Visa na Mikasa vya kusaka kwangu Utajiri toka Kigoma mpaka Kongo

Mimi nadhani kama una nia ya dhati ya kumsaidia mtu utamsaidia tu, sababu anachofanya ni maamuzi yake na sio yako, pia kiuhalisia unatakiwa kumpa namna ya kufika huko kwa mtaalam husika na yeye ndio atachagua mwenyewe, na sio unaanza kumpa tahadhari ambazo hazina msingi, mimi nadhani ni mmoja wa watu ambao niliwahi kukuomba connection lakini hukunipa na sidhani hata msg yangu ulijibu, embu mwisho wa siku tuache unafiki, mtu akikuomba kitu kama hutaki sema sitaki kukupa, sio unazunguka zunguka na kutoa vitisho na tahadhari ..kwani anayeamua kufuata hio njia hajui? Anyway ni makavu laivu nakupa mzee baba, na wengine wenye tabia kama yako, nimepata shida kupata connection lakini kuna wenye nia ya dhati ambao wamenisaidia.
Kwahiyo mkuu umeshatoboa maisha?
Tunasubiri series yako utakapokuwa kuwa tayari kushare nasi
 
Mie mkuu naangalia how can I save my surrounding nimetokea jamii masikini so nawaza hata kuwajengea shule kama laizer anavyofanya kule kijijini kwao.pia wale Wazee Wangu waliovuka 65yrs kule kijijini niwe nawapa angalau posho ya kutumia kama lakairo anavyofanya kwao rorya.
Nawaza how can help like 1000 my village boys to get elimu mpaka chuo kikuu kwa nguvu zangu.
I feel urge to suffer just to rescue others mkuu. This is my burning desire. I'd like to make or leave a mark after my life hapa duniani.
Am ready to sacrifice my life for others this is my ambition.
So kila MTU ana dream zake just ni kuombeana tuzitimize usione za mwenzako hazifai za kwako ndo zinatakiwa kila MTU azifuate
Mkuu Mungu akubariki sana katika njia zako uje kufanikisha hilo. Actually you will leave a very unique legacy behind your life on your birth place.
Ili jamiizetu zibadirike lazima tuwepo watu tunaofikiria mambo positive kwenye jamii zetu. Mungu atusaidie
 
Napenda stori tu za aina yoyote ile, siangalii sana maidhui, hata hadithi zilizohadithiwa hapa jf nadhani nimesoma karibu zote ambazo nilifanikiwa kuziona, zilizoisha na ambazo zimeishia njiani
Hizo za njiani hazijaisha Sasa, Ila zengine zilikatizwa kwasababu maalumu. Nilichogundua walio kwenye ulimwengu wa giza wanapenda mambo yao yabakie kuwa unknown while mbele ya macho ya jamii wako so humble, Ila waingilie anga zao sasa.
Sasa ikatokea mtu ukaanza kusimulia dah wanakuandama kisirisiri.
Safari yetu ya Dec visiwani ilifanikiwa? Ya awamu hii sikosi
 
Drama ni nyingi sana jf, hata hadithi pia zipo zilizoishia njiani kwahiyo mi naona kama huwa wanaamua tu,
Ilifanikiwa sana safari ile kuliko matarajio na kiukweli nashukuru sana kwa hilo,
Acha kuahidi sasa maana sitakawia kukutumia ratiba mpya PM halafu uanze kuleta excuses
 
PART IV

Tulifika Kigoma late hours. Tukalala tukiwa tumechoka sana kwa mjomba wake Abdul. Kesho saa 3 baada ya chai nlikuwa wa kwanza kuaga kuelekea nyumbani.

Nlikuta nyumbani kumetulia sana.mzee hakuwepo na mama alikuwa amelala tu chumbani kuniona alianza kulia.dada akaja kutaka kujua kulikoni. Aliponikuta mimi akaanza kulalamika nliondoka siku zote hizo home hawana taarifa za kueleweka nipo wapi na siku kadhaa ago mama alizidiwa sana kwa mawazo akawa analia anasema nataka kumuua.

Nlishtuka kidogo na kumuuliza ilikuaje. Akanambia mama alizidiwa sana.joto lilipanda akawa anaweweseka kuwa mwanangu kwa nini unataka nife.

Wao walijua mama alikuwa analalamika sababu nliondoka muda na hakuwa akijua nipo wapi. Mama alikuwa akinipenda sana kuliko watoto wengine pale home.

