Vita dhidi ya corona mahusiano mabaya ya wafanya biashara na serikali

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
2,859
2,000
Katika pita pita yangu nikitafakari kwa kina kuna nini hasa kiasi yaliyo dhahiri yanafanywa uchuro na yaliyo uchuro kuhusu ugonjwa huu yanafanywa amali, nimegundua yafuatayo:

1. Makundi mengi ya wafanya biashara (yana gundu) yamebambikiwa viwango vikubwa zaidi vya kodi visivyoendana na biashara zao kwa mwaka huu wa 2020. Kwamba katika maeneo yote ya biashara, kwa mwaka huu kodi za mapato ya biashara zote zimepandishwa sana.

2. Kama alivyomweleza jiwe, king msukuma kwenye ule mkutano wa wafanya biashara kuhusiana na makadirio tata ya biashara, bambikizi hizi za kodi zimekamilika leo 31 March 2020.

Katika kipindi chote cha makadirio ya kodi, TRA kama kawaida yao wamefanya mavuno kweli kweli kupitia rushwa katika kipindi chote kilicho kamilika leo. Na wameneemeka kweli kweli.

3. Kodi zimepandishwa bila kujali mdororo wowote wa biashara ulioletwa na Corona, wala bila kujali mdororo huo utaendelea hadi lini. Hii ni kwa Tanzania tu ambako walipa kodi wake hufikiriwa kuwa "immune" kwa mazahama yoyote hata yawezekana mazito mazito ya kidunia kama corona.

Kwingine kote serikali zimekuja na stimulus packages za aina mbalimbali kusaidia biashara zao zisife ili pia ziendelee kutoa ajira.

Tanzania ng'ombe hukamuliwa hadi atoe damu au afe kabisa.

Kwa mwonekano wa hali ilivyo na hii pandisha pandisha ya kodi, kwa hakika serikali ya Tanzania haijaathirika kwa vyovyote kimapato na Corona bali imechukua wasaa huo kikamilifu kujinufaisha kweli kweli.

Ni aibu kubwa kuwa kuna institution yoyote kuwa ati kwa namna yoyote iko kwenye kunufaika kwa namna yoyote katika kipindi hiki cha ugonjwa huu.

Kwa hakika, kwa hali ilivyo mtaani, ni wazi kuwa pana ukakasi wa kutosha baina ya wafanya biashara na serikali. Kinyume na sehemu zingine ambako wafanya biashara na serikali wameshikana mikono kuona jamii zao zinavuka athari zinazoletwa na ugonjwa huu kwa salama kadri inavyowezekana.

Yale yale ya matetemeko ya Kagera.

Ama kweli jasiri haachi asili.
 
Bushloiaz

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
585
500
Hapo ccm haitawali kote,siku nchi nzima ni ccm hakuna rangi tutaacha kuona.CCM ni shetani.
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
2,859
2,000
Sasa ni dhahiri kuwa kumbe suala la hii kodi ya March 31 ndiyo ilikuwa agenda ya siri kwa serikali kutokuchukua hatua thabiti kuhusiana na ugonjwa huu kabla.

Maisha yaliyoanza kupotea na yatakayopotea kutokana na kuchelewa mno kwa hatua hizo itabidi kufanyiwa tathmini.

Hii ikiwa na pamoja na kiasi cha maambukizi zaidi ambacho kingaliweza kuzuilika.

Kumbe maisha ya binadamu haitakuwa na umuhimu sana kulinganisha na hii kodi.

Pia kumbe kwingine wakati serikali zinatoa relief mbali mbali kuwawezesha wananchi wao kujikimu kwenye kipindi hiki kigumu mno, sisi yetu iko busy kuwakamua wananchi wake vilivyo ili kujineemesha.

March 31 imepita naambiwa nyingine itakuwa due June 30. Hali ikiwa bado hivi hivi watakuwapo kuyaona.

