Visa na Mikasa ya Ethiopian Airlines - Waafrika Kulikoni?

Upepo wa Pesa

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
17,977
2,000
Nakumbuka liliwahi kutua Arusha Airport, na haina hata barabara ya kutoshea boeng...Ndege ikakita mwisho kabisa wa running way mpaka likakaa upande.

Siku linaondoka ilikuwa ni drama, inasemekana walilazimika kumleta Mtaalamu anayeweza kuiinua kwenye running way fupi...na akafanikisha.
Hiyo nadhani ilikua emergency landing! Mpongeze pilot aliye tua ndege hapo kwa kuokoa maisha ya watu
 
Drifter

JF-Expert Member
Jan 4, 2010
3,406
2,000
Huu ni Wenda wazimu wenyewe.

Pale Addis wamesha angusha chapa Max 2 mpya. Yawezekana wala si makosa ya mtengenezaji.

Ni siri iliyo wazi - hawafai.

Sahihisho:

Kilichotokea Arusha. Siku Ethiopian (B767) inawasili KIA, kuna ndege ndogo ilipata breakdown mwanzoni mwa runway. Control tower ya KIA wakamuelekeza pilot wa Ethiopian afanye emergency landing kwenye uwanja mdogo wa Arusha. Pilot akaishusha B767 Arusha na kumaliza runway yote tairi la mbele likaishia kwenye mchanga. Siku ya kuichukua wakaja na wakaguzi, mafundi na mapilot nguli wao. Wakapunguza baadhi ya fixtures kupunguza uzito na kufanikiwa kuirusha toka pale.

Ajali ya Ethiopian B737 Max 8 ni habari ya kimataifa iliyotikisa na kuleta mabadiliko makubwa huko Boeing na FAA. Haihitaji maelezo zaidi kwa mtu anayefuatilia international affairs.

Certainly Ethiopian haijafikia viwango vya Emirates, Qatar, Etihad, BA, na mashirika kadhaa ya nchi tajiri. LAKINI sio shirika la ovyo kiasi hicho ulichoelezea hapa. Kwa Waafrika tena nchi masikini kiasi kile, wanajitahidi sana.

Flight incidents na accidents ulizoeleza hapa hutokea mara kwa mara duniani kote na zinakuwa noted. Tatizo la crosswinds, maelekezo mabaya ya atc, poor visibility, defective instruments, ni common occurrences. Ukiweza kupitia accident records zinazotunzwa na CAAs, FAA, ICAO, IATA n.k. utaelewa.
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
16,451

Ninaifahamu vyema incident hiyo ya KIA, Arusha na hatimaye nje ya Arusha.

Ninazifahamu vyema incidents za chapa Max 8 za Addis.

Ninayafahamu mapungufu ya Ethiopian airlines na hata points of strength zao kama zilivyo airlines nyingine.

Ila mkuu kwa habari hii iliyokuja kwenye ufahamu wangu jana:

Ethiopian Airlines Airbus A350 Suffers Wing Tip Strike During Landing

IMG_20211119_201242_640.jpg

Give me a break. Usafiri wa anga na maisha ya watu si wa kufanyia mzaha hivi.

Wewe unaona hiyo ni sawa sawa?

Kama hao ni sawa:

IMG_20211119_154513_412.jpg

IMG_20211118_181728_474.jpg

Kwa hakika hata hawa wanaona ni sawa ndiyo maana wangali ofisini.

Kazi inaendelea kana kwamba hakuna lilitokea.
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
16,451
2,000
nilitegemea comment hii kutoka kwa m-bongo

Hicho ni kitu kizito utosini.

Nisiache "kuchema" ungekuwa umewatendea haki zaidi wabongo wa maana ambao wangalipo kwa kubadili pale:

"M-bongo" --> "mawazo duni kabisa"

Hiiiiii bagosha!
 
Ibambasi

JF-Expert Member
Jul 25, 2007
9,034
2,000
Kwa kusoma maandiko yao tu, hawa utawalinganisha na watu kama Etwege, Iboya, USSR, Idugunde, Yohodaya na wale wapuuzi wengine. Kwenye hilo kundi, afadhali kidogo Yohodaya, anaonekana kuwa na akili ila huamua kujivika ujinga. Lakini hao wengine, hakuna shaka ni very low minda.
Hao ndugu zako wa Ufipa Wana matatizo
 
Schmidt

JF-Expert Member
Aug 29, 2008
5,473
2,000
Zisome vizuri comments zote. Usisahau hata ya Magonjwa Mtambuka nayo inaweza kuwemo humo 😁😁.

Haya ni maajabu ya Mussa yanayoweza kutokea Afrika tu
Soma wewe uelewe mkuu. Una utaalamu na hii kitu au unazungumza tu? Huoni kuna some rational reason behind ndege mbili za shirika moja kujaribu kutua same airport iliyo under construction same day within 2.5 hours of each other? Umejaribu kufuatilia ET wametoa maelezo gani kuhusu hizi incidents au umeishiai ku insinuate "innate inferioty" of Africans?
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
16,451
2,000
Wewe una utaalamu na hii kitu au unazungumza tu?

Pana haja ya hata ya kukumbushana wataalamu wa hizo vitu waliko?

Boeing: The Boeing Company: General Information

Ndege inatokana nje ya nchi inakwenda kutua hadi kufikia 10m kutoka ardhini aliyekuwa nayo hajui kuwa amepotea njia?

Kama vile haitoshi na ndege nyingine kampuni hiyo hiyo inafanya hayo hayo. Hivi hizo ndege mbili za kampuni hiyo hiyo hawawasiliani wao kwa wao au hata base yoyote yao?

Haya si ya Einstein - "doing the same thing over and over,expecting different results." Kuna haja ya kuita jina uzuri? Hiyo si ndiyo insanity sasa?

Ndege zinatua viwanjani zikishirikisha vyema control towers husika.

Hakuna visingizio hapa. Usanii huu na wa maji na umeme wa kina Majaliwa ni baba mmoja mama mmoja!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom