Visa na Mikasa vya kusaka kwangu Utajiri toka Kigoma mpaka Kongo

Scoob102

JF-Expert Member
Nov 22, 2014
276
500
Hivi mkuu Chizi Maarifa mkasa huu ulikutokea kabla ya ule wa wewe kugombea demu na jini au??

Maana kwenye ule uzi ulisema we umekulia sinza na maisha yako yalikuwa mazuri tu na ulikuwa unapush....
Hapa umekulia huko vijijini au mi ndio ambae sielewi vizuri???
Tupate chai tu ambayo pia haitaisha. Mambo ya huyu jamaa huwa hivi hivi yalivyo. Uzi zake hazinaga uhai kwanza!!!
 

Mafiningo

JF-Expert Member
Sep 5, 2016
4,071
2,000
PART I

Katika harakati za kutafuta maisha kuna mengi sana ambayo wanaume tunapitia. Leo ntawaelezea visa na mikasa ambayo nlipitia toka nimemaliza kidato cha nne mwaka 1995. Mambo haya yametokea nikiyaona na pia nikihusika.

Mimi ni mtoto wa kwanza katika familia ya watoto 7. Nikiwa na dada watano na mdogo wa kiume mmoja.

Nakumbuka mwaka 1995 mara baada ya kumaliza masomo nikawa home mara nyingi na vijana wenzangu.mpaka matokeo yametoka nlikuwa na division 2 hivyo nlipaswa niendelee na masomo.

Mzee hakuwa ametaka niendelee na masomo kwa kuwa hakuwa na pesa na pia mama alikuwa akiumwa mara kwa mara hivyo ikawa tunauza ng'ombe na mawese ili mama atibiwe.tukiwa na mahangaiko hayo mdogo wangu wa nne naye alishikwa na ugonjwa wa ajabu sana.

Akawa kama ana mashetani yakimpanda anatoka jasho jingi sana huku akitetemeka. Kipindi hicho anaishi Ujiji kwa Bamdogo. Ikabidi aletwe home kuja kuugua. Hapo ikabidi aitwe ustaadhi ayasikilize na kuyatuliza.tulihangaika sana. Dada zangu kuumwa umwa chanzo kilikuwa hao dada zangu kiukweli walikuwa warembo sana. Kila mtu pale kijijini aliwapenda. Wazee wengi walitamani kuoa kwetu.

Baba yangu alioa mwanamke wa mpakani na Burundi.alikuwa mzuri sana.

Pale alipokuwa anaishi sister Mzee mmoja alitaka mwoa huyu dada kama mke wa nne kipindi hicho mdogo tu.mzee alikataa. Kumbe yule mzee akamrushia majini ili yamsumbue asiolewe. Kwa hiyo ikawa shughuli hasa pale home.

Mama anaumwa sister anaumwa. Mi naendaje shule? Hali ile iliniumiza sana.nikatamani ngesoma ili niwaondoe wazee pale kijijini na akili nlikuwa nayo sana.shuleni ni wawili tu ambao tulipata division 2 wengine wote walipata 3,4 na 0.

Basi baada ya kuhangaika sana kutafuta pesa ili nikasome tulishauriana na jamaa zangu wengine wawili.

Hawa walikuwa nao wanataka pesa wamechoka maisha ya umaskini. Ahmed na Abdul. Ahmed yeye alikuwa ameishia darasa la saba akaamua kuwa mvuvi.

Jamaa alikuwa angalau anapata pata vijicent kidogo lakini hakuridhika.kila mara alikuwa ananipa mikasa ya ziwa tanganyika kwa mambo ya ushirikina.

Akisimulia jinsi ambavyo kuna siku ilikuwa wavuvi wenzie wamtoe kafara ili wapate samaki wengi.(hiki kisa ntakisimulia siku moja) Ahmed alikuwa akinikataza kupenda kupanda mitumbwi ya watu. Alinambia jinsi ambavyo kuna shangazi yake mtoto wake alianza umwa ghafla baada ya kupakizwa kwenye mtumbwi uliokuwa umepark ufukweni. Ikaja onekana yule mtoto aliguswa na misukule kwenye mtumbwi. Yule mtoto alianza kuumwa ghafla na kutokwa na udenda.walimuwahi kwa mganga ndo kupona kwake.

