Visa Card Vs Master Card

Viper

JF-Expert Member
Dec 21, 2007
3,667
1,400
Wakuu ....

naomba mwenye uwelewa wa hivyo vitu viwili anieleze Tofauti yake ni nini hasa ?!

sssssssssssssssssssss
Visa_Master_Card_Logos.jpg
 
Zote ni kadi za benki zinazorahisisha matumizi ya fedha. Zote ni kampuni za Kimarekani. Unaweza ukazipata katika namna mbili; kama debit card au kama credit card.

Debit card inachukua nafasi ya pesa taslimu. Yaani badala ya kubeba hela na kuzitumia ktk malipo yako, unaweza ukatumia debit card iliyounganisha moja kwa moja na checking account yako. Ukinunua kitu au huduma basi unaichanja tu hiyo debit card yako na hela zinatoka moja kwa moja kwenye akaunti yako kwenda kwa huyo unayemlipa. Hii inahitaji kimashine cha kuchanjia. Pia unaweza kulipia hivyo kwa njia ya simu au mtandao.

Credi card ni kama mkopo. Badala ya kupewa mkopo wa pesa taslimu unapewa ki-card hicho badala yake. Na chenyewe unakitumia kama ilivyo debit card lakini tofauti ni kwamba hela itokayo kwenye credit card si yako. Ni mkopo na hivyo itabidi uulipe kwa kadri utumiavyo (ukopavyo).

Nimeeleweka?
 
Zote ni kadi za benki zinazorahisisha matumizi ya fedha. Zote ni kampuni za Kimarekani. Unaweza ukazipata katika namna mbili; kama debit card au kama credit card.Debit card inachukua nafasi ya pesa taslimu. Yaani badala ya kubeba hela na kuzitumia ktk malipo yako, unaweza ukatumia debit card iliyounganisha moja kwa moja na checking account yako. Ukinunua kitu au huduma basi unaichanja tu hiyo debit card yako na hela zinatoka moja kwa moja kwenye akaunti yako kwenda kwa huyo unayemlipa. Hii inahitaji kimashine cha kuchanjia. Pia unaweza kulipia hivyo kwa njia ya simu au mtandao.Credi card ni kama mkopo. Badala ya kupewa mkopo wa pesa taslimu unapewa ki-card hicho badala yake. Na chenyewe unakitumia kama ilivyo debit card lakini tofauti ni kwamba hela itokayo kwenye credit card si yako. Ni mkopo na hivyo itabidi uulipe kwa kadri utumiavyo (ukopavyo).Nimeeleweka?
Excellent N.N
 
Jamaa hapo juu ameongea vizuri sana. Sasa ikija suala la kulipia vitu kwenye internet, unatumia credit card, huwezi tumia debt card mpaka uende kwenye benki yako waiwezeshe kufanya hivyo. Ciao!
 
Zote ni kadi za benki zinazorahisisha matumizi ya fedha. Zote ni kampuni za Kimarekani. Unaweza ukazipata katika namna mbili; kama debit card au kama credit card.

Debit card inachukua nafasi ya pesa taslimu. Yaani badala ya kubeba hela na kuzitumia ktk malipo yako, unaweza ukatumia debit card iliyounganisha moja kwa moja na checking account yako. Ukinunua kitu au huduma basi unaichanja tu hiyo debit card yako na hela zinatoka moja kwa moja kwenye akaunti yako kwenda kwa huyo unayemlipa. Hii inahitaji kimashine cha kuchanjia. Pia unaweza kulipia hivyo kwa njia ya simu au mtandao.

Credi card ni kama mkopo. Badala ya kupewa mkopo wa pesa taslimu unapewa ki-card hicho badala yake. Na chenyewe unakitumia kama ilivyo debit card lakini tofauti ni kwamba hela itokayo kwenye credit card si yako. Ni mkopo na hivyo itabidi uulipe kwa kadri utumiavyo (ukopavyo).

Nimeeleweka?

nimekualewa 100% mkuu

ahsante
 
Master Card ni kadi ya benki inayokuwezesha kuchukua pesa kwenye ATM yeyote duniani iliyopo katika mfumo huo wa MASTER. Kwa mfano kama unayo master card ya CRDB unaweza kuchukua pesa kwenye ATM ya Exim, NBC au Backlays etc ...

Visa Card ni kadi ya benki inayokuwezesha kuchukua pesa kwenye ATM za benki yako peke yake. Kama unayo visa card ya CRDB huwezi kuitumia kuchukua pesa kwenye ATM ya NBC, Exim au Backlays
 
Huo ni uongo! Mimi ninazo zote, Mastercard na Visa (check card and platinum check card, respectively). Na nina uwezo wa kuchukua hela katika ATM yoyote ile. Hata zile ATM zisizo za benki yangu. Nikichukua hela kwenye ATM ambazo si za benki yangu natozwa ada ndogo.
 
Safi sana. Kuna wana JF wanadhani kwamba ni lazima wachangie hata kama hawajui kitu.
 
Master Card ni kadi ya benki inayokuwezesha kuchukua pesa kwenye ATM yeyote duniani iliyopo katika mfumo huo wa MASTER. Kwa mfano kama unayo master card ya CRDB unaweza kuchukua pesa kwenye ATM ya Exim, NBC au Backlays etc ...

