Visa Application Fees zinazotozwa na Serikali ya Tanzania ni chanzo cha mapato kilichotelekezwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Visa Application Fees zinazotozwa na Serikali ya Tanzania ni chanzo cha mapato kilichotelekezwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Patriote, Feb 21, 2012.

 1. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #1
  Feb 21, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Nimepitia Visa application form ya Tanzania inayotolewa na ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza nimebaini kuwa Form hiyo haina ubora unaotakiwa (kama ilivyojadiliwa kwenye thread mojawapo). Aidha, nlienda mbali zaidi kutaka kujua kiasi kinachotozwa yaani visa application fee. Kwa bahati mbaya form hizi hazioneshi kiasi unachopaswa kulipia i.e Visa Application Fee, bei hizo zipo kwenye maelezo ya ziada sasa cjui kama maelezo hayo hutolewa kwa mdomo au lah!!!Hili gap la information laweza kutumika kwa ajili ya ufisadi. Ni mategemeo yangu kuwa kulitakiwa kuwepo na sehemu imeainisha kiasi kinachopaswa kulipwa ndani ya visa application form na iwe clearly stated kuwa ni Non Refundable kama nchi nyingine zinavyotufanyia tukiapply kwenda kwao.

  Aidha, inashangaza sana kuona nchi yetu inatoza visa application fee ndogo sana ilihali kila siku nchi inalalamika kuwa haina vyanzo vya mapato. Ukitaka kuapply visa ya Tanzania kutoka U.K ada yake ni just £38 sawa na TZS 96,164/=Kwa Tourist/Holiday visa single entry only na Business visa fees ni £38 single entry valid for 2 months or Multiple entry 6 months £80 and 12 months £100 (multiple entry permits holder a maximum of 2 months stay in Tanzania per visit). Ni imani yangu kuwa hii ni maximum fees kutozwa na nchi yetu mana kama waingereza wanatozwa hivi, wageni wengine lazma itakuwa either sawa na hii au chini ya hapa.

  Sasa kwa bei hizo kweli kwanini nchi isitokee chini kiuchumi???Kwenda nchi za wenzetu ni laki 3-5 kwanini sisi tunajirahisi hivi ilihali kwetu kuna maresources ya kutosha na ndiyo yanayowafanya hawa wageni waje kwetu??kama nchini kwetu kusingekuwa na marasilimali haya tuliyonayo na yanayowasukuma wageni kulazimika kuja mnadhani wangekuja???Kwa jinsi wageni walivyo wengi hapa nchini, Visa application fee ingekuwa kubwa either wasingekuwa wengi kama leo au nchi ingepata mapato mengi sana tena kiulaini kabisa. Kama visa application fee ingekuwa laki tatu, chukulia wageni wapo laki moja tu hapo serikali ingeingiza TZS 30 Billions, Hivi sasa kwa idadi hiyo ya wageni (yaani 100,000) kwa bei inayotozwa na serikali (Tsh 96, 164) nchi inapata 9.6 Billions. Je tunapoteza Tsh ngap kwa uzembe wa kutoreview application fees zetu???Tena sio ajabu hiyo fee iliyopo ina miaka zaidi ya kumi.

  Mimi nadhani kuna haja ya kureview hizi Visa Application Fees, bei hizi zinaonesha kuwa hatupo serious na labda ndio maana wazungu wanasema kama Rais angepunguza 10% ya jitihada anazotumia kuzunguka kuombaomba misaada na kuhudhuria mikutano isyo na tija na muda huo angetumia kureview policies/plans/tozo mbalimbali. Nchi ingekuwa sehemu nzuri ya kuishi. Je mnaonaje wana JF???
   
 2. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #2
  Feb 21, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Nchi gani hiyo iliyokaribu na tanzania wanalipa hiyo hela kwa ajili ya Visa mkuu? Otherwise, ujue bado nchi zetu ziko remotely controlled pamoja na kuwa tunajiita tuko huru na kila kitu lakini suala la kutegemea badget kutoka kwa mzungu bado hatuko huru.
   
 3. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #3
  Feb 21, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Sijasema nchi iliyo karibu na Tanzania, nimesema kwenda nchi za wenzetu unatozwaa kati ya laki 3-5. Nenda hapo Umoja house pamoja na balozi za jirani na umoja house utaelezwa. Suala la kupandisha visa application fee halihitaji consensus ni nchi kutangaza kuwa imepandisha visa application fees full stop.

  Huitaji kikao cha umoja wa mataifa kupandisha visa application fee ya nchi yako, nchi za wenzetu ukiamka asubuhi unafungua mtandao unakuta tangazo kuwa visa application fee imechange full stop, huna wa kumuuliza kwanini. Wewe ukiona hiyo bei ni kubwa basi kaa kwenu mana kwenda kwa watu sio basic need.
   
Loading...