Serikali yetu iko kimaslahi zaidi maisha ya watu wake baadaye.
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
2,859
2,000
Mkuu kodi gani imepandishwa na kwa asilimia ngapi? (Nimeshalipa kiasi NILICHOJIKADIRIA 31/03/2020)
Sijakupata hapo. Umelipa ulichokadiria? Wewe ni mfanyakazi TRA bila shaka. Kwa hoja zilizopo pia mmevuna kweli kweli. Sijui mwaziitaje huku. Wenzenu wanaita za kubrashia viatu.

Niliowasikia wamekadiriwa kwa mbinde na rushwa wamelipa na vitisho kutokwenda kwa Brigedia Mbungo wamepewa.

Yale yale ya King Msukuma.
 
RRONDO

JF-Expert Member
Jan 3, 2010
39,606
2,000
Sijakupata hapo. Umelipa ulichokadiria? Wewe ni mfanyakazi TRA bila shaka. Kwa hoja zilizopo pia mmevuna kweli kweli. Sijui mwaziitaje huku. Wenzenu wanaita za kubrashia viatu.

Niliowasikia wamekadiriwa kwa mbinde na rushwa wamelipa na vitisho kutokwenda kwa Mbungo wamepewa.

Yale yale ya King Msukuma.
Ni wazi hujui taratibu za kodi za Tz. Kodi za robo mwaka mfanyabiashara anajikadiria na kama nilivyosema mimi nishalipa NILICHOJIKADIRIA. Naomba useme kodi ipi iliopandishwa na ni kwa asilimia ngapi.
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
2,859
2,000
Ni wazi hujui taratibu za kodi za Tz. Kodi za robo mwaka mfanyabiashara anajikadiria na kama nilivyosema mimi nishalipa NILICHOJIKADIRIA. Naomba useme kodi ipi iliopandishwa na ni kwa asilimia ngapi.
Wewe utashindwa vipi kuzijua taratibu za TRA wakati ni mfanyakazi kazi huko?

Mada hii imekuchoma moja kwa moja siyo?

Yasemekana mmevuna sana na vya kwenu kwenye hilo duru la bambikizi kuhalalisha na vya kwenu.
 
amu

JF-Expert Member
Aug 8, 2012
13,417
2,000
Mkuu kunywa maji upumzike.
Mambo ya kodi huyajui.
Sijakupata hapo. Umelipa ulichokadiria? Wewe ni mfanyakazi TRA bila shaka. Kwa hoja zilizopo pia mmevuna kweli kweli. Sijui mwaziitaje huku. Wenzenu wanaita za kubrashia viatu.

Niliowasikia wamekadiriwa kwa mbinde na rushwa wamelipa na vitisho kutokwenda kwa Brigedia Mbungo wamepewa.

Yale yale ya King Msukuma.
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
2,859
2,000
Mkuu kunywa maji upumzike.
Ni wazi mambo ya kodi huyajui.
Ni kweli mkuu. Siwezi kuyajua kama nyie mnaofanya kazi TRA.

Ila kumbukeni nafasi zenu kuingia mbinguni kama watoza ushuru zilivyo finyu.

Mbungo asipowatembelea Mungu anawaona.

Katika pita pita yangu kugundua haya, ni wazi kuwa pia mnachukiwa sana labda kuliko askari wa usalama barabarani.

Ni heri mkajitathimini kabla ya hatari. Usawa huu wa Corona kumbe nyie mna yenu?
 
amu

JF-Expert Member
Aug 8, 2012
13,417
2,000
Ni kweli mkuu. Haiwezi kuyajua kama nyie wafanya kazi wa TRA.

Ila kumbukeni nafasi zenu kuingia mbinguni kama watoza ushauri zilivyo finyu.

