Visa na Mikasa vya kusaka kwangu Utajiri toka Kigoma mpaka Kongo

PART V

Kurudi mwenge kwa jamaa akanambia nitafute maisha mengine yeye alishasaidia nimepata uzoefu.

Nikarudi Kariakoo kutafuta kazi.baada ya siku chache nikapata kwa mhindi mmoja.nlifanya naye kazi yule mama na mumewe. Nao walikuwa wakifungua duka asubuhi mimi natakiwa nisubiri nje.wakimaliza ndo wananiita.

Wale wahindi walikuwa watu wa ibada sana, ila cha kushangaza sasa asubuhi ilikuwa mteja yeyote akija wa kwanza kama anataka kitu lazima auziwe. Hata kwa bei nusu.hamna mteja wa kwanza kuondoka bila kununua kitu. Walifundisha hilo pia.kuwa ni vyema mteja wa kwanza aondoke amenunua kitu.

Siku moja yule mama akanambia pale nlipokaa nivute draw nimpatie kitabu cha mahesabu.kumbe nlivuta nyingine ya juu kimakosa. Ile kuvuta hivi nikakuta kuna paka mkubwa sana yule mle ndani. Yule mama kuona nimevuta ile draw alinifuata kwa hasira akataka kunipiga kibao nlimtizama akasita.akatukana sana.

Akanambia nibebe kila changu mle ndani akanipa tsh 50,000 nisikanyage tena dukani kwake.na asije akasikia lolote lile maana atasema nimemwibia.nliondoka nikiwa na maswali mengi. Nakumbuka yule mama na mumewe kuna rangi walinikataza nisivae mle dukani. Wao walipendelea rangi ya kijani.wakiwa wanajifunga tukamba twa kijani pia.mikononi. lakini pia hata kwenye gari pale kwenye steering na gear walifunga vitambaa vya kijani. Mle ndani hawakuacha kuchoma ubani hasa asub,mchana na jion saa 10.

Kijani Ilikuwa ndiyo rangi yao pendwa pale dukani.nlitoka na maswali mengi sana.sikuwa na hamu tena ya kuuza duka kariakoo.

Miaka yangu yote nlikuwa napenda sana magari. Hivyo nliona ni wakati mzuri wa mimi kwenda jifunza ufundi makenika.

Nlitembea mpaka kijitonyama huko nikakuta kuna garage moja hivi maeneo ya karibu na sayansi kama.unataka kwenda kilipo kituo cha daladala kwa sasa.nliomba kujifunza ufundi.

Jamaa walishauriana sana kuhusu kunichukua. wakaamua niwe nafika asubuhi kujifunza mpaka jioni.

Nikawa sina pa kulala.nikawa natoka jioni naenda lala Mwenge.ikaenda hivi kama mwezi mzima.jamaa walinipenda sababu nlikuwa mpole na pia najituma sana.pia nlikuwa mwaminifu sana.so jioni natembea taratibu hadi mwenge najizungusha zungusha mpaka night ndo nalala.

Siku moja nikamwambia mlinzi issue yangu.akanielewa ila alishangaa sana kuwa kipindi chote hicho kumbe nlikuwa sina pa kulala. Wakaniruhusu niwe nalala mle ndani ya garage. Ikawa ndo maisha yangu.

Nlijifunza ufundi kwa bidii sana.nikaja fundishwa udereva na fundi mkuu. Nikawa angalau napata pesa kidogo natunza kwa mmiliki wa gereji ambaye alinipenda kama mdogo wake.

Ikawa kila mara napopata nafasi naenda Mwenge kuwasalimia jamaa wa pale.

Baadaye nikawa fundi mzuri wa body (panel beating )na mechanics kidogo.nliipenda kazi ndani ya miaka miwili nlikuwa napata kazi sehemu mbalimbali.