Nlimfuata mama na kukaa naye karibu. Machozi yakinitoka.mama alikuwa amenyongea sana. Alinishika mkono akajaribu kutabasamu kwa kulazimisha.

Nlikuwa sijui niseme nini.maana ni wazi kuwa kama ningechoma mkuki kwenye beseni nlikuwa namuua mama yangu. Ili niwe tajiri.

Nliumia sana kuwaza yale. Baba alirudi tukaongea mambo kadhaa nlidanganya kama ambavyo nlikuwa nimesema mwanzo.

Mama alipenda mara nyingi tukae nimwongeleshe. Mimi nlikuwa nauguza vidonda kwa kificho maana hakuna ambaye angeviona akanielewa.mara nyingi nlivaa shati mikono mirefu na suruali.

Ila bado nlikuwa na maumivu kwenye makalio,mgongoni na magotini. Bahati nzuri usoni hakukuwa na alama za kuleta maswali mengi.

Nlijikaza sana nisioneshe mabadiliko yoyote pale nyumbani.

Baada ya siku mbili nilimfuata Abdul. Yeye alikuwa mtu ambaye wakati mwingine kama kachanganyikiwa.nlikaa naye masaa zaidi ya mawili nikimsemesha ila sometimes ni kama hayupo nami.

Nikamuuliza nini kilimpata. Abdul alinieleza kuwa alienda mazingira ambayo yalikuwa kama yangu. Akiwa kule chini aliletewa kiumbe kama mtoto.na kuambiwa kinatakiwa kula kidogo sehemu ya nyama yake kwenye paja au mguu baada ya goti kwa nyuma.

Na kuwa angepata kidonda ambacho kisingepona. Ila kila kile kidonda anapokuwa nacho pesa zinapatikana kwa biashara ndogo tu atakayofanya.

Anasema alishindwa sababu anamfahamu tajiri mmoja wa mabasi ambaye alikuwa na kidonda mpaka kinatoa harufu ila ni tajiri sana. Hakutaka jambo hilo hivyo akakataa kung'atwa/kukilisha kile kiumbe nyama yake.

Maana yake pale ambapo kingekula pasingepona asilani.aligoma. ila sasa amerudi mtaani anakuona tena kugumu pesa hamna.

Nlimweleza kisa changu.alinishangaa.akaniuliza hata hivyo si mama yangu ni mgonjwa?so kungekuwa na tofauti gani?

Abdul shida kubwa aliyokuwa nayo alipenda sana apate pesa awe anatanua na mademu. Alishawahi nambia kuna kipindi alipewa dawa kule Ujiji na babu yake ya kuvutia mademu.akavunja mwiko baada ya kutembea na mke wa mtu. Babu yake akamkatalia kumpa tena dawa ya kurekebisha. Sasa this time anataka pesa.

Abdul alikuwa anapenda sana wanawake ndipo nligundua kipindi kile anatembea sana na mademu kumbe ilikuwa ni sababu ya dawa.

Sasa tukawa tunawaza kumtafuta Ahmed. Tulienda kwao siku hiyo Jioni. Hatumkuta. Tukaenda kesho yake tukaambiwa alitoka jana na hajarudi.

Baadaye mdogo wake akatwambia Ahmed aliondoka na hatorudi.ameenda mwanza. Tulishangaa jama kaondoka bila hata kuaga.

Mimi maisha yakawa yale yale ya kuhangaika tukakubaliana na Ahmed tuende Dar kutafuta maisha.

Mimi nlikuwa na shangazi anakaa Dar akifanya biashara na abdul yeye hakuwa na ndugu anayemtegemea.

Mimi nlirudi home nikaanza jipanga namna ya kuwaeleza home wanielewe na wanipe mawasiliano ya shangazi.

Mzee alipinga sana mimi kuja dar.tena kufikia kwa ndugu.akanambia kama vipi nije dar ila nisifikie kwa ndugu zake.hataki maneno na watu.

Mama nlimwaga nikamweleza kuwa naenda Dar kupambana na maisha.alikubali kwa shingo upande.

Mzee alikuwa na some cash na nyingine nliuza kasehemu ka shamba langu. Baada ya week tukawa tayari na Abdul kupanda train kuja Dar.

