Visa nilivyoshuhudia kwa ndugu yangu Mtaalam wa Tiba za Asili

Nimekufuatilia nimegundua upo smart. Yale maeneo yanayoleta maswali unakuja yatolea suluhisho kwenye story ndani kwa ndani hivyo unapitia mawazo ya watu na kuangalia wanakosoa wapi.

Then unakuja na kuweka kwenye story namna ambayo inajibu waswasi wao. Ni mwandishi makini. Unajua kutunga na ku twist story vizuri. Hii unaweza andikia kitabu.

Kuna mtu alisema wewe si mgeni wa huyo mganga mbona unaandika kama msaidizi. Haraka umekuja umejibu kuwa kweli ulienda kama ku prove so ikabidi uwe msaidizi wake... Napenda ulivyo mjanja.
We una kipolo kule naona unakosoa wenzako tu
 
Mchawi alikuja na mtu aliyemloga,mganga akaagiza vifaa, baadae akarudi Yule Bibi Mchawi peke yake kumueleza mganga asimtibie yule mgonjwa maana yeye ndio aliyemloga,Mganga Akashangaa na akaanza kuuliza hadi faida za kuwa mchawi?
Swali huyo Mganga aliona nn kwa mgonjwa? Kama alishindwa kumtambua yule bibi aliyemleta mgonjwa kama ndio mchawi uganga wake upo wapi? Na Huyo bibi Mchawi mwenye vyeo angerudi vp kutoa pesa kwa mganga ambaye alishindwa kumtambua mpaka ajitambulishe? Ukijibu tutaendelea
Yule bibi hakwenda kichawi!! Alienda pale kama mtu wa kawaida tu ndo maana. Mbona panajieleza tu mkuu?
 
Wajameni bongo kutoboa kama huna Mungu basi uwe na mganga sugu anayekufanyia manuva,yaani kijiji nilichokulia hapa kuna wanga balaa,huwezi amini mbaka kuna mama mmoja alikua ni mwinjilisti na kitaa aliheshimika kama mtumishi aisee mwaka juzi kadakwa sehemu live anawanga alienda kwa aliyemzidi nguvu daaa hata sikuamini ukimwona madhabahuni anahubiri utatamani akufanyie Sara ya toba kumbe yelewiiiiiii ni grade 1 night walker witch!
Mkuu nimeelewa sana hiyo night walker
Marehemu binamu yangu kuna siku alinambia "dogo trust nobody, suspect everybody" nadhani ndio alifundisha kaungalia movies za intelligence

Sent from my SM-G925F using JamiiForums mobile app
 
Mwaka 2011 nimemuuguza mzee..nikampeleka India..then South Africa kote huko kwa miezi minne mzee akawa bado hajapona natika kipindi chote hicho cha miezi minne hapati choo lakini anakula vizuri.. Hosp vipimo vikaonyesha kaoza kila kitu ndani(mapafu, utumbo, figo,) lakini mzee nk,mzima..

Dr mmoja kule South akaniiita chamber ..huyu jamaa nk, mtanzania ila anabeba box huko..tukaongea sana..akaniuliza sana historia ya mzee. Kisha akaniambia huku utapotEza hela mrudishe home mkaangalIe tiba za asili ..maradhi ya mzee sio ya kawaida.

Nikaarange safar tukarudi bongo..nikafikia Lugalo hosp..mzee akalazwa tena hapo.. muda wote huo nilikiwa siamini kama mzee karogwa..siku moja akaja rafiki yangu kunisalimia ila akaambatana na jamaa yake mmoja wakaja hadi hosp..kufika yule jamaa yake rafiki yangu alipomuona mzee akaguna kwa nguvu kiaha akatoka nje.. sikujali sana ila nikanote kitu..badae akarudi..akawa kimua mda wote..

Walipotoka nikawasindikiza kidogo jamaa yule akaniambia naomba bro naomba naomba namba yako nitakuchek..
Kesho yake akanicheki akaomba tuonane ..tukaonana..akaniambia mkuu wewe umekulia bongo hii.. asili yenu wapi..kwa kifupi akaniambia mbona pale baba hayupo kile ni kivuli.. yule sio mtu.. unauguza kitu kingine.. niliogopa sana.. akanishauri anipeleke kwa mdogo wake ni mtalam wa tiba asili..nikamtoa mzee hosp nikamuacha Bunju kwa bro..nikasepa Kigoma..

