Visa nilivyoshuhudia kwa ndugu yangu Mtaalam wa Tiba za Asili

Miaka ya zamani kulikuwa na mganga Ukerewe huko alikuwa na uwezo Mkubwa ila alikuwa anapenda pesa sana, alikuwa anauza wagonjwa kwa wachawi, pia usiku alikuwa anawakamata wachawi na kuwaomba hela au mifugo kwa kitisho kuwa mchawi asipompa pesa au mifugo kesho yake basi usiku huo angemgandisha alipomkuta na asubuhi ataonwa na watu
 
Jamani nina miaka mingi sijalog in huwa nasomaga tu ila huu uzi umenifanya nimelia sana acheni tu hii dunia.itoshe tu kusema nateseka lakini maombi yamenifunilia yalio sirini naonyeshwa kabisa anayenitesa. Ukiniona huwezi jua mateso nayopitishwa hapa nalia nitahadithia nikitulia
Pole sana ndugu. Usiache muomba Mungu... japo binadam tumeumbiwa kusahau na uvivu poa.
 
Jamani nina miaka mingi sijalog in huwa nasomaga tu ila huu uzi umenifanya nimelia sana acheni tu hii dunia.itoshe tu kusema nateseka lakini maombi yamenifunilia yalio sirini naonyeshwa kabisa anayenitesa. Ukiniona huwezi jua mateso nayopitishwa hapa nalia nitahadithia nikitulia
Hadithia basi
 
Kwa jinsi huu uzi umeenda viral, inaonyesha kuwa jamii zetu zinateseka sana na uchawi. Uchawi mbaya sana. Kwenye kila familia NAHISI lazima kuwe na hata mmoja aliyeteswa na uchawi. Mimi kakangu jamani almanusura awe kichaa.
Kuna mtu anaeenda kwa mganga ili kumloga mtu na kuna wachawi wenyewe. Ubaya unaweza kuta hata mchawi au mshiriki nae anacomment hapa kusikitikia hizi habari, kwasababu sifa zao kubwa ni UNAFIKI.
All in all, uchawi unatesa na kuumiza sana sio victim tu hata wale watu wakaribu na victim.
To God be the Glory
 
Mwaka 2011 nimemuuguza mzee..nikampeleka India..then South Africa kote huko kwa miezi minne mzee akawa bado hajapona natika kipindi chote hicho cha miezi minne hapati choo lakini anakula vizuri.. Hosp vipimo vikaonyesha kaoza kila kitu ndani(mapafu, utumbo, figo,) lakini mzee nk,mzima..

Dr mmoja kule South akaniiita chamber ..huyu jamaa nk, mtanzania ila anabeba box huko..tukaongea sana..akaniuliza sana historia ya mzee. Kisha akaniambia huku utapotEza hela mrudishe home mkaangalIe tiba za asili ..maradhi ya mzee sio ya kawaida.

Nikaarange safar tukarudi bongo..nikafikia Lugalo hosp..mzee akalazwa tena hapo.. muda wote huo nilikiwa siamini kama mzee karogwa..siku moja akaja rafiki yangu kunisalimia ila akaambatana na jamaa yake mmoja wakaja hadi hosp..kufika yule jamaa yake rafiki yangu alipomuona mzee akaguna kwa nguvu kiaha akatoka nje.. sikujali sana ila nikanote kitu..badae akarudi..akawa kimua mda wote..

Walipotoka nikawasindikiza kidogo jamaa yule akaniambia naomba bro naomba naomba namba yako nitakuchek..
Kesho yake akanicheki akaomba tuonane ..tukaonana..akaniambia mkuu wewe umekulia bongo hii.. asili yenu wapi..kwa kifupi akaniambia mbona pale baba hayupo kile ni kivuli.. yule sio mtu.. unauguza kitu kingine.. niliogopa sana.. akanishauri anipeleke kwa mdogo wake ni mtalam wa tiba asili..nikamtoa mzee hosp nikamuacha Bunju kwa bro..nikasepa Kigoma..

To cut thw story short ..mzee wangu alirogwa na kule kwa mtaalam nikaona chain nzima waliohusika na mganga akasema tumeshachelewa na mzee ..tar 14 Dec mzee akafa..nikapeleka Mwanza kwetu tukazika..baada ya siku mbili nikasafiri na kuondoka Mwanza kurudi Kigoma..nikakaa kule kwa wiki tatu..nikafanya jambo ambalo sikuwahi kulipanga katika maisha..KISASI KIKUU..

Niliemjulisha na anaejua jambo hili ni kaka yangu mkubwa tu.. wengine wote hadi kesho hawajui..
Wachawi washenzi sana..
 
Inaendelea....SEHEMU YA NNE

Huyu mke wa mganga nae ana majini nae ingawa hajishughulishi sana na mambo ya uganga zaidi ya kutumwa moto na vitu vidogo vidogo tena kwa kufanya kuitwa, ila siku hiyo majini yake yalikuja kwa uchungu baada ya kuona mganga amezidiwa.

Mke wa mganga akasema njia ya kumsaidia kaonyeshwa hivyo akaingia kilingeni na kuchukua dawa kadhaa za maduka ya dawa za asili na kuchanganya na dawa fulani ya kwenye tunguri na kuchanganya na unga wa sembe na kisha kumpaka mume wake baadhi ya sehemu na nyingine kumnywesha.

Baada ya muda akapata nafuu na kunyanyuka na hapo tukaanza kumcheka kuwa kawezwa, na yeye akacheka kidogo na kusema wale wamekuja kiume lakini moto ukokwe arudishe majibu muda huo huo.

Hapo tukafanya haraka kukoka moto na kuuweka katika chungu maalum anachokiita Bukhuri shari, akabadili nguo na kuvaa nyekundu tupu hadi kilemba na kuchukua tunguri yake ambayo ki umbo ni kubwa kuliko zote alizonazo na tunguri hiyo kipindi anaitengeneza nilikuwepo na ni mpya mwenyewe anaiamini sana.

Tunguri hii alipokuwa anaiunda alimchoma bundi aliyeuwawa na makunguru na majivu yake akachanganya unga wa mti uliopigwa na radi, mti wa nyumba ambayo ina maiti ndani, kisiki kinachokwaa watu njiani, mzizi uliokata njia, unga wa kichwa cha nyoka na vitu vingine pamoja na damu ya kuku wawili wa rangi maalum na ule ulimi wa tunguri pia ni miongoni mwa miti yenye siri kubwa kulingana na maelezo yake.

Naam kwa mara ya kwanza nikaona tunguri hiyo imeshikwa kwa jazba huku akiuelekea moto na kusema leo naua kuanzia walioshiriki na mpaka vilivyomo katika nyumba zao! Akaanza na kutia ubani na kusema na Waalim wake! "Enyi majini nimechokozwa kama mlivyoona, hamkunipa uganga nije niteseke...mmeniachisha shughuli zangu za maana mkanitia kichaa ili leo yanikute haya nife? Sasa leo naangamiza watu na kama mnaona huruma na kuona ni kufuru kaeni pembeni, niacheni na wakulungwa wa bara nitende malukazi....

Inaendelea....
Aisee kama yote haya umekariri we kiboko kabisa
🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom