Visasi Vya nini Serikalini? Mwogopeni Mungu na fahamu kwamba siku moja MTALALA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Visasi Vya nini Serikalini? Mwogopeni Mungu na fahamu kwamba siku moja MTALALA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mapambano Yetu, Aug 16, 2012.

 1. Mapambano Yetu

  Mapambano Yetu JF-Expert Member

  #1
  Aug 16, 2012
  Joined: Aug 14, 2012
  Messages: 936
  Likes Received: 960
  Trophy Points: 180
  *Mh. Sita aliruhusu mijadala ya wazi, mmojawapo ukamwomdoa ALIYETUNUKIWA (u)waziri mkuu mstaafu. Ngoma ilichezwa kwa mbwembwe zote lakini matokeo yake Sita akalipwa fadhila kwa kuhitaji spika mwanamke.
  *Mh. Mwakyembe aliongoza kamati iliyojipa jina la wapambanaji dhidi ya ufisadi. fadhila yake ni kile kilichompeleka india (hakutaka kuweka wazi mwenyewe bali kupitia midomo ya maswahiba wake kama Mh. Sita)
  *Dr. Ulimboka akasimama kutetea matibabu bora kwa watanzania kwa kudai maslai bora na maboresho ya maeneo ya kazi. fadhila yake, akapelekwa mstuni akang'olewa meno na kucha bila praizi. (ikumbukwe msitu huo umehusishwa kuwa eneo litumiwalo na wanaojiita wanausalama kutekeleza maovu yao)
  *Walimu wakaamua kudai maslai bora. Matokeo yake ni kuondolewa kwenye zoezi la kuhesabu sensa, kutishwa kuondolewa ukuu wa shule, mwalim mkuu na wengine kuhamishiwa vijijini.
  *Mh. Lema akasimama kuwatetea watanzania na watu wa jimbo lake (arusha). fadhila yake ni kile kinachodaiwa kuwa ni shinikizo kutoka kwa bosi na watu wake wa usalama kumdhulum haki yake.


  Hiyo ni mifano michache sana, mingi ipo hasa katika vyombo vya usalama. Mwanausalama tena aliyeshika wadhifa mkubwa serikalini anauawa hadharani na wauaji wanaachwa huru kutanua na kula bata(msemo wa kileo)
  1.Wana JF tafakarini na mnisaidie kunielewesha wapi tunaelekea.
  2. Hivi hawa wanaotekeleza haya yote wanajua kuwa ipo siku watarudi mavumbini?
  3. Makanisani na misikitini kwa nini watumishi wa MUNGU msilaani na kuhubili mjukwaani juu ya maswala
  haya?
  NAOMBA KUWASILISHA
   
 2. B

  Bahati Risiki JF-Expert Member

  #2
  Aug 16, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 531
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tanzania ya kikwete imejaa visasi. Na mbaya zaidi kuna watu wananyanyaswa kufa na hayupo wa kuwatetea. Mfano mzuri sana ni watoto wetu wanaoranda mitaa kwa kukosa elimu bora. Wazee wetu wanakufa mahospitalini kwa kukosa huduma bora na vifaa vya matibabu. Ndugu zetu wanaosotea magerezani kwa makosa yaliyotendwa na mapolis na usalama wa taifa. Kweli ndugu zanguni kilio cha hawa watu wetu kinaliangamiza taifa letu mchana wa jua. Tunajidai kusingizia wanyonge huku wakubwa wakitanua na haki zao. Wote tutakufa na tutajibu mbele ya Mungu yale tuliyotenda tena kwa makusudi tukijineemesha wenyewe na kuua wanyonge!
   
 3. m

  majebere JF-Expert Member

  #3
  Aug 16, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,520
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  Hizi ni propaganda za CDM, mtaani wamesha choka na kelele zenu mnakuja kujaza server ya JF na propaganda za kipumbavu. Nyie juweni kuwa mtabaki wapinzani milele na mtabaki na kulia lia tu.
   
 4. MATESLAA

  MATESLAA JF-Expert Member

  #4
  Aug 16, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,252
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  aiseeee baba yangu watu wanajadili mambo ya maana unasema cdm kwahio unataka mabaya yasiweke ,,,,utakuwa wamwisho darasani mpaka unakwenda kaburini wewe na kizazi chako
   
 5. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #5
  Aug 16, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  ni wapi katika mada, chama kimetajwa? una uhakika gani kuwa ni mtu/mfuasi wa "CDM"? una guarantee ipi kusema "CDM" watabaki wapinzani milele? pamoja na hoja na sababu za msingi za mtoa hoja(unaona ni propaganda)? halafu hata kama ingekuwa kweli jifunze kumkosoa mtu na si kwa matusi, adabu na heshima viwepo! hayo ni maoni na mtazamo kama hupendi mkosoe kwa hoja?
   
 6. Mapambano Yetu

  Mapambano Yetu JF-Expert Member

  #6
  Aug 16, 2012
  Joined: Aug 14, 2012
  Messages: 936
  Likes Received: 960
  Trophy Points: 180
  siku yenu ipo. fikilia kama hayo yote akifanyiwa mzazi wako, ndugu, mtoto, rafiki au wewe mwenyewe.
   
 7. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #7
  Aug 16, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  nafikiri mungu ashasahau kama kuna nchi inaitwa BONGOLAND
   
Loading...