To cut thw story short ..mzee wangu alirogwa na kule kwa mtaalam nikaona chain nzima waliohusika na mganga akasema tumeshachelewa na mzee ..tar 14 Dec mzee akafa..nikapeleka Mwanza kwetu tukazika..baada ya siku mbili nikasafiri na kuondoka Mwanza kurudi Kigoma..nikakaa kule kwa wiki tatu..nikafanya jambo ambalo sikuwahi kulipanga katika maisha..KISASI KIKUU..

Niliemjulisha na anaejua jambo hili ni kaka yangu mkubwa tu.. wengine wote hadi kesho hawajui..
Wachawi washenzi sana..
Daaah..
Pole sana mkuu..
Tena sana.
 
Mkuu nimeelewa sana hiyo night walker
Marehemu binamu yangu kuna siku alinambia "dogo trust nobody, suspect everybody" nadhani ndio alifundisha kaungalia movies za intelligence

Sent from my SM-G925F using JamiiForums mobile app
Usimuamini yoyote kabisa
Kuna dogo ana hardware hapa kitaaa.
Alikua ana kaka zake wafaanya biashara ila kila wakimuomba mtaji wanamzungusha.
Kawatengeneza kaka zake wamefilisika kabisa.
Sasa hivi dogo ana pesa chafu...na hatak hata kuwaona.ni stor ndefu

Ila usiwaamin hata wa tumbo moja
 
Jaribu kufikiri mkuu..nimeuguza india mieiz miwili ..south miez minne..jula 6..lugalo wiki tatu. Na bado kumbe nilikiwa nauguza kitu kingine kisicho na uhai..mshua nimemwacha mwanza wanatamba nae na kumtesa kichawi..tumezika kitu kingine...familia imeyumba..imagine mkuu mzee katusomesha watoto wote 6 level ya masters..gafla kuanzia 2010 wakubwa zangu wakaanza kupoteza kaz na kusimamishwa..nikabaki peke yangu tena nadhan nilipona sababu nilikuwa nje..lakn wengine wote watano walipata shida kazini.. bado mzee wakamtenda jeur..
Kweli wahisika wamelipa garama ya matendo yao..
Daah..
So painful mkuu..
Hata mimi nisingesamehe ushenzi huu
 
Inaendelea.....SEHEMU YA SITA

Ndugu zangu nifafanue kidogo, nilikuwa siamini haya mambo hapo awali na jambo usipoliamini usilipinge bali tafuta ukweli wake kwa waliozama katika fani hiyo...naam ndivyo nilivyofanya na ndiyo maana nikawa karibu na nikawa ni mfano wa msaidizi au kwa lugha zao wanaita mwana maji na hapo ndipo nikajua mengi na sasa naamini sana uwepo wa nguvu hizi kwani pengine zingenitoa roho kama si Mungu mwenyewe.

Wakati yule kiumbe namfuata nilikuwa kama zezeta fulani au kama nipo kwenye ndoto ila naona kila kitu lakini mwili siwezi kujizuia hivyo nikafungua mlango na kumfuata huku yeye akiongoza mbele.

Kitendo cha kufungua mlango na kuuacha wazi ulirudi wenyewe na kujifunga kwa nguvu na hilo likaenda sambamba na mganga kupandisha ndani kwake na kutoka nje haraka huku akifuatwa na mkewe na ndipo walipokuja kunikuta nyuma ya uchochoro wa nyumba nikitembea kama zuzu! Hapo nikarudishwa na nilipokuja kuzinduka (nilipoteza fahamu) ndipo nikaambiwa nimeaguliwa sana ndiyo pona yangu lakini ilikuwa niende na maji na kwamba yule aliyekuja ni jini la kichawi limetumwa kunichukua mimi ili wakanipoteze na ameyafanya yote hayo chini ya uangalizi maalum wa wachawi wale wale wanaoona uchungu kuaguliwa kwa yule binti, alitakiwa aachwe afe!!

Nikauliza sasa mimi nahusika na nini na vita vyenu huu si uonevu?

