Vita anayopigana Rais Samia ni kubwa sana katika ujenzi wa Taifa letu, tukeshe tukimuombea

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,225
9,654
Ndugu zangu Watanzania,

Rais wetu mama Samia suluhu Hassani kipenzi Cha watanzania na chaguo la watanzania anapigana Vita Kali Sana,vita ya kiuchumi, Vita ya kuinua maisha ya watanzania, vita ya kutokomeza umaskini wa kipato,ujinga na maradhi, Vita dhidi ya Rushwa na ufisadi, Vita ya kupunguza na kukomesha vifo vya mama na mtoto,Vita ya kuleta haki katika Taifa letu na kuhakikisha kila mtu anatenda haki,kutendewa haki na kuwatendea haki watanzania, Vita ya kuondoa Giza na kuleta nuru , Tabasamu na matumaini katika maisha ya watu, Vita ya kuwafuta machozi walioumizwa kwa namna yoyote Ile, Vita ya kuhakikisha uchumi wetu unakuwa mikononi mwa Mtanzania.

Ni Vita Kali, Ni Vita inayohitaji ujasiri, ushupavu na umadhubuti,Ni vita ya kuwanyang'anya tonge na Ulaji baadhi ya watu wanaojiona kuwa nchi hii Ni Yao, Wana haki kuliko wengine, wanastahili kupata na kupewa chochote wanachokihitaji kutoka popote na kwa yoyote yule, siyo Vita ndogo ni Vita kubwa Sana aipiganayo Rais wetu, Ni Vita inayotuhusu watanzania wote, Ni Vita inayotutaka watanzania wote wazalendo kusimama imara na Rais wetu mpendwa, Ni Vita inayotutaka kumuombea Rais wetu wakati wote.

Ni Vita inayotutaka watanzania kuwa ngao ya Rais wetu na mama yetu mama Samia, ni Vita inayotutaka watanzania kuwa wakali na mbogo na wachungu kwa yeyote atakayeonyesha kutaka kumkwamisha au kumhujumu Rais wetu katika kuliongoza Taifa letu.

Ni Vita ambayo watanzania hatupaswi kumuacha mpweke Rais wetu,lazima tumpe faraja na kumtia moyo Rais wetu,lazima tuonyeshe kumuunga mkono na kuwa Naye, lazima tufahamu kuwa anapigana kwa ajili yetu wenyewe na hivyo Hatuna budi kuwa upande wake.

Watanzania lazima tufahamu ya kuwa Kuna watu wanakesha wakiomba Rais Samia asifanikiwe na Wala hawafurahishwi na maendeleo makubwa na mafanikio makubwa yaliyopatikana katika uongozi wake ndani ya muda mfupi, kuna watu wanomba kila Siku mabaya yatupate ya kiuchumi ili ionekane Rais wetu ameshindwa kazi.

Maombi Yao hayafanikiwi na Dua zao hazizai matunda kwa kuwa Mwenyezi MUNGU ndiye aliyemuinua Rais Samia na kumpatia kibali Cha uongozi ,Mungu ndiye anayeendelea kumpa njia na maarifa ya kuliongoza Taifa letu,maombi ya Watanzania Ni mengi na makubwa katika kumuombea heri Rais wetu na mama yetu wa kipekee kabisa katika Taifa letu.

Tusichoke kumuombea Rais wetu,tusiache kumuunga mkono Rais wetu,maana hata maadui zake na wa Taifa letu wanatambua ya kuwa nguvu ya watanzania iliyo nyuma yake katika kumpigania Rais Samia na kumuunga mkono Ni kubwa Sana, hiyo ndio inayowapa hofu,ndio inayowapa homa kali sana.

Rais wetu na mama yetu mama Samia songa mbele, usiteteleke Wala kuteteleshwa, Watanzania tupo pamoja na wewe,tunakuunga mkono na kukuombea kwa Mwenyezi Mungu wakati wote ili akujalie Afya njema na nguvu za Kuendelea kututumikia watanzania, hukujiinua kwa mikono yako Mwenyewe kufika hapo ulipo fika kiuongozi Bali Ni kwa mipango ya Mwenyezi MUNGU aliyetuumba sisi wanadamu, hivyo mwana Damu yeyote hawezi kukushusha au kukukwamisha kwa kuwa Mungu yupo pamoja nawe. na uwepo wake upo kwako Rais wetu na Taifa letu kwa ujumla wake, utulivu na Amani hii iliyotamalaki hapa nchini Ni ishara ya uwepo wa mkono na uso wa Mwenyezi MUNGU katika Taifa letu.

Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627
 
Huyo mama anatuharibia nchi apumzike tu Sasa.

Hakuna jambo la maana linaloendelea kwa Sasa.

Ubadhirifu upo kila mahali.

Hiyo ndio vita iliyopo.

Uharibifu wa nchi.
Lakini pesa zi zipo, kama pesa zipo we shida yako nini?
 
Mjinga ni wewe,ombea mama yako aliye kuzaa achana na mama za watu
Watanzania wazalendo tutaendelea kumwombea Rais wetu Afya njema na nguvu za Kuendelea kututumikia watanzania,Tunakuwa kuwa mpo wachache Aina yako msiofurahishwa na kazi njema na ya kutukuka inayofanywa na mh Rais wetu katika kuliongoza Taifa letu
 
Wanafunzi wakamwambia Yesu " Mwalimu tufundishe kuomba"

Yesu akawaambia, semeni;

Baba Yetu uliye mbinguni Jina lako litukuzwe, Ufalme wako Uje Mapenzi Yako yatimizwe hapa Duniani kama yanavyotimizwa mbinguni, Utupe leo riziki Yetu Utusamehe makosa Yetu kama na Sisi tunavyowasamehe Waliotukosea Usitutie majaribuni lakini utuokoe na yule mwovu

Kwa kuwa Ufalme ni wako na Nguvu na Utukufu hata Milele, amen.
 
Back
Top Bottom