Visa na Mikasa ya Ethiopian Airlines - Waafrika Kulikoni?

Zisome vizuri comments zote. Usisahau hata ya Magonjwa Mtambuka nayo inaweza kuwemo humo 😁😁.

Haya ni maajabu ya Mussa yanayoweza kutokea Afrika tu
Soma wewe uelewe mkuu. Una utaalamu na hii kitu au unazungumza tu? Huoni kuna some rational reason behind ndege mbili za shirika moja kujaribu kutua same airport iliyo under construction same day within 2.5 hours of each other? Umejaribu kufuatilia ET wametoa maelezo gani kuhusu hizi incidents au umeishiai ku insinuate "innate inferioty" of Africans?
 
Wewe una utaalamu na hii kitu au unazungumza tu?

Pana haja ya hata ya kukumbushana wataalamu wa hizo vitu waliko?

Boeing: The Boeing Company: General Information

Ndege inatokana nje ya nchi inakwenda kutua hadi kufikia 10m kutoka ardhini aliyekuwa nayo hajui kuwa amepotea njia?

Kama vile haitoshi na ndege nyingine kampuni hiyo hiyo inafanya hayo hayo. Hivi hizo ndege mbili za kampuni hiyo hiyo hawawasiliani wao kwa wao au hata base yoyote yao?

Haya si ya Einstein - "doing the same thing over and over,expecting different results." Kuna haja ya kuita jina uzuri? Hiyo si ndiyo insanity sasa?

Ndege zinatua viwanjani zikishirikisha vyema control towers husika.

Hakuna visingizio hapa. Usanii huu na wa maji na umeme wa kina Majaliwa ni baba mmoja mama mmoja!
 
Pana haja ya hata ya kukumbushana wataalamu wa hizo vitu waliko?

Boeing: The Boeing Company: General Information

Ndege inatokana nje ya nchi inakwenda kutua hadi kufikia 10m kutoka ardhini aliyekuwa nayo hajui kuwa amepotea njia?

Kama vile haitoshi na ndege nyingine kampuni hiyo hiyo inafanya hayo hayo.

Haya si ya Einstein - "doing the same thing over and over,expecting different results." Kuna haja ya kuita jina uzuri? Hiyo si ndiyo insanity sasa?

Ndege zinatua viwanjani zikishirikisha vyema control towers husika.

Wewe lengo lako ni malumbano ya hoja za kisiasa. Hii ishu ya ndege umeingia cha kike bora ungetafuta mfano mwingine sababu hujui chochote.
 
Wewe lengo lako ni malumbano ya hoja za kisiasa. Hii ishu ya ndege umeingia cha kike bora ungetafuta mfano mwingine sababu hujui chochote.

Wewe si Jaji kama Tiganga kutoa hukumu yoyote.

Hoja iko wazi kuna madege marubani hawafai. Bahati mbaya tuna wengine makwetu nao hawafai pia.

Cha kike umejisokomeza wewe. Huna lolote unalolijua.

Habari ndiyo hiyo.
 
Kama sinema vile madege ya Ethiopian airlines hutua viwanjani kwa hisia huku yamebeba abiria:

Ethiopian Airlines Airbus A350 Suffers Wing Tip Strike During Landing

Mtu anaweza vipi tua dege kwa kusikiliza wazimu wake tu?

View attachment 2016618

Siyo case 1 bali ni case baada ya case na katika kipindi kifupi.

Haya yanawezekana namna gani?

Haya si ndiyo yale mambo yetu kama haya na kina Sirro, Siyani, Tiganga, Majaliwa, Mwambe, Makamba nk? Mambo kama haya yanatokea hivi kwa wenzetu walio staarabika kweli?

Pana haja ya kumkagua mtu mweusi vizuri. Kumbe tunaweza walaumu kina Majaliwa na wenzao kwa kuwaonea.

Yawezekana tuna matatizo ya ndani kwa ndani.

Yawezekana siyo bure.
Mtu mweusi unasikia ni IGP unadhani ni mtu aliyeelevuka kweli kweli kumbe sio.

Ukisikia ni Jaji utadhani ni mtu wa maana sana kumbe ni kinyumr chake. Mtu mweusi usimtambue kwa title.
 