Mbungo asipowatembelea Mungu anawaona.
Kunywa maji boss.
Tena ya moto hakikisha umeweka na kipande cha ndimu.
Inasaidia mambo mengi sana halafu itabidi usome walau vitu basic vinavyohusu kodi za mfanyabiashara.
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
2,859
2,000
Kunywa maji boss.
Tena ya moto hakikisha umeweka na kipande cha ndimu.
Inasaidia mambo mengi sana halafu itabidi usome walau vitu basic vinavyohusu kodi za mfanyabiashara.
Mkuu tuko kwenye Corona ngoja tutafute (uhai) survival kwanza. Kutuvuta kwenda kwenye masomo ya kodi ni kututaka kutoka kwenye mada.

Mkuu jikite kwenye mada Corona inaua.
 
RRONDO

JF-Expert Member
Jan 3, 2010
39,606
2,000
Wewe utashindwa vipi kuzijua taratibu za TRA wakati ni mfanyakazi kazi huko?

Mada hii imekuchoma moja kwa moja siyo?

Yasemekana mmevuna sana na vya kwenu kwenye hilo duru la bambikizi kuhalalisha na vya kwenu.
Pole sana. Siku ingine usiandike usivyovijua.
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
2,859
2,000
Pole sana. Siku ingine usiandike usivyovijua.
Mkuu vipi, bandiko limewafichua? Nia haikuwa kuwafichua lakini. Lengo lilikuwa ni Corona, nyie mmekuwa collateral tu inavyoonyesha. Ngoja tumalizane na Corona kwanza kuna taarifa nyingi za kufuatilia kuhusu nyie.

Kwa tabia zenu za tamaa na njaa zenu hizi mnazoendekeza mithili ya fisi maji, tunachagua kumalizana na Corona kwanza tutawarejea.

Wala msijaribu kututisha. Tuna uhakika Mbungo atasikiliza hata kama hatachukua hatua.

Kukujibu kabla ya kuniuliza, sisi ni wananchi wa nchi hii ambao tungependa kuona hatuwi wahanga wa janga hili la Corona kizembe zembe. Janga tulilokuwa tunaweza kujikinga nalo kwa maamuzi sahihi tu.

Stay tuned.
 
FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
19,733
2,000
Aisee income Tax ya 2020 imepandishwa juu mno, lakini mwisho wa siku huu mzigo itabidi abebeshwe mlaji wa mwisho, hakuna mfanya biashara atakaekubali hasara, faida kwake ni lazima, hata kama ni kidogo lakini faida ni lazima.
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
2,859
2,000
Kuna nafasi ya kazi?
Mkuu umefanya vyema kumwuliza usipofanya hivyo atajua vipi kuwa ungependa kulitumikia taifa kwa uadilifu mkubwa, hususan katika kitengo hiki?

Wanasema gonga mlango - utafunguliwa.
 
FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
19,733
2,000
Sasa ni dhahiri kuwa kumbe suala la hii kodi ya March 31 ndiyo ilikuwa agenda ya siri kwa serikali kutokuchukua hatua thabiti kuhusiana na ugonjwa huu kabla.

Maisha yaliyoanza kupotea na yatakayopotea kutokana na kuchelewa mno kwa hatua hizo itabidi kufanyiwa tathmini.

Hii ikiwa na pamoja na kiasi cha maambukizi zaidi ambacho kingaliweza kuzuilika.

Kumbe maisha ya binadamu haitakuwa na umuhimu sana kulinganisha na hii kodi.

Pia kumbe kwingine wakati serikali zinatoa relief mbali mbali kuwawezesha wananchi wao kujikimu kwenye kipindi hiki kigumu mno, sisi yetu iko busy kuwakamua wananchi wake vilivyo ili kujineemesha.

March 31 imepita naambiwa nyingine itakuwa due June 30. Hali ikiwa bado hivi hivi watakuwapo kuyaona.

Serikali yetu iko kimaslahi zaidi maisha ya watu wake baadaye.
Na hiyo kodi ya June 30 ndio muhimu zaidi kwao kuliko hii ya 31st March, hawawezi kuiacha iende hivihivi, wataendesha vipi nchi?
 
Top Bottom