Virusi vya Corona: Trump asema suala la kuvaa barakoa ni uchaguzi binafsi wa mtu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
Rais Donald Trump, ambaye siku zote amekuwa akipinga muongozo wa uvaaji barakoa uliotolewa na maafisa wa afya, amesema atavaa barakoa kama atakuwa ''katika mazingira ya watu yatakayomlazimu kufanya hivyo''.

Bwana Trump ambaye amekwepa kujitokeza mbele Umma akiwa amevaa barakoa, pia amekuwa akishikilia msimamo wake kuwa kufunika uso hakuhitaji kuwa suala la lazima katika kudhibiti kuenea kwa ugonjwa wa Covid-19.

Kauli yake aliyoitoa kwa Fox News imekuja siku moja baada ya kiongozi wa Republican kutoa wito kwa Bwana Trump kuvaa barakoa ili aoneshe mfano.

Majimbo kadhaa nchini Marekani yameshuhudia ongezeko la maambukizi na vifo siku za hivi karibuni. Marekani sasa ina watu zaidi ya milioni 2.6 waliothibitishwa kuambukizwa virusi vya corona na vifo zaidi ya 127,000.

Trump alisema nini kuhusu barakoa?
Kituo cha kudhibiti magonjwa (CDC) mwezi Aprili kilipowataka watu kuvaa barakoa au kujifunika na nguo wanapokuwa maeneo ya watu wengi ili kudhibiti kuenea kwa maambukizi, Bwana Trump aliwaambia wanahabari kuwa hatafuata kanuni hiyo.

''Sidhani kama nitafanya hivyo,'' alisema wakati huo. ''Kuvaa barakoa ninapowasalimia marais, mawaziri, maikteta, wafalme na malkia- kwa kweli sioni nikivaa.''

Lakini Trump amesisitiza mara kwa mara kuwa kuchagua kufuata muongozo wa wataalamu wa afya kuhusu barakoa ni suala la uamuzi binafsi.

Mwezi uliopita, aliliambia jarida la Wall Street kuwa baadhi ya watu huvaa barakoa kama jambo la kiasiasa dhidi yake.

BBC
 
Shithole President ameifanya US kua shithole Country Per se mpk wananchi wake wanakua denied kuingia EU, yaani anashindwa mpk na Algeria, Morocco ambao wataruhusiwa kuingia EU.

Kisa hatua zake dhaifu alizochukua khs mambo za Covid,yaani nchi kubwa/superpower imeshindwa hata kufanya contact tracing?It's weird.
 
Back
Top Bottom