sirluta
JF-Expert Member
- Nov 28, 2012
- 6,325
- 2,487
Habari wadau,
Kama mtakumbuka miaka ya nyuma kidogo, wasichana wa kazi za nyumbani walikuwa wanajituma na walikuwa waaminifu tofauti na sasa zaidi ya 90% ya wasichana wa kazi za nyumbani ni wale wenye matatizo mbali mbali yakiwemo ya kifamilia ama ya kimaisha. Lakini pia kwa miaka hii kumekuwa na uhitaji mkubwa wa wasichana hao lakini pia kumekuwa na mpenyezo mkubwa wa mawakala wa shetani wanaotumika katika familia zetu.
Kungekuwa na vituo vya redio vinavyoripoti visa mbalimbali vya mahousegirl hawa kama stori zinavyopigwa mitaani, nadhani kungekuwa na hofu kubwa kumwachia housegirl nyumba na mnaenda kazini.
Tupatie baadhi ya visa vya mahousegirl ulivyopata kuvisikia ama kuvishuhudia pande hizo kama hivi&
1. Kuna mmoja alikuwa anachapa kazi vizuri ila ikifika jioni muda wa kulala anatoweka, kumbe alikuwa anaenda kulala kwenye shimo kando ya mto, ilipokuja kugundulika anapolala na alipoulizwa, akasema akilala ndani bibi yake anamtokea usiku anamchapa sana.
2. Wengine wanasumbuliwa na mizimu ya bibi zao, hasa wa huko Tanga. Anaweza akafika kwako leo kuanza kazi, kesho yake anakuambia anahitajika kwao amekaa sana kwako!
3. Kuna mwingine alikuwa akiamka yeye na tv, tv na yeye labda umeme ukatike ndipo afanye kazi kidogo na alikuwa anataka bill ya maziwa asubuhi ya kwake, na bia mbili kila siku jioni! Hatare!
Yaani wanafanya mambo ya kusikitisha kiasi kwamba wameleta hofu. Wengine ni agent wa shetani, ukishamsanukia kwako, anajibadili sura anaingia chumba cha pili anaendelea kupiga kazi