Visa na Mikasa vya kusaka kwangu Utajiri toka Kigoma mpaka Kongo

Kamwe kwe hadithi za ushuhuda wa kweli kama huu, huwezi nikosaaaa, hawanitag ila mzee nyuzi hizi nazifukuzia humu jf balaaa Abdul kakuta mkongojo hamna
Hatari sana mkuu..!

Wakati mleta mada anameza mate ngoja niwape hii nayo kiufupi!

Enzi hizo mkoani Dodoma kulikuwa na mganga maarufu(jina kapuni) akatokea kijana mmoja akavutiwa na shughuli ile, akamwomba mganga amfundishe(dawa,miiko,masharti n.k) mganga akamwambia nitakupa mtihani ukiushinda nakupa mikoba, Kijana akasema nipo tayari kwa lolote.

Mtihani wenyewe ulikuwa kulala makaburini usiku kucha peke yake!
Kwakuwa kijana aliutaka uganga, akaondoka jioni kuelekea makaburini.. kufanyiwa majaribio!

Kilichofuata saa chache baadaye ni kijana kurudi nyumbani kwa mganga mbio huku akipiga kelele za kuomba msaada katika kusimulia kilichojiri akasema ilipofika kwenye saa6 hivi akaanza kuhisi mauzauza mara kama watu wanaongea, mara watu wanalia..baadaye akasikia vishindo vya watu wengi wakijongea kumfuata, uzalendo ukamshinda akatimua mbio

Mganga akamwambia alikuwa anamjaribu yeye kwa matukio hayo na alitakiwa kuwa jasiri na kuvumilia sasa kwakuwa amashindwa basi uganga ndio ikawa basi tena!
 
Back
Top Bottom