Basi Ahmed akawa anasisitiza sana kuwa tuvuke tuingie kongo kuna pesa nyingi sana.binafsi nlikuwa nasita maana sikuwa mzuri sana ziwani.nilikuwa na woga sababu nlishawi mezwa na mamba nikiwa mdogo lakini mzee alimng'amua kuwa alikuwa mzee jirani(mzee luyaga) akamkemea. Yule mamba alinitapika mzima kabisa.nikawa mwoga sana wa maji.

Basi tulishauriana sana baadaye tukaamua jioni moja tuondoke twende kongo.

Basi nyumbani mimi nliwaaga kuwa kuna tajiri mmoja kaomba nimsindikize kasulu kuna mambo anataka nimsaidie.mzee alihoji sana lakini akaniruhusu.

Siku hiyo ilikuwa jioni giza limeingia. Tukapanda boat tukiwa wengi kidogo kila mtu akiwa kimya.

Tulikutana na misuko suko mingi sana ziwani.nakumbuka kuna sehemu tulifika ile boat ikazima.halafu ikawa inazunguka pale pale yaani kama mtu anaizungusha hivi. Wakati huo inazunguka kwa kasi inatengeneza kama shimo kwenda chini.wale waongozaji walikuwa watatu.walipambana sana wakinyunyizia dawa n.k mwishowe wakakubaliana kuwa pale lazima tuache mtu mmoja.

Sikuelewa maana yake mpaka Ahmed alipofafanua.kuwa hatutoki pale mpaka tumtose mtu mmoja. Wakati natafakari mle ndani tupo kama 10 hivi wale jamaa wakawa kama wanashauriana jambo ila kwa kunong'onezana. Wakaanza kuuliza kila mtu aliondokaje.mimi nikajikuta nasema nliaga kuwa naenda kongo ktk wale watu mmoja akasema ye alitoroka tu hamna anayejua yupo wapi.

Wakati huo bado tunazungushwa pale pale na kuna shimo kuelekea chini ya maji kama unavyoona kimbunga.wale jamaa wakashauriana.ghafla wakamkamata yule jamaa na kumtupia kwenye maji pale shimoni. Alipogusa tu maji ni kama alivutwa chini halafu kikatokea kitu kama moshi mweusi ukamnyonya/mpokea kumshusha chini. Kukawa kimya.

Ziwa likawa limetulia sana.hapo mimi moyo unadunda sana.wale jamaa wakasema mmeona kilichotokea.tukatikisa vichwa. Wakasema hakijatokea kitu na tulivyo ndivyo tulivyotoka nchi kavu.hakuna mtu kuongelea hilo jambo kwa mtu yeyote.

Nlitetemeka sana.nilikuja shtuka tumefika ukingoni.walikuja kama migambo hivi pale pembezoni mwa maji.wakaongea na wale jamaa watatu wakapewa mshiko wakatwambia tutawanyike haraka sana wao wanaenda kusini sisi twende magharibi.

Safari ikaanza tukiongozwa na ahmad.ahmad alitutembeza sana kama masaa matatu mpaka tulipofika sehemu tukakuta kuna nyumba mbavu za mbwa na watu wanaota moto.akauliza kama tunaweza fika kwa mzee Shangai.wale jamaa wakatutizama kwa mshangao sana na kugundua tumetoka kigoma.wakahoji sana why tunataka enda mwona huyo mzee. Ahmed alisema tu kuwa kuna mwenzetu ana shida ndo tumemsindikiza.wakatuelekeza.

Ahmed alitaka tuendelee kutembea usiku huo huo. Tulitembea kama mwendo wa masaa 4. Tukifuata tu hiyo njia.mpaka kuja fika nyumba moja imezungukwa na miti.

Ile nyumba tuliifikia shida ikawa kuvuka kizingiti cha majani kwenda uwanja nyumba husika. Ilikuwa tunavuka tunakanyaga majani yametandikwa chini ila hatufiki kwenye nyumba.tulihangaika sana.hebu fikiria umbali wa kurusha jiwe kuanzia sijui saa tisa ile mpaka tunasikia jogoo hatuwezi fika hiyo sehemu. Alipowika jogoo tukagundua kumekuchwa sasa maana ilikuwa tunakaa baada ya muda tunajaribu tena.

Safari hii tukaweza vuka bila shida.tumefika karibu na mlango ahmed anaita babu, babu,babuu. Akatokea paka. Akaja akatuangalia...halafu akarudi ndani.baada ya dk moja akatokea mbabu flani hivi anatabasamu.

