Virusi vya corona: Watu 10 Nchini India wamekufa kwa kunywa vitakasa mikono baada ya uuzaji pombe kupigwa marufuku

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,520
9,322
People using hand sanitiser in Kolkata, India in July


Watu 10 wamekufa kwa kunywa kitakasa mikono kilichochanganywa kwa pombe baada ya uuzaji pombe kupigwa marafuku katika kijiji kilichopo jimbo la Andhra Pradesh nchini India.

Kijiji cha Kurichedu kimewekewa hatua ya kutotoka nje kama njia moja ya kukabiliana na ongezeko la maambukizi ya Virusi vya Corona.

Polisi wa eneo la Siddharth Kaushal alisema kuwa watu waliokufa walikuwa wamechanganya kitakasa mikono na vinywaji vitamu mfano wa soda.

Watu hao walikuwa waraibu wa pombe, aliongeza, walikuwa wameanza kunywa mchangayiko huo siku 10 kabla ya kufa.

"Tunachunguza ikiwa kitakasa mkono kilikuwa na sumu nyengine yoyote," Bwana Kaushal amewaarifu wanahabari.

Aliongeza kwamba wametuma sampuli za vitakasa mkono vingine kufanyiwa uchunguzi
 
Back
Top Bottom