Visa vya Uchawi na Ushirikina Mkoani Kigoma Mwisho wa Reli

Huwezi kupewa kidono kama huna kinkuti.hizi dawa huenda sambamba lakini ni za wakongomani(wabembe)
Kinkuti ni dawa iliyokuwa zamani sana ila kuanzia miaka ya sabini 70's ilianza kupotea na kubaki kidono pekee,hivyo uliweza kupewa kidono bila kinkuti na kwenye miaka ya hivi karibuni hata hicho kidono kwa kweli hakipo labda uvuke maji lakna si kwa huu mwambao wa hapa kwetu
 
We msenge inabidi siku moja ukutanishwe na nguli wa shughuli tu akuchukue maelezo kisha ndani ya week tu akubadilishie program za kwenye ubongo uanze kucheza na majalala tu!
Hahahah huyu hajakutana na makonki

Anajaribu tu kuushawishi ubongo wake

Ila moyoni anajua hizi mambo ni hatari
 
Kwahiyo wachawi wanaweza kila kitu isipokua kupata details na nywele za mtu?

Enyi mitanganyika mnakuaje mazwazwa kiasi cha kuhadaika kirahisi hivi.
Taja majina ysko matatu na ya mama yako mzazi watu wamalize mambo

We si unajifanya konki
 
Kigoma Visa vya Uchawi na Ushirikina.

Kigoma ni moja ya Mikoa ambayo inasifika kwa Uchawi nchini Tanzania. Huu mkoa kiasili una watu wachapa kazi sana. Si wazembe ukilinganisha na mikoa mingine yenye ushirikina kama Tanga,Pwani au Zanzibar.

Kigoma maeneo ambayo yanasifika sana kwa Uchawi ni Mwandiga, Ujiji,Mwamgongo n.k

Hapo Mwamgongo ni hatari sana karibu na Mbuga ya Gombe. Kunasifika na moja ya visa vya uchawi ni kimoja ambacho kilitokea mwaka 2020 ni kifo cha Diwani mmoja ambaye inasemekana alichukua Mke wa mtu.

Huyu Diwani ambaye allhamdulilah alikuwa na vijicent ilitokea akawa anatembea na mke wa raia mmoja kijijini hapo.

Yule bwana Raia alipata taarifa. Akanyamaza. Diwani akafikia hatua akaona aoe kabisa mke wa jamaa. Na mke akadai talaka ili akaolewe na Diwani.

Jamaa alimfuata Diwani na kumwambia kwa upole tu kuwa "Mheshimiwa najua unatembea na mke wangu, tafadhali usimwoe maana mimi ntapata shida kulea watoto hawa 6 nlio nao na nina mke mwingine. Uwe na uhusiano naye lakini usimuoe"

Diwani alijibu kwa jeuri tu kuwa "mkeo ndiye anayenilazimisha mzuie yeye siyo mimi"

Jamaa akamenda mpaka kwa viongozi wengine wa kijijini pale akitaka wakamsihi Diwani asimwoe mkewe. Diwani akakaza.

Mpaka jamaa akaenda kwa Rafiki mkubwa wa Diwani kumwomba amsihi rafiki yake asimwoe mkewe yeye atapata shida na watoto. Diwani akamtolea nje jamaa.

Basi jamaa akanyamaza. Siku moja Diwani akakutana na Jamaa Mitaa flani kuna Soko. Diwani akaanza mshambulia jamaa kwa maneno kuwa "nasikia unataka niroga..

Huniwezi,mimi mpaka kufika kuwa Diwani nmetoka mbali sana..." Akaendelea mbele na kumwambia haya nakupa mate na nyayo hii chukua." Akatema mate. Jamaa alimwambia tu Diwani "huo uchawi wa kuchukua mate na nyayo ni mdogo sana,wa watu ambao ni underdog/amateur"

Akaondoka zake. Baada ya siku chache tu Diwani akaanza kuumwa sukari ikapanda mara akaanguka ndo basi tena. Akafa.

Akazikwa. Baada ya siku chache wanafamilia yake wakawa wanamwona Diwani anakuja anagonga pale kwao kuwa afunguliwe mlango anateswa sana.

Diwani alikuwa amevaa pensi chafu.anagonga dirishani akisema anachapwa sana viboko. Afunguliwe.

Mke na watoto wakawa nao wanajawa woga.

Hili tukio lilitokea Mkoani Kigoma mwisho wa Reli.

Na watu wa Kigoma tofauti na Mikoa ya Pwani. Pwani mchawi wako mnaweza mkawa mnacheka naye na kula naye huku anakuroga.

Kigoma ukikorofishana na mtu anakwambia kabisa bila kuuma uma maneno "nitakuroga" hata hatumii sauti ya vitisho. Anakuambia kwa upole tu akikuahidi kuwa kweli atakuroga mbele za watu wengine.na anaenda kukuroga kweli.

Hiki ni moja ya kisa cha mambo ya Uchawi Kigoma.nitaleta Visa vingine vya Uchawi na Ushirikina Kigoma.

Kisa Cha Pili
Kuna jamaa mmoja alikuwa ana tatizo dogo tu na jirani yake shambani. Akawa anasema migomba flani ni ya kwake. yule mzee akamwambia hapana hili shina la Mgomba lipo shambani kwangu. Jamaa mbabe akasema ni lake na atakata.

