Virusi vya Corona Virus - Elimu Kwa Njia ya Mtandao

Mlenge

R I P
Oct 31, 2006
2,125
2,291
Habarini,

Kutokana na tishio la ugonjwa wa Covid-19 utokanao na virusi vipya vya corona, upo uwezekano wa mashule kuja kulazimika kufungwa katikati ya muhula, japo ugonjwa huo haujafika Tanzania.

Ili kujiandaa na janga hilo, matumizi ya elimu kwa masafa ni kitu kifaacho.

Kwa sasa, Gestalt Open School, inaandaa miundombinu ya kuwezesha wanaotaka kujielimisha kwa kutumia mtandao wa Internet na simu zao ili kujipatia elimu popote walipo. Miundombinu hiyo inaweza kuwafaa wote wengine wanaotaka kujipatia elimu.

Nini maoni yako kuhusu njia hii ya Gestalt Open School kuweka mazingira ya kujipatia elimu kwa njia ya masafa? Nini kiongezwe au kupunguzwa? Waweza pia kutuma imeili kwa: info@gestalt.co.tz

UPDATE 1: Virusi vya korona vimebainishwa kuathiri walau mtu mmoja Tanzania. Kutokana na tishio hilo, mashule yameamriwa kufungwa.
 
Back
Top Bottom