Mganga akasema hapana, ni sahihi kufanyiwa haya wewe maana wameshindwa kuyatekeleza haya kwangu, kwa mke wangu na wanangu maana wamekula miti mingi, hivyo kwa namna yeyote wanatafuta mahali pa kuniliza, nijutie na nilie kwa kusaga meno na hapo ndipo ilipoonekana panapofaa ni kwako!! Na wewe ni mbishi ulipoingia tu nilikwambia nikutengeneze huku si kuzuri na ukikaa nyumba hii upo vitani ila ukanijibu urogwe una nini, si wangerogwa akina Bakhressa wewe urogwe kwa lipi.

Nikakosa cha kusema na kwa mara ya kwanza nikaandikiwa makombe na madawa yenye harufu mbaya mbaya kujifukiza na hapo ndipo nikawa sawa hata kichwa na uchovu vikaacha na ukapita mwezi mzima salama salmini.

Siku moja ni kama ilianza na shughuli mbaya mbaya tangu kulipokucha kwani alikuja dada mmoja amedhoofu sana lakini kwa macho anaonekana ni mzima, huyu alikuja akiwa na majonzi huku machozi yakimlenga! Akatusalimia na kukaribishwa kilingeni, akamwambia mganga unanikumbuka? Akajibiwa kwa mfumo wa swali, "naam si yule uliyechukuliwa mpenzi wako?

Dada akajibu; "ndiyo kaka, nilikuja nikakwambia nina rafiki yangu ananichukulia mtu wangu hali akijua kabisa hivyo nikataka tumuondoe na ukaniagiza jogoo jekundu, sanda na pweza mbichi, tukaenda kufanya kazi kaburini na yule pweza tukamzika huko....
Mganga akadakia; "vipi maendeleo je bado tuongeze nguvu? Maana sikukuona tena ni miezi sasa na nilikwambia uniambie maendeleo yake".

Dada akaendelea; "mh! Kwanza yule mtu ni ndugu yangu tumbo moja sema nilimleta kwangu baada ya kufeli masomo yake ya kidato cha nne hivyo baada ya kupata kazi na kuondoka kwangu nikaja kugundua anatembea na shemeji yake kwa ushahidi wa sms kabisa na nilipomuuliza ndugu yangu akaanza maneno ya kejeli! Iliniuma sana ndiyo nikaja kwako na nikakwambia ni rafiki ili unitendee jambo langu bila maswali mengi.

Mganga akadakia; "aisee!!

Dada akaendelea; "baada ya ile shughuli ndugu yangu akaanza kuumwa sana wazazi wakamaliza tiba za kizungu na kushauriwa tujaribu kienyeji, tumezaliwa sisi wawili tu hivyo ikawa kila msafara na mimi niwepo kwenye kuuguza na tulikwenda Pemba, Pangani na hata Turiani lakini kote huko ramli zilisema KIKULACHO KI NGUONI MWAKO bila kutaja nani adui ila walimuagua bila mafanikio yeyote...na sasa hivi yupo tu nyumbani hali mbaya amekwisha na mwili unanuka maana ana mapele yanatoka maji kama Pweza na kila akikaa ananyanyua mikono juu kumuomba Mungu amchukue kwani anateseka....nimeuza kila kitu na nimekonda hivi sababu ya mawazo na kujutia hivyo naomba tumlete kwako umuague apone.

Mganga akajibu kwa chuki; watu mbona mna matatizo? Yasingempata uliyoyataka ungesema mimi si mganga sasa leo hii unaleta kigeugeu! Siwezi kumuopoa nilisema tangu mwanzo kuwa atakaeweza kumuagua huyo ni atakaeweza kumpata pweza tuliyemzika...na sasa si ameshakuwa mchanga!! Haaguliki mama nenda kapumzike!!

Yule dada akaanza kulia kwa sauti huku akisema; "nisaidie ndugu yangu anakufa jamani umemuua ndugu yangu, huyo mpenzi wangu mwenyewe pia ametuacha sote na sasa hivi ameoa mwanamke mwengine...

Inaendelea....
Eeeeh ...
Maskuni hawa wadada dah..
BTTS
 
ulijuaje kama ni mchawi ,huwa unamuona akiwanga?? basi na wewe kuna namna
Kuna bibi mtaani kwetu huwa hakosi kusali Jumapili, hakosi jumuiya, ni mwanachama wa vikundi mbalimbali vya kitawa kanisani, yani ni muumini safi kwa 100%.

Lakini nyuma ya pazia ni mchawi grade A, leo ndio nimejua kwa nini wana-act hivyo.
Unforgetable
 
Back
Top Bottom