Pale garage nikawa sikai mara nyingi naitwa kwenda fanya kazi nje.mwenye gereji akaamua kuwa aniajiri.nikakubali.nlifanya kazi miezi 3 ananipa posho tu. Mshahara hanipi.kila nikimwambia maneno yanakuwa mengi.na kipindi hiki nimeshapanga nina maisha yangu.

Nikahamia garage nyingine.niliendelea kujijenga vizuri tu nikafahamika sana.baadaye yakaanza majungu kazini.mwenye gereji alikuwa anapenda sana majungu. Anapenda apewe hbr za watu wote pale gereji.mimi nlichukiwa sababu sikuwa napenda maneno na pia tabia ya wizi sikuwa nayo.hivyo ikawa matajiri wanapenda gari zao wanikabidhi mimi.

Sometimes wanaleta gari wanataka mimi ndo nikanunue spares wakati kazi inafanywa na mtu mwingine. Siwezi sahau siku ambayo walinizushia nimeiba spare ya gari Prado ambayo ilishushwa engine.

Nlifadhaishwa sana.nikaambiwa nisikanyage tena pale gereji.nikarudi mtaani.nikahangaika sana kupata kazi. Mara nyngi ilikuwa ni day worker tu. Nikaenda Pugu Road kuna tajiri mmoja ana magari makubwa pale.

Nlienda omba kazi kwa wahindi.walinambia hamna kazi.nikarudi mnyonge sana. Kule home miaka ilikuwa imeshapita na mama alisha fariki. Nikawa nawasiliana na mzee.

Nikamweleza suala la kazi. Akanambia atanisaidia kwenda kwa mzee wetu flani kule kijijini. Kweli baba alienda akanambia nimtumie kiasi flani cha pesa.nikatuma. zilitumwa dawa za kuoga na kutafuna. Niliambiwa nioge usiku ambao kesho yake naenda tafuta kazi. Then nilale chini, nisi sex ,nisinywe pombe.nlioga nikalala chini.

Kesho yake nikarudi Pugu Road( Nyerere Road) kule kule kwa wahindi. Nikasema nataka onana na manager.kweli nikapelekwa kwake.nikaonana naye nikamwambia nahitaji kazi.

Akanambia kama nipo tayari nianze muda huo anipeleke kwa supervisor.kweli akanipeleka kwa supervisor na kunambia nianze kazi ni deal na yale magari ambayo yalikuwa na shida kwenye body(panel beating)

Nikaanza kazi.

Itaendelea....
Nikamweleza suala la kazi. Akanambia atanisaidia kwenda kwa mzee wetu flani kule kijijini. Kweli baba alienda akanambia nimtumie kiasi flani cha pesa.nikatuma. zilitumwa dawa za kuoga na kutafuna. Niliambiwa nioge usiku ambao kesho yake naenda tafuta kazi. Then nilale chini, nisi sex ,nisinywe pombe.nlioga nikalala chini.

Kesho yake nikarudi Pugu Road( Nyerere Road) kule kule kwa wahindi. Nikasema nataka onana na manager.kweli nikapelekwa kwake.nikaonana naye nikamwambia nahitaji kazi.

Akanambia kama nipo tayari nianze muda huo anipeleke kwa supervisor.kweli akanipeleka kwa supervisor na kunambia nianze kazi ni deal na yale magari ambayo yalikuwa na shida kwenye body(panel beating)

Nikaanza kazi.

Hichi kipande kimenisisimua sanaa....
 
PART IV

Tulifika Kigoma late hours. Tukalala tukiwa tumechoka sana kwa mjomba wake Abdul. Kesho saa 3 baada ya chai nlikuwa wa kwanza kuaga kuelekea nyumbani.

Nlikuta nyumbani kumetulia sana.mzee hakuwepo na mama alikuwa amelala tu chumbani kuniona alianza kulia.dada akaja kutaka kujua kulikoni. Aliponikuta mimi akaanza kulalamika nliondoka siku zote hizo home hawana taarifa za kueleweka nipo wapi na siku kadhaa ago mama alizidiwa sana kwa mawazo akawa analia anasema nataka kumuua.

