#COVID19 Visions & Trends Readings: Unaweza Usiamini Hili, "Namuona Baba Askofu Mpinga Chanjo, Ukichanjwa Chanjo ya Corona!"

Amekosea huyu na kukubaliana naye ktk mawazo hayo ni kukubaliana na mawazo ya kishirikina...

Paschal Mayalla anamjadili Bishop Rev. Josephat Gwajima huku akiwa hamfahamu vizuri...

Huyu Mchungaji akisimamia kitu anachokiamini, kamwe hawezi ku - back down na kamwe hawezi kurudi nyuma wala kusujudu mashetani na mipango yao...!
Imani yako imekuzidi kimo. Akili yako inataka kufika kikomo cha kujiaminisha Gwajiuno ni mungu' wako hapa duniani.

Yule ni 'tapeli mwerevu' kwa muda sasa, siku zake zipo mashakani !!
 
Pengo alifariki au alistaafu?? kwahiyo kustaafu naturally ni sababu ya vita na Gwajima??

Mfano Gwajima alisema Lowassa lazima awe Rais na CCM ila baada ya uchaguzi akamkana??

Alisema hana imani na CCM kabisa kipindi JPM amekua Rais. Akasema hana shida na JPM ila ana shida na CCM tena akliita "Hili lidude". But akagombea ubunge kupitia CCM huo msimamo wake ni upi??

Alisema katiba mpya ni muhimu enzi hizo 2014 lakini toka ameingia CCM ameufyata huo ndio msimamo???

Alisema yye ni mkubwa kuliko Rais au mbunge so hawezi gombea but amekua mbunge. Je huo ndio msimamo??

Gwajima ni tapeli kupitia mgongo wa dini, iko siku ataumbuka tu maana huwezi kumfool Mungu miaka yote tu. His time is coming!!
1. Kila jambo halitokei unless some conditions are fulfilled...

2. Mtumishi wa Mungu yeyote kukutamkia baraka wewe, haina maana kuwa inashuka tu kama mana toka mbinguni. Ni lazima ufanye kitu kwa upande wako maana Mungu anakuwa amefanya yanayomhusu...

3. Lowassa kutokuwa Rais. Sina hakika kama Rev. Bishop Josephat Gwajima alitumia neno " LAZIMA" unless ulete proof. Hata kama, lakini kama hakufanya yaliyompasa kufanya kwa upande wake angewezaje kuwa Rais..?

4. Kutokuwa na imani na CCM na mengine kama hayo na kisha yeye mwenyewe kawa CCM mpaka sasa...

Kutokuwa na imani na mtu au kitu maana yake ni mtu huyo au kitu hicho kushindwa kukupa unachotaka. Jawabu lake ni kukiacha au kukitupa kitu hicho maana hakina faida kwako..

Rev. Bishop Josephat Gwajima yuko CCM sasa ku - accomplish mission hiyo japo wengi hawaelewi na wanamwona kama an opportunist fulani tu..

5.Mwisho, tunazungumzia mambo haya in spiritual perspectives zaidi kwa kiasi kikubwa. Polycarp Pengo kuondoka ktk nafasi yake ya mamlaka ya utawala wa kidini ndiyo kufa mwenyewe huko. Makonda hayuko kwenye active politics, amekufa kisiasa huyo..!!
 
Uthibitisho wa Bi Mkubwa kwamba chanjo ni salama, na haina madhara:

1. Mimi ni Mama
2. Mimi ni Mke
3. Nina Watoto
4. Nina Wajukuu
5. Mimi ni Rais
6. Mimi ni Mkuu wa Nchi & Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi Yote
7. Nishawahi kupewa chanjo ya magonjwa mengine zamani
8. Kama ugonjwa wa korona umemkumba ndugu au jamaa yako wa karibu, lazima utakuwa na mtazamo tofauti kuhusu chanjo
9. Niko tayari kuchanjwa
10. Siwadanganyi Watanzania

^Brigedia, hapa tumepigwa!!!^ ~ JPM
yan na mimi nmeshangaa ndo uthibitisho eti daah.Mungu tunusuru
 
Ukimsikiliza Askofu Ngwajima neno kwa neno, sentensi kwa sentensi utagundua kwamba mtumishi hakatai chanjo ila anawaamsha watu na serikali kuhusu umuhimu wa kuweka utaalamu mbele katika maamuzi makubwa.
Ndio maana ukiangalia hoja zake inatakiwa ajibiwe na wataalamu kitaalamu Sasa bahati mbaya viongozi wetu wao wanachojua ni kutumia mabavu na nguvu kiufupi bwana Askofu anawakilisha mitazamo ya watanzania wengi ndio maana chanjo karibu zaidi millioni moja lakini mpaka sasa licha ya kutumia nguvu hatujafikisha watu laki tano waliochanjwa kulinganisha na idadi ya watanzania wote karibu 60m kitu ambacho ni cha kutafakari sana hasa kwa wataalamu, viongozi na serikali kwa ujumla.
Kwa hiyo ni wake up call kwa Tanzania kuwa tutumie wataalamu ili kupata matokeo badala ya kutengemea kauli za mtu au watu ambao sio wataalamu ie mwendazake na baadhi ya viongozi ambao wengine ni wataalamu ila kwa unafiki tu suala la corona waliliweka kisiasa zaidi na ndio matokeo ya tunachokiona Sasa. Kuanzia madam prezdent,makamu wake, waziri mkuu na baraza lake hasa waziri wa afya na naibu wake, viongozi wa taasisi za afya na taasisi zingine ambao hawakusema ukweli juu ya hatua zilizokua zinachukuliwa wakati wa mwendazake juu ya janga la corona wamepoteza moral authority ya kuhamasisha mbinu za kitaalamu na kisayansi kupambana na corona. Watanzania tuache unafiki na kuabudu viongozi hasa wanapokua wanakosea tuambiane ukweli.
Najua mtaji wa serikali na CCM ni ujinga wa watanzania lakini kwenye mambo muhimu viongozi na wanaCCM wajitahidi kuweka siasa pembeni.
 
Gwajima hana msimamo na anatafta kiki kwa hii ya chanjo kuipima serikali hata mimi naamini atachoma chanjo, ka alisema kuwa ubunge si hadhi yake na sasa ni mbunge wa ccm, ka alikataa clip ya yule mrembo na kusema ni mkono wa baunsa, na Jana kakubali kuwa mrembo hakuwa na shida, I do believe chanjo atachoma tu huyu, na atatunga uongo mwingine wa kuhadaa wale nyumbu wake
 
Gwajima tu anashughlisha nchi nzima vp ingekuwa kama huko kwa wenzetu tungekuwa na hadi madaktari wenye kupinga chanjo hali ingekuaje?
 
Gwajima hana msimamo na anatafta kiki kwa hii ya chanjo kuipima serikali hata mimi naamini atachoma chanjo, ka alisema kuwa ubunge si hadhi yake na sasa ni mbunge wa ccm, ka alikataa clip ya yule mrembo na kusema ni mkono wa baunsa, na Jana kakubali kuwa mrembo hakuwa na shida, I do believe chanjo atachoma tu huyu, na atatunga uongo mwingine wa kuhadaa wale nyumbu wake
Akiona sababu ya kuchanjwa na kuamua kuchanjwa si shida ila itakuwa ajabu mtu ambaye hadi sasa hajaona umuhimu wa kujikinga na corona hata kwa kuvaa barakoa tu aibuke kwenda kuchanja bila sababu.
 
Back
Top Bottom