Visa Official Thread

Bavaria

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
53,102
53,352
Huu ni uzi rasmi wa kiTanzania wa kupeana michongo ya njia rahisi za kupata VISA za nchi mbalimbali duniani.

Pia uta-share experience yako taratibu ulizofuata hadi ukapata visa ya nchi yeyote. (Usiwe mchoyo mtu akikuomba ushauri).

Tutaelezana nchi ambazo Watanzania wanaweza kuingia bila visa, nchi ambazo unapata visa ukifika airport na nchi ambazo lazima uombe visa kwanza kabla hujaenda.

Karibuni.
 
Nilifikiri ushafikisha umri na status ya kupata Visa ya nchi yoyote
Kwani unajua umri na status yangu ? Yaani hata kupata visa ya kwenda tu hapo Kenya ni mtihani. Nisaidie jinsi ya kupata visa ya kwenda Australia jamani.
 
Jinsi ya kupata visa ya Australia.
Mimi nilienda Australia mji unaitwa perh. Nilienda kufanya kazi nikarudi. Visa ilikuwa rahisi kupata sasa sijui kwa sababu nilikuwa naenda fanya kazi. Kwanza kabisa nilituma maombi SA sababu TZ hamna ubalozi wa australia. Wakaninyima na kuniambia inabidi niombe visa kwenye nchi yangu au nchi karibu ya yangu. Nikajaza tena nikapeleka nairobi kwa njia ya DHL. wakaanza kuprocess na huku wakiniuliza maswali ya hapa na pale kwenye simu. Ila swali kubwa lilikuwa ni ulishawahi kusafiri nje ya africa? Nikawajibu no. Baada ya wiki wakanitumia kwenye email yangu elecronic visa. Australia wanajali sana unique professionalism.
 
Back
Top Bottom