Kweli ule mgomba mmoja ukazaa. Siku hiyo jamaa akaenda shambani akachonga chonga majani ili akate ndizi. Kunyanyua panga. Mkono ulipigwa ganzi haukushuka. Ukabaki juu na panga.

Akapiga kelele sana maana mkono ukawa kama unanyongwa hivi. Watu wakamchukua kumpeleka kwake. Mkono ulipooza.
WAROMBO NI WACHAWI BALAA
 
Stori za kitaani. Na wengi wanaozianzishaga wanakuwa wagonjwa wa akili. Ukiwa mgonjwa wa akili kuna vitu unakuwa unaona au unahisi. Baadaye unaanza kusema ni uchawi. Huo mnaita uchawi ni mawenge yenu tu.
@Red Giant uchawi upo ,hayajakukuta tu
 
Sijui nani mjinga zaidi aliyekusimulia hiyo story ya kusadikika au wewe uliyeamini?

Kwa kuanzia tu tupe jina la huyo diwani maana udiwani ni ofisi ya umma na taarifa zao ni wazi kwa umma.

Nyie mitanganyika mijinga sana mnaamini sana story za ushirikina mkisimuliwa tu mnaamini kama zilivyo na nyie mnaenda kusimulia. Hakuna uchawi.
@Bufa uchawi upo hayajakukuta tu!!!
 
Nasikia eti hata yule jamaa aliyemnyang'anya Zito kabwe Jimbo lake pia tangu uchaguzi wa dhuruma uishe hajawahi kukanyaga bungeni ni mgonjwa mpaka leo tafadhali Kama kuna mtu anajua ukweli wa hii kitu atujuze
 
Nasikia eti hata yule jamaa aliyemnyang'anya Zito kabwe Jimbo lake pia tangu uchaguzi wa dhuruma uishe hajawahi kukanyaga bungeni ni mgonjwa mpaka leo tafadhali Kama kuna mtu anajua ukweli wa hii kitu atujuze
urongo tu kirumbe ng'enda yupo mzima wa afya na bungeni alichangia kumhusu gwajima
 
Uchawi ni nini?

Unajuaje huu uchawi na hiki ni kitu tu hujakijua lakini si uchawi?

Mfano, mtu ambaye haujui mchezo wa karata tatu, akioneshwa mchezo huo kwa mara ya kwanza, anaweza kuamini ni uchawi.

Au, tukimchukua babu wa babu wa babu wa babu yako aliyezaliwa miaka zaidi ya 140 iliyopita, ukamleta leo aone watu wanavyowasiliana kwa simu, ataona kama uchawi, wakati si uchawi, ni teknolojia tu ambayo hajaijua.

Sasa wewe hicho unachokiita uchawi unajuaje ni uchawi kweli na si karata tatu au kitu kingine usichokijua?
Au, tukimchukua babu wa babu wa babu wa babu yako aliyezaliwa miaka zaidi ya 140 iliyopita, ukamleta leo aone watu wanavyowasiliana kwa simu, ataona kama uchawi, wakati si uchawi, ni teknolojia tu ambayo hajaijua.

Kiranga nilikuwa sijawahi kushiriki mazishi ambayo baada ya miezi miwili marehemu akatolewa na waganga dukani kwa Kaka yake .KUMBE NI TEKNOLOJIA TU AMBAYO SIJAIJUA nilidhani ni uchawi.
 
Kinkuti ni dawa iliyokuwa zamani sana ila kuanzia miaka ya sabini 70's ilianza kupotea na kubaki kidono pekee,hivyo uliweza kupewa kidono bila kinkuti na kwenye miaka ya hivi karibuni hata hicho kidono kwa kweli hakipo labda uvuke maji lakna si kwa huu mwambao wa hapa kwetu
Kalya huko siwezi pata kinkuti
 
Kalya huko siwezi pata kinkuti
Kuanzia hiyo Kalya mpaka Kapalamsenga ni ngumu kuipata,miaka ya 2000 mwanzoni nilisikia labda maeneo ya Mwese ila napo ni kubahatisha
Shida kuu ni miiko yake inakinzana sana na hii modern Life hivyo kufanya hata waganga waogope kuitoa
 
Traffic huwa wahawakamati vijana bodaboda na probox wa ujiji,na huwa hawaendi ujiji wanaishiaga maweni tu.maana ujiji wabembe ni balaa,lakini kigoma wachawi ni watongwe wa ilagala na watu wa njia za maji) kama wanavyoita hao huku mwamgongo kalya mpaka ufipa.ila waha sio wachawi nao wanaogopa sana watongwe,wabembe na warundi.
Kiongozi hiyo kanda uliyoisema ina mengi ya kuogofya,kustaajabisha na kutafakarisha sana na kwa upande wangu mtu anapotokea kupingana na hayo ma miziziology huwa namsikiliza na kumsoma tuu kikubwa huwa natamani ningeishi na kukulia ktk hiyo jamii yake isiyokuwa na haya mazingaombwe
 
33 Reactions
Reply
Back
Top Bottom