa kugeuka muhanga (martyr: somebody who is seeking attention to elicit sympathy from others / somebody who sacrifices) kisha kuanzisha jambo kubwa likasambaa kila kona.

Tuzingatie mazingira ya sasa ambayo huyu kirusi amegusa nyoyo za watu sana, na zile tuhuma zilizorushwa huko mitandaoni bado zipo mitaani zikiwa zimejenga hofu na hasira kwa baadhi ya familia za wahanga wa huduma za kuhifadhiwa wapendwa wao bila mikusanyiko tena katika mazingira ya jua kuzama. Waliorusha tuhuma siyo watu waliokosa kazi tu ambao kazi yao ya kusambaza habari inaweza kubezwa kirahisi sana na mambo yakasahaulika, athari za habari hizo zikafutika kimiujiza.

Kama ningepata nafasi ya kushauri wahusika ningeshauri hili jambo lingemalizwa kimya kimya sana bila purukushani za kwa Pilato, ikitokea bahati mbaya huyu mwanasheria akapatwa na cheche za kirusi cha COVID-19 akiwa chini ya uangalizi wa wenyeji wake waliomuita na kumpa sehemu ya kumpumzika kwa masaa kadhaa inaweza kuleta kelele mbaya sana. Si unajua mgeni akipatwa madhara ugenini mwenyeji anaangaliwa kwa jicho la tuhuma kwamba huenda alizembea kumtunza mgeni.

Kwa taarifa za vyombo vya habari huyu nguli wa sheria ameshapewa dhamana, Huu ni mwanzo mzuri sana na ningewaomba malizeni hili kwa njia ya busara ya hali ya juu. Saa nyingine kusamehe sio udhaifu bali ni kuonyesha ukomavu.

Nihitimishe sio kila ushauri ni wa kuchukuliwa hasa kama unatoka kwa mtu kama mimi ambae sijui mengi yaliyo nyuma ya pazia.
Kushauri pia siyo kosa kwa hivyo nisingetegemea mimi kuwa mkosaji kwa kutoa ushauri kama huu.
 
Huko kwingine kuna mkusanyiko wakati wa kumuaga jaji mstaafu Ramadhani. Nadhani bado hatujaelewa somo la kuji-isolate, hatujaelewa kabisa. Worse enough, JK, Jaji mkuu nk wapo.

 
Huko kwingine kuna mkusanyiko wakati wa kumuaga jaji mstaafu Ramadhani. Nadhani bado hatujaelewa somo la kuji-isolate, hatujaelewa kabisa. Worse enough, JK, Jaji mkuu nk wapo.


Ahsante, Maoni yako ni muhimu.
 
Back
Top Bottom