Akatukaribisha akitaka kwanza tujimwagie dawa miguuni.akatupa kila mtu kibuyu.tukaosha miguu. Akatwambia mmechoka laleni.

Mi nakumbuka nlikuja shtuka saa saba au nane hivi tukiwa tumelala kwenye ngozi kwenye kakibanda kengine nyuma ya nyumba.nlifikaje sikumbuki.

Tukajieleza sana.yule mzee akatwambia ngoja atueleze zaidi akatuambia tabia zetu na mambo mbalimbali ya ukweli.akamwambia Abduli wewe shida yako unapenda sana wasichana. Abdul alikataa kabisa kuwa si kweli.Mzee Shangai akawa anacheka tu.

Baadaye tumekaa akaja binti kutuletea chakula. Alikuwa binti mzuri sana.sana mzee hakutuambia kitu.basi tumemaliza kura mzee akatwambia yule binti atatupeleka kutembea shambani tuchume matunda.

Kiufupi tulimwambia mzee tunataka dawa ya utajiri.alituhoji sana hasa akisema tatizo la Abdul ni mademu.tukae naye siku tatu tufikirie kama bado tunataka dawa atatupeleka sehemu kama tumebadili mawazo ataturuhusu turudi.

Tuliona kama anatuchelewesha sana.ila hatukuwa na namna. Basi yule bint mzuri akawa anatupeleka kwenye matunda.

Abduli alishaonekana kumtaka yule demu.hivyo akawa amekaa mbele kabisa ana mdadisi dadisi bint. Mwishowe akaanza mwimbisha.yule bint alikataa sana.

Abdul akamwimbisha sana bint akasema basi tukirudi sababu mzee shangai atatoka kwenda porini mpaka kesho yake basi wataonana.

Abdul alikuja tusimulia huku anafuraha sana. Akidai anaenda kumla yule binti jioni mtoni.

Tulimtaka sana aachane na hizo issue baadaye akaanza sema ni wivu tu unatusumbua.

Kweli. Jioni mzee akaaga kuwa anaenda porini kuna watu anaenda kutana nao wanajeshi waasi.atatuacha na yule bint.

Baada kama ya kutoka masaa mawili abduli akatoka na yule bint.baadaye tumekaa chini ya mti tunaota moto abdul alirudi anapiga kelele sana

Kumuuliza tatizo nini akatujibu haoni sehemu zake za siri.mimi na Ahmed tulicheka sana tukijua jamaa anatudanganya .hapo Abdul aliangua kilio kikatushtua. Kweli Ahmed akaenda papasa.jamaa hakuwa na Ub**. Kabisa. Abdul akazidisha kulia.

Wakati tunatafakari hayo yule bint akarudi mbio naye.akaingia ndani. Abdul akawa anamwambia amwite babu shangai.bint anasema tusubiri kesho.ktk hali ya kuhangaika Ahmed akaenda mletea maji ya kunywa Abdul.

Hapo nlishindwa jizuia kucheka kuwa anamleteaje maji ya kunywa wakati jamaa hatoweza kojoa? Abduli akazidi kulia sana.nadhani akakumbuka akinywa maji hatoweza kojoa.

Nikawaza jamaa atakuwa anajisaidia kama kuku vyote vinatokea kwa nyuma.nikajikuta nacheka mpaka machozi yananitoka.

Abduli siku hiyo alikesha. Asubuhi sana akaja mzee Shangai.akaelezwa hali ile.alicheka sana.akasema Abdul tatizo lako wewe unapenda sana wanawake. Huyo ni mke wangu mi nlitaka nikuone tu je kweli ulivyokuwa unakataa.akampaka masizi kichwani. Akampiga mgongoni Abdul akalala. Alikuja amka anashika mashine.imerudi. Alifurahi sana aisee akaanza ruka ruka. Ndi kutueleza kweli alitaka kumla yule binti ila ndo akagundua yupo flat.

Na pia usiku alienda kukojoa haja ndogo ikatokea nyuma maji mengi sana. Tulijikuta tunacheka sana.

Baada ya siku tatu mzee akatwambia sasa muda umefika kama tupo tayari jioni tutaondoka wote.

Nakumbuka tulibeba maji tu kwenye vibuyu. Tulitembea sana tukipanda milima na kushuka,vijito na mito hatimaye tukafika kwenye mti mkuuuubwa sana. Mzee akatwambia tumefika tutulie hapo atuelekeze mambo ambayo yanaenda tokea.....

Nitaendelea.
Umeishia part 3 au unaendelea?

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom