Visa nilivyoshuhudia kwa ndugu yangu Mtaalam wa Tiba za Asili

Nilimuuliza swali hili hili, akanijibu angemtibia angekuwa kaanzisha vita kubwa wangeitana jeshi kupambana naye, naye hakuwa na sababu ya kupambana vita isiyomhusu. Akanipa kisa kilichomtokea miaka miwili kabla, aliletewa mgonjwa yani mke alimleta mume akiwa mgonjwa sana jamaa anadai akakaa pale anamtibia. Anasema kuna siku akaamka kama anaumwa yani kama kachanganyikiwa anagawa gawa nguo anatoa wosia kwa watoto wake, ilikuwa ijumaa. Anasema baadaye akaja kijana akamwambia anaitwa na mzee yuko kwenye gari kule chini. Alipoenda akaambiwa aingie kwenye gari, mzee kuingia akamkuta mzee flani.
Eti akamuuliza kwanini unataka kuniharibia kazi yangu, huyo ni mwanangu na mimi ndiye nataka kumtoa kwa ajili ya biashara zangu. Jamaa akamwambia ashakula pesa lazima amalize kazi, mzee akatoa chupa na glass nyuma ya kiti cha gari akamwekea maji akamwambia kunywa nijue kama unataka pambana nami au utaachana naye.
Jamaa akanywa nusu glass kumaanisha kuwa hataki shari, wakaachana, alivyofika kwake akamwambia yule mama na mme wake kuwa ugonjwa umemshinda hawezi kuutibu. baadaye akakusikia yule jamaa alifariki.
Noma sana.
Tupe kisa kingine mkuu.
 
Inaendelea.... SEHEMU YA PILI

Baada ya yule bibi kusema hayo akanyamaza akisubiri majibu ya upande wa pili.

Moyoni mwangu nilidhani rabda mganga atamfukuza yule mchawi au hata kugombana nae kutokana na hizo hila zake za kishenzi, ila kinyume chake mganga akatulia kidogo na kisha kumuuliza yule bibi, "unafanya hayo yote ili kuutumikia uchawi! Uchawi una faida gani?

Bibi akatabasamu na kujibu kwa hisia za furaha "baba uchawi una faida kubwa mno mwanangu kuzidi hata huo uganga wenu, mimi hapa nilipo nina pembe inakaa ziwani...inakusanya pesa za biashara za mji mzima kwa njia ya chumaulete, hebu fikiria ni wangapi ambao hawajazindika shughuli zao na wananichumia mimi? Bado sijagusia misekule ambao hunisaidia na kunizalishia mashambani kwangu.

Mganga akauliza tena kwa kama dharau fulani hivi, "sasa kama mna nyenzo hizo mbona mnakufa masikini na kuishi katika nyumba duni, kula yenu tu ni tabu achilia mbali mavazi yenu?

Ndugu msomaji, huyo bibi alikuwa amevaa khanga tofauti kuukuu na chini amekuja na ndala tofauti zilizoshonwa shonwa hivyo yale maongezi yake yalishangaza kidogo.

Safari hii bibi alicheka kwa kama kebehi na kumjibu mganga, "kumbe mwanangu bado wewe ni mtoto mdogo sana hujui kitu! Sisi fahari yetu siyo mchana ila ni usiku! Kwenye mwembe mkubwa kikaoni ndiyo utamjua tajiri ni nani kulingana tu na usafiri na zana za gharama atakazo ingia nazo...wapo wanaingia na ungo, wanaoingia na Fisi, wanaokuja kwa ufagio na ndege ya watu wengi nk na pia kuna watu wana pembe wamenunua zaidi ya milioni ishirini na hiyo ikiwekwa chini huioni na hata ukionyeshwa hutaweza kuinyanyua na uganga wako wote.

Najua nyinyi ufahari wenu ni makazi, mavazi na kula ila sisi raha yetu ipo sehemu tofauti kabisa na nikujuze tu usiku ni raha sana mwanangu na sasa nikipata hiki cheo nauelekea ukubwa sasa na kiti changu kitabebwa juu juu na katika mji nitaheshimika mno.

Maongezi yalifika mpaka muda wa magharibi na adhana ikalia...hapo yule bibi akasema naondoka nawahi kusali lakini ufanye hivyo nilivyokwambia au kama shida ni pesa nikupe mimi hilo fungu ulilopanga akupe bora tu usimuague.

Bibi wakati akisema hayo alifungua fundo kwenye nguo yake na kuonekana noti nyingi ambazo pengine zinaweza fika hata laki mbili au zaidi! Mganga akasema; sihitaji pesa ila nikuulize jambo? Sasa unakwenda kusali ili iweje ilihali wewe ni mchawi? Huoni unazidi kukufuru?

Bibi akasema huku kasimama anataka kuondoka "unapoingia katika uchawi masharti yake inatakiwa uvae kofia mbili, moja ya uchawi na nyingine ya Imani...hapa kwenye imani unaweza kushika dini sana uwe Mkristo, Muislam au dini yeyote na ukishindwa hilo basi kuwa na imani ya kupenda watu sana na kujitoa...hii inasaidia hata akitokea mtu mmoja akisema wewe ni mchawi, watatokea kumi watakao pingana nae na kuwa upande wako.

Mganga akasema kwa hasira; tafadhali ondoka usije ukadhurika, mimi ni mganga wa majini hivyo sirubuniwi na yeyote bali nawafuata wao walionipa uganga...ondoka haraka kabla sijachoma ubani ukapigwa na chini sasa hivi maana hawataki mambo machafu na ya kipumbavu namna hiyo!!!


NAENDELEA KUANDIKA HIVI NDUGU ZANGU...
 
Back
Top Bottom