Vita dhidi ya Corona: Wanaoadhirika au kuumia zaidi ni masikini ilihali ugonjwa wenyewe unawaumiza zaidi matajiri

Trubarg

JF-Expert Member
Jan 8, 2020
697
1,000
IMG_20200329_173225.JPG

Ukiangakia kwa umakini mapambano yanayoendelea duniani utagundua kwamba wanaoumia zaidi ni masikini au hohe hahe.

Angalia tukio lililotokea pale Kenya waliothirika kwa kipigo ni masikini ambao wengi wao walikua wanatoka kwenye miangaiko ya kujitafutia chakula chao na cha watoto.

Kuna usemi unasema 'IT IS VERY EASY TO PUNISH THE POOR' na ndiyo hichi nachokiona.
Tukiangalia walioathirika zaidi na ugonjwa huu kwa kuangalia takwimu hasa kwa nchi za africa mashariki utagundua kwamba wengi wa wagonjwa si watu wa kawaida ambao wanakula stick kila siku mitaani.

Wengi wao ni wale ambao walitoka nje ya nchi au kukutana na watu waliotoka nchi zenye maambukizi na hivyo kuwaletea masikini ambao leo hii wanaadhibiwa na kulazimishwa kujifungia ndani.

Tuangalie hii video hapa chini inaonyesha askari wakiwaadhibu watu huko india na utagundua ni watu wa aina gani wanaadhirika
 
Top Bottom