Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,013
- 144,371
Katika kupambana na corona,naishauri serikali kupeleka muswaada Bungeni katika Bunge linaloendelea kwa hati ya dharura,muswaada ambao ukiwa sheria, utataka kila sehemu(jengo la kibiashara,duka,n,k) ambapo watu huingia kupata huduma ni lazima kuwe na sanitizer au ndoo ya maji na sababuni na pia sheria itamke ni kosa kwa mtu kutonawa mikono na kuwe na adhabu ya faini kwa atakebainika kupuuza sheria hiyo.
Nashauri hivi kwasababu kuna sehemu hakuna huduma za watu kunawa miklono licha ya sehemu hizo kupokea watu wengi kwa wakati mmoja, na pia kuna madai(taarifa) kuwa baadhi ya watu wanakaidi kunawa mikono wanapotakiwa kufanya hivyo.
Kwenye masoko.japo ni vigumu sana,nashauri Halmashauri husika zichukue jukumu la kusambaza ndoo za maji na sabani katika njia zote za kuingilia na kutokea sokoni na mgambo wa Halmashauri wapewe jukumu la kusimamia watu kunawa mikono.
Kama tutaona gharama ya fedha ni muhimu kuliko afya zetu,ipo siku tutajua bila afya, hata hizo fedha hazina maana unless Mungu mwenyewe atatunusuru na hili janga.
Kama kila hatua itatushinda au tutaiona ni ngumu,basi tujiandae kushindwa na corona na kutengwa na mataifa mengine siku za baadae unless gonjwa hili hapa Bongo litatoweka kwa maombi kama tulivyoambiwa.