Hatukulipa tiketi. Pale station tulikuwa wenyeji kiasi na hatukuwa na mizigo.mimi nlivaa kaptula na suruali mbili. Tshirts mbili na shati juu.

Abdul yeye alivaa suruali ya jeans moja na tshirts tatu.tukapanda train.

Mle ndani wakati wa ukaguzi tukawa tunazunguka tu ktk mabehewa na sometimes wale Titii tunawapa pesa kidogo. Mpaka kufika Dar Station. Tulilala station.

Baada ya hapo nakumbuka tulitembea siku ya kwanza Mpaka zilipokuwepo Ofisi za NASACO. Tulienda kuomba kazi ya usafi.

Jamaa walitujibu hamna kazi.tukatembea sana kutafuta sehemu ya kujisitiri mpaka tulipokuja fika viwanja vya mnazi mmoja.tulilala pale mpaka jioni tukaenda kula kwenye mabanda kilipokuwepo kituo cha mnazi mmoja.

Wazo likawa sasa tukatafute kazi.siku mbili tulikuwa tunalala pale. Tunakula mara moja tu.

Mpaka siku walipokuja tuvamia wenyewe wakatufukuza lile eneo tukaondoka kuelekea kariakoo.

Siku ya kwanza tunaliona lile soko nlishangaa sana. Nlikuwa napasikia tu.katika kuhangaika tukaamua kupanda gari ambalo lilikuja kutuleta mwenge. Stand ya Zamani.

Kule tulianza kuhangaika. Usiku ule tulilala nje ya maduka pale mwenge. Kesho yake katika kuzunguka tukakuta kuna wenzetu wengi wa kigoma wana maduka ya vipodozi.

Hapo pesa ilikuwa imekata sana. Tunakula mihogo na maji ya kuomba kwa watu.jamaa mmoja alikubali niwe nauza naye dukani. Abdul yeye alikuwa bado na mawazo yake ya mbali.akaniambia hajaja kuuza duka la mtu Dar. Akanambia ikiwa nitaondoka basi nimwambie jamaa muuzaji wa pale au frames nyingine naenda wapi ili yeye apate taarifa siku akinifuata.

Nlikaa pale kama miezi miwili nikipata uzoefu na nilikuwa mwaminifu sana. Sisi watu wa kigoma si wezi.na tunaogopa sababu tunajua ukimuibia Muha utalipa tu tena kwa majonzi. Utamtafuta uliyemuibia umbembeleze kumlipa.

Baadaye yule bwana akaniunganisha kwa bro mwingine alikuwa na duka kariakoo.duka la huyu lilikuwa kubwa sana.

Huko ndo nilijua wauzaji wengi ni wachawi.yule mwenye duka alikuwa na kawaida akifungua duka asubuhi sitakiwi kuwepo. Na ana draw yake hiyo sitakiwi kugusa.

Siku tumekaa dukani alikuja dada mmoja tukani kununua vipodozi vya jumla.yule dada alikuja na mtoto wake.yule mtoto akawa analia akililia kushushwa.

Yule mwenye duka akamwambia dada mshushe mwache acheze.yule dada akamshusha akaendelea kuchagua vipodozi mtoto akaja kule kaunta akaingia chini ya meza. Akawa kimya tu.

Yule dada alipomaliza kuchagua akataka mtoto wake.jamaa akasema mbona ametoka kukufuata...yule dada akawa mkali akasema mtoto hajatoka nje yupo mle mle ndani. Akataka leta mzozo.yule jamaa akajizungusha kisha akasema hajamwona mtoto.mimi nikasema mtoto aliingia chini ya meza kule karibu na anapoweka jamaa mizigo yake.jamaa akawa mzito kidogo.mimi nikaenda kule chini naenda mkuta mtoto kumbe alikuwa amelala.

Yule dada alisha panic.akapewa mtoto akiwa amelala.akamwamsha yule mtoto alizinduka kama mtu mwenye mawenge.akaanza kulia sana.hakunyamaza mpaka wanaondoka.

Jamaa siku hiyo akanipa pesa zangu akanambia namwingilia kwenye shughuli zake.asinione tena pale dukani.sikuelewa kosa langu.(baadaye nlikuja fahamu jamaa alikuwa na msukule mtoto kule chini)

Nitaendele....
 
Daaa mkuu endelea kushusha balaa ,, sasa tuko Daslama.
 
Back
Top Bottom