Visababishi vya upungufu nguvu za kiume hizi hapa

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Ongezeko la wagonjwa wa saratani na tatizo la wanaume kupungukiwa nguvu za kiume kutokana na kula vyakula visivyochavusha mbegu kwenye miili yao kutokana na matumizi ya mazao yaliyolimwa bila kutumia kilimo hai.

Hayo yamebainishwa katika Mkutano na wandishi wa Habari kuhusu Mafunzo yaliyoandaliwa na Shirika la Kuendeleza Kilimo Hai Tanzania (TOAM) na mjumbe wa Bodi hiyo, Richard Mhina kuwa matumizi ya kemikali mbalimbali kwenye kilimo ni chanzo cha ongezeko la magonjwa mbalimbali ikiwemo kuchavusha mbegu za kiume.

Alisema matumizi hayo yamekuwa yakichangia saratani za aina mbalimbali pamoja na wanaume wengi kupunguziwa nguvu hali ambayo imeleta mtafaruku kwenye baadhi ya familia.

Alisema vyakula vinavyozalishwa kwa kutumia vimelea vya sumu kwa sababu ya mbolea na dawa za kuulia wadudu ndio sababu kila wakati kumeibuka changamoto mbalimbali za afya ikiwemo upungufu wa nguvu za kiume na magonjwa ikiwemo saratani.

Alisema Kilimo hai ni endelevu kwa vizazi vijavyo na siyo kuangalia wingi wa uzalishaji mazao bila ubora wa mazao na hifadhi ya ardhi pamoja na uchevushaji ni muhimu kwakuwa una manufaa makubwa ndani ya jamii.

Mshauri wa mawasiliano kuhusu kilimo hai, Constantine Akitanda alisema matimizi ya kilimo hai kuna faida nyingi ikiwemo kiafya kwani hakutakuwa na kemikali yeyote kwenye mazao.

Alisema kilimo hicho kinaweza kufanyika kwa kupanda mazao mchanganyiko, kupumzika mashamba pamoja na kutumia dawa asili kufukuza wadudu mfano harufu ya kitunguu, pilipili na nyinginezo na siyo kuwaua kwani kila kiumbe kina umuimu wake kwenye ardhi.

Alisema wakati sasa umefika kwa wanahabari kutumia karamu zao kuelimisha jamii njia sahihi za kuhimiza kilimo hai ambacho halina madhara kwa maendeleo endelevu bila kuchosha ardhi.

Akitanda aliongeza kuwa,ipo Mikoa kadhaa imeathirika na upuliziaji dawa za kuua wadudu kwenye mazao ambapo Mkoa wa Ruvuma inaongoza kwa kupata athari itokanayo na upuliziaji dawa kwenye mazao

Alisema hadi sasa kuna jumla ya wazalishaji 250, 000 waliokidhi viwango vya uzalishaji wa kilimo hai na kupata masoko hususan katika, zao la kahawa ambalo lililolimwa kwa kilimo hai ni dola kumi kwa kilo huku kahawa ikiwa ni dola mbili.

Chanzo: Habari Leo
 
Kila mtu anakuja Na justification za nguvu za kiume kutangaza biashara yake. Haya wazee WA organic farming tumewasikia, lakini naomba data za kupungukiwa nguvu za kiume Kati ya nchi zinazotumia GMO produces tulinganishe Na kwetu hapa.
 
Mpaka sasa ukiniambia sababu 3 kuu za hili janga ntakujibu ni:

1.Sedentary Lifestyle
2.High Fats Consumption
3.High Sugar Consumption

Hii ni kwa ukubwa wa elimu na utashi nilionao juu ya maswala kama hayo.
 
Back
Top Bottom