Wee mbuzi subiri J3 utupe mrejesho kwenye kesi ya basha lako. Haya mambo yandege huna weledi nayo.

JF raha sana. Sawa mbuzi jike. Eti mtalaamu wa ndege.

IMG_20210906_210504_636.jpg

Mtalaamu wa ndege uwe wewe? Una nini cha kumwambia nani wewe?

IMG_20211118_181728_474.jpg

Kawaambie waliokutuma, hatudanganyiki!
 
Hiyo nadhani ilikua emergency landing! Mpongeze pilot aliye tua ndege hapo kwa kuokoa maisha ya watu

Ni muhimu kutofautisha emergency landing na diverted flight.

KIA - Arusha na kutua Arusha, haikuwa emergency landing bali ilikuwa ni diverted flight.
 
Sahihisho:

Kilichotokea Arusha. Siku Ethiopian (B767) inawasili KIA, kuna ndege ndogo ilipata breakdown mwanzoni mwa runway. Control tower ya KIA wakamuelekeza pilot wa Ethiopian afanye emergency landing kwenye uwanja mdogo wa Arusha. Pilot akaishusha B767 Arusha na kumaliza runway yote tairi la mbele likaishia kwenye mchanga. Siku ya kuichukua wakaja na wakaguzi, mafundi na mapilot nguli wao. Wakapunguza baadhi ya fixtures kupunguza uzito na kufanikiwa kuirusha toka pale.

Ajali ya Ethiopian B737 Max 8 ni habari ya kimataifa iliyotikisa na kuleta mabadiliko makubwa huko Boeing na FAA. Haihitaji maelezo zaidi kwa mtu anayefuatilia international affairs.

Certainly Ethiopian haijafikia viwango vya Emirates, Qatar, Etihad, BA, na mashirika kadhaa ya nchi tajiri. LAKINI sio shirika la ovyo kiasi hicho ulichoelezea hapa. Kwa Waafrika tena nchi masikini kiasi kile, wanajitahidi sana.

Flight incidents na accidents ulizoeleza hapa hutokea mara kwa mara duniani kote na zinakuwa noted. Tatizo la crosswinds, maelekezo mabaya ya atc, poor visibility, defective instruments, ni common occurrences. Ukiweza kupitia accident records zinazotunzwa na CAAs, FAA, ICAO, IATA n.k. utaelewa.

Kama kweli unachokieleza hapa ndicho kilichopelekea jamaa kushauriwa watue Arusha, wanabahati sana hayakutokea madhara makubwa. Ndege ingeweza kupitiliza ikapinduka au kugonga vitu ikalipuka. Urefu wa uwanja wa Arusha unafahamika, ukubwa na uwezo wa ndege ya Ethipoia hali kadhalika unafahamika, kimsingi ni nadra sana ndege itue pale bila kupata mushkel.

Kwa akili zangu bora ndege ingetua kwa kuanzia upande wenye ndege ndogo iliyopata hitilafu mwanzo wa uwanja ikamalizia safari yake upande ulio salama.

Najua kuna factor ya mwelekeo wa upepo unaoamua ndege itue kuelekea upande upi ( kutua Arusha ilikua maamuzi mabovu).
 
..kutua ktk uwanja mdogo wa arusha si walielekezwa na control tower ya kia?

..na kama waliweza kuiteremsha hiyo ndege bila madhara huenda they are good at what they are doing.
 
..kutua ktk uwanja mdogo wa arusha si walielekezwa na control tower ya kia?

..na kama waliweza kuiteremsha hiyo ndege bila madhara huenda they are good at what they are doing.

Ndege ilikuwa diverted kwenda Arusha vigezo vyote vikiwa vimezingatiwa.

Ingeweza kuelekezwa Jomo Kenyatta, Mwanza, Zanzibar, Mombasa au hata JKNIA kama ingekuwa lazima Kwamba Arusha pana walakini.

Umapepe wa hawa ndugu kwa kuzingatia rekodi zao hauwezi kupuuzwa jumla kwenye yaliyofuata baada ya kufika Arusha.

NB: Hii haikuwa emergency landing.
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom