Visa na Mikasa vya kusaka kwangu Utajiri toka Kigoma mpaka Kongo

Walimtanga kidogo sana akapotea huyu jamaa story yake ya kweli maana hiki kipande nakifaham vzur mzee magu ndio kaukata mzizi na shina lake sasa hv hakunaga biashara hzo si wakubwa si wadogo
Usidanganyike mzee hiyo biz ipo tena Sana tu. Kilichofanyika ni shake up ya madealers wa zamani then wa kaingia wapya. Au naishi mtaa gani ndugu yangu ambao hauna mateja. Unadhani wanapata wapi ngada hao mateja. Ngada ipo tena ipo sna tu. Sema madila ndio wapya.
Hata hao Mataifa makubwa Wameshindwa hii biz maana mpunga wake si wanchi hii.
 
Walimtanga kidogo sana akapotea huyu jamaa story yake ya kweli maana hiki kipande nakifaham vzur mzee magu ndio kaukata mzizi na shina lake sasa hv hakunaga biashara hzo si wakubwa si wadogo
Shame on u!!eti sasa hivi hakunaga biashara hiyo?!!hiyo repoti ya USA, ya mwaka jana hukuiona juu ya lango la kupitishia madawa ya kulevya ni dar?!!mbona watu wanatumia tu, sema imepungua sio kuisha?!!duniani wapi wamefanikiwa kuitokomeza, huko uarabuni kwenyewe kwenye adhabu za kuuawa bado inafanyika sembuse huku?!!
 
PART VI


Maisha mwenzangu alikuwa ameyapatia.ana gari zuri tu.mimi sikuwa hata na wazo la kununua gari kwa muda huo. Sikuwa na uwezo huo.

Abdul alinielezea biashara za madawa ya kulevya alinielezea kuwa kama naweza nijiunge naye.hofu yangu ilikuwa ni kuwa hiyo ni biashara kharamu.

Abdul alinihakikishia sipaswi kuwa na mashaka sababu ni biashara ambayo anaifanya na watu wakubwa mmoja wapo ambaye anajua alikuwa mtoto wa kiongozi mkubwa sana wa nchi na mwingine mtoto wa mkuu wa polisi jiji flani (huyu mkuu wa polisi alikuja uawa baada ya mtoto wake kukamatwa china akiwa na mtoto wa kiongozi mkubwa halafu mtoto wa kiongozi mkubwa alimtoa mwanawe akamwacha mtoto wa huyu mkuu wa polisi.huyu mkuu alitaka akaharibu kila kitu.akawahiwa akauawa)

Abdul alinielezea mambo makubwa na mazito ambayo sitayaandika hapa kwa sababu kadhaa.lakini jambo moja ambalo alinihakikishia ni kuwa alikuwa pia ameshaenda sana Kigoma kupikwa.

Abdul alikuwa anaenda Kigoma Ujiji kwa mzee mmoja ambaye alikuwa anamweka kwenye pipa la maji na kuchanganya na dawa ambazo baada ya hapo Abdul anakuwa haonekani.

Hizi dawa zipo. Unatakiwa zile nguo ambazo unatakiwa uzitumie siku hiyo uzivae. Halafu unawekwa kwenye pia na maji yanachemshwa kiasi flani. Unazama mwili mzima.ukiwa na viatu na kila kitu.

Ukitoka hapo huonekani labda kwa mtu ambaye ana supernatural power pia.lakini hawa wakawaida huonekani.

Mnakumbuka kisa cha yule kijana mmoja mbezi kama sikosei ambaye alikuwa anatembea na wake za watu kimazingara? Haya mambo yapo. Mtu anakuww haonekani ila anaweza fanya chochote kile kama kufungua mlango na ukaona mlango unafunguka. Au ukasikia mtu anatembea ila ukigeuka humwoni.

Kwa Kigoma Ujiji na mpakani mwa kigoma na Kongo,Kigoma na Burundi ni maeneo ambayo nafahamu hizi dawa zipo sana.

Na dawa za mazonge ambazo unaweza ukawa unaona kitu wewe tu wenzako hawaoni. Kukutia uchizi. Kama kuna mtu aliwahi kaa Kigoma miaka flani pale sokoni na karibu na Stesheni alikuwepo chizi mmoja ambaye alikuwa akitembea anakimbiza hewan Ubooh wake. Anasema anaona ubooh unakimbia hewani.

Huyu inasemekana alipenda sana onesha urijali na akatembea na mke mdogo wa Mzee Mmoja alikuwa akifahamika kama Mkataamkali kama sikosei.

Akawa ametiwa hayo mazonge anatembea anakimbiza Ubooh hewani.ikawa ndo basi tena. Mwishowe akawa Kichaa kabisa.

Kigoma watu walikuwa wanaogopa hata kuibiana.sijui siku hizi maana na kule nako ukionesha tu una mafanikio ukarudi kwenu unaweza usirudi tena Mjini.

Abdul alikuwa na pesa. Amebadilika sana ndani ya muda mfupi. Alinishawishi sana lakini sikuweza kubaliana naye. Akawa ananambia kina safari anaifanyia kazi ya kwenda South Africa na China. Huko ndo maisha ataya win hasa.

Mimi nlikuwa njia panda.nikifahamu athari za madawa ya kulevya.nikifahamu kuwa ikitokea nakamatwa kifungo nitakipata tu. Abdul alikuwa akijiamini. Ingawa anasema bado hakuwa mfanyabiashara mkubwa sana lakini alikuwa na connections na watu walishaanza mwona kuwa ni potential.

Nlirudi kwangu tukaendelea kuonana na Abdul na kupeana salamu. Mwishowe akachoka.

Mimi nliendelea na kazi yangu ya ufundi.siku moja nimechukua gari ya mteja nikawa nmeenda Ilala pale Shaurimoyo kununua spare.ile gari kuna mteja alileta itengenezwe na unajua sisi mafundi huwa tunatumia usafiri huo huo unaoletwa na wateja.

Basi narudi nipo surrender kwenye kifoleni ghafla nligongwa na gari Range Rover nyeusi. Gari nliyokuwa nayo haikuumia sana.

Kwenye ile Range alitoka kijana mmoja mweupe hivi mwembamba.akaniuliza gharama ya kutengeneza ile gari itakuwa tsh ngapi? Yule kijana alinishtua sana. Mwili ulinisisimka sana. Sijawahi kutana na mtu mwili ukasisimka kama vile. Nlimtizama sidhani kama alikuwa binadamu wa kawaida maana nliona kama wakati flani anataka kupotea then anakuwepo.

Nlitamka milion 1. Hakujibu kitu.akaingia kwenye gari akachukua pesa na kuja nipa. Sikuhesabu.nikabeba hadi kwenye gari nikawa naondoka.kucheck zile pesa nikajiwa na hamu ya kuhesabu.

Nliingia pale mbele barabara ya kushoto kama naelekea makaburini.nikapark gari. Kuhesabu ilikuwa tsh 1,700,000. Sikuamini. Nikahesabu tena.nikahesabu mara tano. Ili 1,700,000.

Repair ya ile gari ilikuwa haizidi tsh 50,000. Nlishangaa sana. Why yule bwana mdogo anipe pesa zote hizo.

Katika ulimwengu wa roho. Msiamini kama humu duniani tupo peke yetu. Kuna majini mengi yapo njiani.mitaani kwa namna mbalimbali.hili nlihakikishiwa kabisa na mzee na siku moja alitaka nipaka dawa usoni nione.nlimgomea. alinambia nione viumbe vilivyopo duniani. Sikuafiki...

Siku zote hizi nlianza pata mawazo ya kumtafuta Ahmed.sasa nlikuwa na nauli ya kwenda Mwanza kumtafuta Ahmed.maana nliambiwa Ahmed yupo mwanza anafanya biashara ya uvuvi na ni tajiri kweli kweli...

Itaendelea.....
Chizi Maarifa tunaomba muendelezo basi mkuu
 
Back
Top Bottom