Visa vya chuki za kibaguzi Uingereza baada ya ushindi wa Brexit

MK254

JF-Expert Member
May 11, 2013
31,745
48,375
Watu wasiokua wenye asili ya Waingereza weupe wanapitia katika hali ngumu Uingereza. Hii ni baada ya kura ya maamuzi ambapo Waingereza wengi walionyesha kutaka waondoke kutoka kwenye muungano wa EU.

Wengi wa waliopiga kura ya kuondoka walielewa ina maanisha kwamba wageni wote wataondoka Uingereza na kuwaachia weupe wa huko nchi yao. Sasa imekua ni visa kila maeneo wengi wakiwakumbushia hao wageni waondoke mara moja, huku wakiwatusi na kejeli na dharau za kila aina. Kumekua hadi na visa vya wageni kupigwa kabisa.

Mkusanyo wa visa vyote huu hapa #PostRefRacism: Twitter documents appalling rise of post-Brexit racism
 
Hali ni mbaya sana.......
Public transport zimekuwa mwiba kwa wengi......hasa hapa mjini Bradford.......
 
Hali ni mbaya sana.......
Public transport zimekuwa mwiba kwa wengi......hasa hapa mjini Bradford.......

Mnapokwenda kwenye nchi za watu, siku zote muwe mnakumbuka nyumbani mlikotoka, hakikisha hadi hata kijijini hujavunja madaraja. Jihusishe na shughuli za watu wenu, hata kwa simu, wekeza nyumbani, tuma hela zihusike kwenye misiba, harusi n.k.

Jifunze kuongea kilugha chenu, wajulie hali bibi na babu, na wazee kijijini.

Muache hayo mambo ya USA baby, mara UK baby. Wakati hao wa huko wanaanza kuidai nchi yao, hutaamini ndio wale huwa mnacheka cheka nao. Binadamu ndivyo alivyo, mkatili na anaweza kukugeuzia kibao hadi ushangae.

Mimi hapa ni Kenya baby!!! kwenda mbele, daima Mkenya na naipenda sana nchi yangu na nitawekeza nyumbani siku zote, huko nje nakwenda kuchuma na kugeuza. Hata kwa mataifa majirani nawekeza tu juu kwa juu lakini akili zangu zipo nyumbani Kenya siku zote.
 
Mkuu MK254 naona umeamua "kuwapa live" bila chenga. Kuna mijitu imezamia nchi za watu kiasi kwamba hata makaburi ya wazazi na babu na bibi zao hawajui yalipo. Hii ni aibu kwamba mtu hajui mzazi wake alizikwa wapi!

Kaka, hamna haja ya kuwapaka kwa mgongo wa chupa, wanafaa kukumbushiwa kwamba huku ndiko walikotoka na ipo siku watakumbuka na kuja wakikimbia. Usije ukasahau nyumbani, hata iweje, hakikisha hata watoto wako mara kwa mara unawatembeza kijijini, kwa bibi, kwa mama, wajulie hali majirani, jihusishe kwenye kamati za mazishi, harusi nenda kanisani/msikitini.
Ongea kilugha, wafunze watoto kilugha na Kiswahili.

Mkirudi kule kwa USA baby, hakikisha haukomi kupiga simu, kutuma walau hata kama hela kidogo kijijini. Wekeza nyumbani.... Diaspora wetu mtanielewa siku moja, wameanza leo Waingereza na ndio kioo cha wazungu wengi. Yaani leo hii nenda kwenye forums zao, aisei matusi, wanarushiana vijembe, chuki full.
 
Nakusoma kwa uzuri Mkuu. Utakuta mtu kwa wazazi wake ni hapo Mtito Andei; mkewe kwao ni hapo Voi lakini akija Kenya anafikia Nairobi hotelini na kugeuza kurudi Europe au US na familia yake. Hii ni aibu sana ndugu yangu. Ushauri wako mzuri sana sana.
 
Hehehe!! Natumai wengi wanasoma na kupita kimya, hawatabisha maana ndio ukweli, na inawaingia. Cha msingi ujumbe unawafikia tu.
 
Back
Top Bottom