Visa nilivyoshuhudia kwa ndugu yangu Mtaalam wa Tiba za Asili

Umethibitisha vp Kama ni mchawi? Au kwa sababu ni bibi (mzee) na anasali Sana.....
Alishawala wanae wanae watatu wa kiume, kabakiza mmoja tuu ambaye ni hohehahe.

Najua utauliza ulijuaje kama yeye ndio kahusika na vifo vyao, and the chain will go on

Kifupi ni kwamba uchawi upo ila kuuthibitisha huwa ni mtihani, hivyo acha maswali yasiyo na mbele wala nyuma.
Unforgetable
 
Kama kweli ungekuwa matured enough ungeandika story nzima pembeni baadae uiweke hapo. trends inaonyesha wengi wenye tabia kama zako mara naenda kula mara nimepitiwa na usingizi baadae wanaomba vocha n.k. Mimi ni mkongwe sana JF nadhani kuliko wewe na hii address ni ya pili mwanzo nilikuwa najiita FD pale JF ilipoanzishwa ambapo member wengi tulihamia toka Darhotwire. So naongea kutokana na uzoefu
Umeona eennhh???!!!
 
Inaendelea....SEHEMU YA NNE

Huyu mke wa mganga nae ana majini nae ingawa hajishughulishi sana na mambo ya uganga zaidi ya kutumwa moto na vitu vidogo vidogo tena kwa kufanya kuitwa, ila siku hiyo majini yake yalikuja kwa uchungu baada ya kuona mganga amezidiwa.

Mke wa mganga akasema njia ya kumsaidia kaonyeshwa hivyo akaingia kilingeni na kuchukua dawa kadhaa za maduka ya dawa za asili na kuchanganya na dawa fulani ya kwenye tunguri na kuchanganya na unga wa sembe na kisha kumpaka mume wake baadhi ya sehemu na nyingine kumnywesha.

Baada ya muda akapata nafuu na kunyanyuka na hapo tukaanza kumcheka kuwa kawezwa, na yeye akacheka kidogo na kusema wale wamekuja kiume lakini moto ukokwe arudishe majibu muda huo huo.

Hapo tukafanya haraka kukoka moto na kuuweka katika chungu maalum anachokiita Bukhuri shari, akabadili nguo na kuvaa nyekundu tupu hadi kilemba na kuchukua tunguri yake ambayo ki umbo ni kubwa kuliko zote alizonazo na tunguri hiyo kipindi anaitengeneza nilikuwepo na ni mpya mwenyewe anaiamini sana.

Tunguri hii alipokuwa anaiunda alimchoma bundi aliyeuwawa na makunguru na majivu yake akachanganya unga wa mti uliopigwa na radi, mti wa nyumba ambayo ina maiti ndani, kisiki kinachokwaa watu njiani, mzizi uliokata njia, unga wa kichwa cha nyoka na vitu vingine pamoja na damu ya kuku wawili wa rangi maalum na ule ulimi wa tunguri pia ni miongoni mwa miti yenye siri kubwa kulingana na maelezo yake.

Naam kwa mara ya kwanza nikaona tunguri hiyo imeshikwa kwa jazba huku akiuelekea moto na kusema leo naua kuanzia walioshiriki na mpaka vilivyomo katika nyumba zao! Akaanza na kutia ubani na kusema na Waalim wake! "Enyi majini nimechokozwa kama mlivyoona, hamkunipa uganga nije niteseke...mmeniachisha shughuli zangu za maana mkanitia kichaa ili leo yanikute haya nife? Sasa leo naangamiza watu na kama mnaona huruma na kuona ni kufuru kaeni pembeni, niacheni na wakulungwa wa bara nitende malukazi....

Inaendelea....
Mkuu muendelezo uni tag
 
Wakulugwa wa bara tunasema endelea na malukazi
 
Wachawi ni viumbe wa kuogopa kuna jamaa mwalimu madrasa amefungwa jela miaka thelathini, michongo wametoa wachawi wametengeza kesi ili ili aonekane kabaka tena wamemfanyia hayo baada ya kuwakatalia wachawi lengo lao yule ostadh akubali kila mwaka jamaa wapate kijana mmoja, Chanika hiyo.
 
Back
Top Bottom