Visa Card ni kadi ya benki inayokuwezesha kuchukua pesa kwenye ATM za benki yako peke yake. Kama unayo visa card ya CRDB huwezi kuitumia kuchukua pesa kwenye ATM ya NBC, Exim au Backlays

sio kweli mpendwa.

mimi kuna wakati natumia tembo card visa na nachukua hela kwenye ATM za mabenki yote ndani na hata nikisafiri nje!

majibu ya NN na changman kwa pamoja yanatosheleza mia kwa mia.

ubarikiwe sana
 
Master Card ni kadi ya benki inayokuwezesha kuchukua pesa kwenye ATM yeyote duniani iliyopo katika mfumo huo wa MASTER. Kwa mfano kama unayo master card ya CRDB unaweza kuchukua pesa kwenye ATM ya Exim, NBC au Backlays etc ...

Visa Card ni kadi ya benki inayokuwezesha kuchukua pesa kwenye ATM za benki yako peke yake. Kama unayo visa card ya CRDB huwezi kuitumia kuchukua pesa kwenye ATM ya NBC, Exim au Backlays

Hapo kwenye red umesema uongo. Kama ilivyo master card ndivyo ilivyo Visa card. Kazi zake ni zile zile. Unaweza kuitumia Visa kadi kupata cash kutoka kwenye ATM yoyote ila utapata local currency za sehemu ulipo. Kama account yako iliyounganishwa na Visa card yako iko kwenye Euro, ukija Tanzania unaweza kwenda kwenye ATM za international banks na kuchukua pesa lakini kwa Tshs.

Tiba
 
Je kama nina AMEX na Discovery Cards nawezafanya cash withdrawals ktk ATM za bongo?
Je naweza-swipe AMEX na Discovery kwenye pumps za gas stations, registers za super markets au malls za hapo Dar, Arusha, Mwanza etc?
 
Naona lile wazo lako la kutaka kurudi uko serious... Na huwezi Swipe AMEX na Discovery kwenye pumps za gas stations, registers za Super markets wala malls... Kwanza kwa mfano Dar kwenyewe mall ipo moja tu!!...lol... Hata hivo welcome back Sherriff....
 
Different Brands..., Same Job...
credit/debit (it does what is says) debit (using what you have) credit (loan according to your limit and you will pay interest)

Usage.... (swipe, online, ATMS...)
Thats means you will have a card

Virtual Credit / Debit Cards (Prepaid One Time Cards)
Hapa unanunua Kadi ambazo zimejazwa pesa tayari (kwa wale wenye credit score mbovu au hawawezi kupata credit/debit card) na unaweza ukazitumia kununulia vitu online (ebay, amazon, n.k) au kufungua account ya paypal au Google Account au kulipia Google Adwords..

Kumbuka kinachohitajika kwenye Credit card ni Jina la Mwenye Kadi, Credit Card Number na CVS number ambazo ni number tatu za mwisho kwenye kadi yako.... (kwahiyo kampuni za virtual credit cards zinakupa hizo information hence unaweza kununua vitu online)
 
Huo ni uongo! Mimi ninazo zote, Mastercard na Visa (check card and platinum check card, respectively). Na nina uwezo wa kuchukua hela katika ATM yoyote ile. Hata zile ATM zisizo za benki yangu. Nikichukua hela kwenye ATM ambazo si za benki yangu natozwa ada ndogo.

Nyani wacha uongo kwa Tanzania inaweza kuwa tofauti hata nchi nyingine kuna cards ambazo huwezi kuchukua mpunga kwenye benki nyingine. Inategemea na mtoa card kakupa masharti gani. unless unapalilia yaliyopo USA.

BTW Tanzania unaweza kuchukua pesa kutoka kwenye mashine za Barclays tu kama una card kutoka nchi za magharibi na hivi vibenki vingine hupati kitu.
 
Huna hata uhakika na unachokiongea halafu unadiriki kuniita mimi muongo.
 
Nilikuwa Tanzania last week sikuweza kupata pesa kwa kadi kwenye bank zisizo Barclays, na hata ile cash back sahau ...... .... khe khe khe kheeeeeeeeeeeeeeee uhakika 100% soma BTW .... .....
 
Naona lile wazo lako la kutaka kurudi uko serious... Na huwezi Swipe AMEX na Discovery kwenye pumps za gas stations, registers za Super markets wala malls... Kwanza kwa mfano Dar kwenyewe mall ipo moja tu!!...lol... Hata hivo welcome back Sherriff....

ADii umeshaanza....ha ha ha!
Ahsante kwa kunijulisha hilo la kuhusu AMEX na Discovery cards.
Kurudi bado kidogo nitapiga box mpaka kibanda changu kiishe kwanza kule maeneo ya Bunju then ndio hesabu za kurudi. Box tamu na halimtupi mtu banaa
 
Nyani wacha uongo kwa Tanzania inaweza kuwa tofauti hata nchi nyingine kuna cards ambazo huwezi kuchukua mpunga kwenye benki nyingine. Inategemea na mtoa card kakupa masharti gani. unless unapalilia yaliyopo USA.

BTW Tanzania unaweza kuchukua pesa kutoka kwenye mashine za Barclays tu kama una card kutoka nchi za magharibi na hivi vibenki vingine hupati kitu.

Mkuu as long as una logo ya visa ama mastercard kwenye debit/credit card yako unachukua mkwanja popote na ndio nimekuwa nikifanya hivyo miaka nenda miaka rudi miji tofauti, states tofauti, ATM's tofauti na benk tofauti. Sijaona mahali wamesema Visa only ama MC only. Labda bongo
 
BTW Tanzania unaweza kuchukua pesa kutoka kwenye mashine za Barclays tu kama una card kutoka nchi za magharibi na hivi vibenki vingine hupati kitu.

Not True! Maestro za UBS zinatumika kwenye ATM za CRDB!
 
Back
Top Bottom