Nlishtuka kidogo na kumuuliza ilikuaje. Akanambia mama alizidiwa sana.joto lilipanda akawa anaweweseka kuwa mwanangu kwa nini unataka nife.

Wao walijua mama alikuwa analalamika sababu nliondoka muda na hakuwa akijua nipo wapi. Mama alikuwa akinipenda sana kuliko watoto wengine pale home.

Nlimfuata mama na kukaa naye karibu. Machozi yakinitoka.mama alikuwa amenyongea sana. Alinishika mkono akajaribu kutabasamu kwa kulazimisha.

Nlikuwa sijui niseme nini.maana ni wazi kuwa kama ningechoma mkuki kwenye beseni nlikuwa namuua mama yangu. Ili niwe tajiri.

Nliumia sana kuwaza yale. Baba alirudi tukaongea mambo kadhaa nlidanganya kama ambavyo nlikuwa nimesema mwanzo.

Mama alipenda mara nyingi tukae nimwongeleshe. Mimi nlikuwa nauguza vidonda kwa kificho maana hakuna ambaye angeviona akanielewa.mara nyingi nlivaa shati mikono mirefu na suruali.

Ila bado nlikuwa na maumivu kwenye makalio,mgongoni na magotini. Bahati nzuri usoni hakukuwa na alama za kuleta maswali mengi.

Nlijikaza sana nisioneshe mabadiliko yoyote pale nyumbani.

Baada ya siku mbili nilimfuata Abdul. Yeye alikuwa mtu ambaye wakati mwingine kama kachanganyikiwa.nlikaa naye masaa zaidi ya mawili nikimsemesha ila sometimes ni kama hayupo nami.

Nikamuuliza nini kilimpata. Abdul alinieleza kuwa alienda mazingira ambayo yalikuwa kama yangu. Akiwa kule chini aliletewa kiumbe kama mtoto.na kuambiwa kinatakiwa kula kidogo sehemu ya nyama yake kwenye paja au mguu baada ya goti kwa nyuma.

Na kuwa angepata kidonda ambacho kisingepona. Ila kila kile kidonda anapokuwa nacho pesa zinapatikana kwa biashara ndogo tu atakayofanya.

Anasema alishindwa sababu anamfahamu tajiri mmoja wa mabasi ambaye alikuwa na kidonda mpaka kinatoa harufu ila ni tajiri sana. Hakutaka jambo hilo hivyo akakataa kung'atwa/kukilisha kile kiumbe nyama yake.

Maana yake pale ambapo kingekula pasingepona asilani.aligoma. ila sasa amerudi mtaani anakuona tena kugumu pesa hamna.

Nlimweleza kisa changu.alinishangaa.akaniuliza hata hivyo si mama yangu ni mgonjwa?so kungekuwa na tofauti gani?

Abdul shida kubwa aliyokuwa nayo alipenda sana apate pesa awe anatanua na mademu. Alishawahi nambia kuna kipindi alipewa dawa kule Ujiji na babu yake ya kuvutia mademu.akavunja mwiko baada ya kutembea na mke wa mtu. Babu yake akamkatalia kumpa tena dawa ya kurekebisha. Sasa this time anataka pesa.

Abdul alikuwa anapenda sana wanawake ndipo nligundua kipindi kile anatembea sana na mademu kumbe ilikuwa ni sababu ya dawa.

Sasa tukawa tunawaza kumtafuta Ahmed. Tulienda kwao siku hiyo Jioni. Hatumkuta. Tukaenda kesho yake tukaambiwa alitoka jana na hajarudi.

Baadaye mdogo wake akatwambia Ahmed aliondoka na hatorudi.ameenda mwanza. Tulishangaa jama kaondoka bila hata kuaga.

Mimi maisha yakawa yale yale ya kuhangaika tukakubaliana na Ahmed tuende Dar kutafuta maisha.

Mimi nlikuwa na shangazi anakaa Dar akifanya biashara na abdul yeye hakuwa na ndugu anayemtegemea.

Mimi nlirudi home nikaanza jipanga namna ya kuwaeleza home wanielewe na wanipe mawasiliano ya shangazi.

Mzee alipinga sana mimi kuja dar.tena kufikia kwa ndugu.akanambia kama vipi nije dar ila nisifikie kwa ndugu zake.hataki maneno na watu.

Mama nlimwaga nikamweleza kuwa naenda Dar kupambana na maisha.alikubali kwa shingo upande.

Mzee alikuwa na some cash na nyingine nliuza kasehemu ka shamba langu. Baada ya week tukawa tayari na Abdul kupanda train kuja Dar.

Hatukulipa tiketi. Pale station tulikuwa wenyeji kiasi na hatukuwa na mizigo.mimi nlivaa kaptula na suruali mbili. Tshirts mbili na shati juu.

Abdul yeye alivaa suruali ya jeans moja na tshirts tatu.tukapanda train.

Mle ndani wakati wa ukaguzi tukawa tunazunguka tu ktk mabehewa na sometimes wale Titii tunawapa pesa kidogo. Mpaka kufika Dar Station. Tulilala station.

Baada ya hapo nakumbuka tulitembea siku ya kwanza Mpaka zilipokuwepo Ofisi za NASACO. Tulienda kuomba kazi ya usafi.

Jamaa walitujibu hamna kazi.tukatembea sana kutafuta sehemu ya kujisitiri mpaka tulipokuja fika viwanja vya mnazi mmoja.tulilala pale mpaka jioni tukaenda kula kwenye mabanda kilipokuwepo kituo cha mnazi mmoja.

Wazo likawa sasa tukatafute kazi.siku mbili tulikuwa tunalala pale. Tunakula mara moja tu.

Mpaka siku walipokuja tuvamia wenyewe wakatufukuza lile eneo tukaondoka kuelekea kariakoo.

Siku ya kwanza tunaliona lile soko nlishangaa sana. Nlikuwa napasikia tu.katika kuhangaika tukaamua kupanda gari ambalo lilikuja kutuleta mwenge. Stand ya Zamani.

Kule tulianza kuhangaika. Usiku ule tulilala nje ya maduka pale mwenge. Kesho yake katika kuzunguka tukakuta kuna wenzetu wengi wa kigoma wana maduka ya vipodozi.

Hapo pesa ilikuwa imekata sana. Tunakula mihogo na maji ya kuomba kwa watu.jamaa mmoja alikubali niwe nauza naye dukani. Abdul yeye alikuwa bado na mawazo yake ya mbali.akaniambia hajaja kuuza duka la mtu Dar. Akanambia ikiwa nitaondoka basi nimwambie jamaa muuzaji wa pale au frames nyingine naenda wapi ili yeye apate taarifa siku akinifuata.

Nlikaa pale kama miezi miwili nikipata uzoefu na nilikuwa mwaminifu sana. Sisi watu wa kigoma si wezi.na tunaogopa sababu tunajua ukimuibia Muha utalipa tu tena kwa majonzi. Utamtafuta uliyemuibia umbembeleze kumlipa.

Baadaye yule bwana akaniunganisha kwa bro mwingine alikuwa na duka kariakoo.duka la huyu lilikuwa kubwa sana.

Huko ndo nilijua wauzaji wengi ni wachawi.yule mwenye duka alikuwa na kawaida akifungua duka asubuhi sitakiwi kuwepo. Na ana draw yake hiyo sitakiwi kugusa.

Siku tumekaa dukani alikuja dada mmoja tukani kununua vipodozi vya jumla.yule dada alikuja na mtoto wake.yule mtoto akawa analia akililia kushushwa.

Yule mwenye duka akamwambia dada mshushe mwache acheze.yule dada akamshusha akaendelea kuchagua vipodozi mtoto akaja kule kaunta akaingia chini ya meza. Akawa kimya tu.

Yule dada alipomaliza kuchagua akataka mtoto wake.jamaa akasema mbona ametoka kukufuata...yule dada akawa mkali akasema mtoto hajatoka nje yupo mle mle ndani. Akataka leta mzozo.yule jamaa akajizungusha kisha akasema hajamwona mtoto.mimi nikasema mtoto aliingia chini ya meza kule karibu na anapoweka jamaa mizigo yake.jamaa akawa mzito kidogo.mimi nikaenda kule chini naenda mkuta mtoto kumbe alikuwa amelala.

Yule dada alisha panic.akapewa mtoto akiwa amelala.akamwamsha yule mtoto alizinduka kama mtu mwenye mawenge.akaanza kulia sana.hakunyamaza mpaka wanaondoka.

Jamaa siku hiyo akanipa pesa zangu akanambia namwingilia kwenye shughuli zake.asinione tena pale dukani.sikuelewa kosa langu.(baadaye nlikuja fahamu jamaa alikuwa na msukule mtoto kule chini)

Nitaendele....
Hatariii
 
Nikamweleza suala la kazi. Akanambia atanisaidia kwenda kwa mzee wetu flani kule kijijini. Kweli baba alienda akanambia nimtumie kiasi flani cha pesa.nikatuma. zilitumwa dawa za kuoga na kutafuna. Niliambiwa nioge usiku ambao kesho yake naenda tafuta kazi. Then nilale chini, nisi sex ,nisinywe pombe.nlioga nikalala chini.

Kesho yake nikarudi Pugu Road( Nyerere Road) kule kule kwa wahindi. Nikasema nataka onana na manager.kweli nikapelekwa kwake.nikaonana naye nikamwambia nahitaji kazi.

Akanambia kama nipo tayari nianze muda huo anipeleke kwa supervisor.kweli akanipeleka kwa supervisor na kunambia nianze kazi ni deal na yale magari ambayo yalikuwa na shida kwenye body(panel beating)

Nikaanza kazi.

Hichi kipande kimenisisimua sanaa....
nimesoma story nzima ila hapa ndio nimepata content....aisee ndio maana nateseka sana na hizi business kuna mdau mmoja aliwahi kuandika hapa jf ulifanikiwa baada ya muda gani wa kufanya biashara..yaliyoelezwa yanafikirisha...ndio maana utajiri unaongelewa nyumbani kwenye familia..familia yako ikiwa bogas kama yangu ..utasoma utafanya biashara hutapata hela..na hutaajirika kazi nzuri...kuna mawili kumtegemea mungu full time au upande wa pili hakuna neutral...
 
Nikamweleza suala la kazi. Akanambia atanisaidia kwenda kwa mzee wetu flani kule kijijini. Kweli baba alienda akanambia nimtumie kiasi flani cha pesa.nikatuma. zilitumwa dawa za kuoga na kutafuna. Niliambiwa nioge usiku ambao kesho yake naenda tafuta kazi. Then nilale chini, nisi sex ,nisinywe pombe.nlioga nikalala chini.

Kesho yake nikarudi Pugu Road( Nyerere Road) kule kule kwa wahindi. Nikasema nataka onana na manager.kweli nikapelekwa kwake.nikaonana naye nikamwambia nahitaji kazi.

Akanambia kama nipo tayari nianze muda huo anipeleke kwa supervisor.kweli akanipeleka kwa supervisor na kunambia nianze kazi ni deal na yale magari ambayo yalikuwa na shida kwenye body(panel beating)

Nikaanza kazi.

Hichi kipande kimenisisimua sanaa....
Hakuna utakachofanikiwa hapa duniani kama shetani au Mungu hajaamua, ila wote wana masharti yao inabidi uyatimize
 
84 Reactions
Reply
Back
Top Bottom