Virusi vya Corona: Saudi Arabia yaweka marufuku ya Hija kwa wageni

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,861
Saudi Arabia imepiga maarufuku raia kutoka mataifa mengine kufanya ibada ya Hija nchini humo mwaka huu ili kudhibiti virusi vya corona.

Ni idadi ndogo tu ya watu wanaoishi kwa sasa katika ufalme huo watakaoweza kushiriki Hija, kulingana na tangazo lililotolewa kwenye vyombo vya habari vya taifa hilo.

Watu takriban milioni mbili vinginevyo wangetembelea Maka na Madina msimu wa kiangazi kwa ajili ya Hija hiyo inayofanyika kila mwaka kulingana na imani ya kiislamu.

Kumekuwa na hofu kwamba Hija inaweza kufutwa kabisa.

Kwa kawaida Hija ni moja ya vipindi muhimu katika kalenda ya dini ya Kiislamu.Lakini ni raia kutoka nchi nyingine ambao tayari ni wakazi wa Saudi Arabia watakaoruhusiwa kuhudhuria Hija ya mwaka huu.

Maafisa nchini humo wanasema hii ndio njia pekee itakayowezesha kufanya mipango ya kutokaribiana ambayo itawezesha watu wawe salama.

Saudi Arabia imerekodi visa vya corona 161,005 na vifo vilivyotokana na ugonjwa huo ni 1,307.

Iliweza kuondoa amri ya kutotoka nje mwishoni mwa juma.

Hijj ni nini?

Hija ni mojawapo ya nguzo tano za Kiislamu ambayo kila Muislamu hutakiwa kuitekeleza walau mara moja.

Kila Muislamu, mwenye afya nzuri na aliye na uwezo anapaswa kutimiza nguzo hii ili kuishi maisha mazuri na ya uwajibikaji, kwa mujibu wa dini ya Kiislamu.

Mahujaji hukusanyika mjini Mecca kusimama mbele ya Kaaba, wakimsifu Allah (Mola) Mungu pamoja.

BBC Swahili
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom