Visa vya Mtanzania Halisi... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Visa vya Mtanzania Halisi...

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by zomba, Jul 14, 2011.

 1. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #1
  Jul 14, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Atasifu utajiri wa mwenzake hata kama anajuwa kuwa kaupata kwa njia zisizo halali.

  Atajisifu kuwa anamjuwa sana tajiri fulani ingawa alipishana nae tu njiani.

  Atajisifia kwa kumzidi akili mwajiri wake kuwa alimchapa elfu tano alipotumwa kitu cha elfu kumi (yeye akamwambia tajiri kanunua kwa elfu kumi na tano).

  Atajisifia kuwa anabadili mademu kila siku mara mbili. Akiamini kabisa huo ndio urijali.

  Atajisifia kuwa anatembea na mke wa mtu. Akiamini kabisa afanyavyo ni uhodari.

  ...endeleza, ntarudi baadae kuona visa vya Watanzania.
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Jul 14, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  yote tisa mimi huwa nabaki hoi na watu wanaojua
  mfano watu wote dar wanaomiliki magari aina ya vogue
  na wamenunua wapi,na shughuli wanazofanya,bei ya magari hayo..
  mambo yao ya ndani,skendo zao....

  huwa nabaki mdomo wazi..
  yaani too much useless information ipo kichwani mwa mtu...
  na yeye mwenyewe yuko hoi..
   
 3. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #3
  Jul 14, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  1. Unamwita mtu usiyemjua(wala kukutana nae kabla) aunt au ancle.

  2. Asilimia 90 ya CD pamoja na cassete za muziki ulizonazo nyumbani ni feki (sio original copies).

  3. Stoo yako imejaa vitu (makorokoro) kwa kuwa hutupi kwa kuamini kuwa ipo siku utayahitaji kwa mfano karpet ukilitoa hulitupi n.k.

  4. Una machupa ya maji matupu ya shampoo perfume pamoja na vipodozi vingine umeweka tuu wala huna shughuli navyo.

  5. Watoto wako wote wana majina ya utani mfano babu Ali, Cat, Mamu, Jose n.k.

  6. Hakuna mtu katika familia yako anayetoa taarifa kwako anapo kuja kukutembelea mfano kaka, shangazi n.k.

  7. Mikoba yako imejaa vitu kama vile vijiti vya kusafishia meno, tissue n.k ulivyochukua sehemu kama vile mgahawani.

  8. Mama yako anamigogoro na ndugu na hawazungumzi kwa muda wa siku 20 au zaidi.

  9. Hupigi simu isipokuwa katika muda ambao gharama za kupiga ni nafuu (mfano usiku sana )na mara nyingi huwa una beep tu… Bado utaangalia salio.

  10. Ulipokua mdogo nguo unazonunuliwa pamoja na viatu ni vikubwa mara mbili ili uweze kuvivaa muda mrefu zaidi.

  11. Wakati ukisafiri na ndege unabeba mzigo wa uzito mkubwa kuliko inavyoruhusiwa.

  12. Unapomsaidia mtu na akafanikiwa basi utakuwa unasema kama sio mimi asingekuwa vile yule

  13. Wale tunaowasaidia wengi wanakosa shukurani na badala yake wanasema, eti kaniletea kijisimu hiki, si hata hapa ningeweza kukipata? Ndio, zawadi ya Ulaya hii?! Halafu wanacheka!

  14. Hatuvai nguo nzuri au mpya na kujipamba tunapokuwa majumbani mwetu isipokuwa tunapokwenda maharusini, kwenye misa au kwenye mialiko ya futari au pale tunapoalikwa vyakula na marafiki!

  15. Ukiwa na kompyuta, basi asilimia 90 kama si 99 ya programu ulizonazo ni 'pirates' na hakuna 'genuine' hata moja.

  16. Rafiki yako anapokuwa na mgogoro na mpenzi wake unatamani kisiri-siri waachane ili umchukue shemeji yako, japo unajidai kuwapatanisha kwa bidii sana.

  17. Wakati ukisafiri japo unayo nauli kamili unatamani konda asahau kukudai ama umlipe pungufu ya nauli ya kawaida.

  18. Ualikwapo kwenye sherehe au mkutano ufika umechelewa badala ya muda ulopangwa kupita waweza zidisha hata masaa mawili mbele au zaidi.

  19. Kudhihirisha kama wewe mbongo ukimaliza kusoma hii utabisha kuwa haya si kweli.
   
 4. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #4
  Jul 14, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  -Kujibu swali kwa kuuliza swali.
   
Loading...