Virusi vya corona: Rais wa Tanzania anasema wagonjwa wanapungua, je yuko sahihi?

Masi Lambo

JF-Expert Member
Apr 8, 2020
532
360
Ukitaka kuwafurahisha wajinga, wape habari nzuri kuhusu habari mbaya, hata kama si ukweli na baada ya kuwarubuni wakuamini wewe tu. Je, ni kweli maambukizi ya corona yamepungua Tanzania?

Na Peter Mwai na Christopher GilesBBC Reality Check

Ibada ikiendelea kanisani Tanzania - waumini wakiwa wamekaribiana bila kukaa umbali unaoshauriwa
Rais wa Tanzania John Magufuli amesema wagonjwa wa virusi vya corona katika hospitali mbalimbali nchini humo wamepungua sana, ingawa serikali haijatoa takwimu rasmi za viwango vya maambukizi kwa wiki tatu.

Kiongozi huyo mara kwa mara amesisitiza kwamba watu hawafai kuwa na hofu kuhusu ugonjwa huo. Hatua zake zimeyatia wasiwasi mataifa jirani na mashirika ya kimataifa.

Tanzania imeruhusu safari za ndege za kubeba abiria za kimataifa kurejea na wageni watakaokuwa wakiwasili hawatawekwa kwenye karantini ya lazima ambayo awali ilikuwa siku 14.

Dkt Magufuli ametangaza pia tarehe ya kufunguliwa kwa vyuo na pia kurejelewa kwa michezo nchini humo.
Je, tunafahamu nini kuhusu kuenea kwa virusi vya corona nchini Tanzania?

Kuna takwimu?
Serikali ilisitisha utangazaji wa takwimu za ugonjwa huo mara kwa mara mwezi Aprili baada ya rais kulalamika kwamba desturi ya kutangaza idadi ya wagonjwa ilikuwa inaongeza hofu. Alisema ilifaa pia maafisa kuangazia waliokuwa wanapona ugonjwa huo.

Kituo cha Kudhibiti Magonjwa cha Umoja wa Afrika wiki iliyopita kilitoa wito kwa Tanzania kutoa takwimu na kwa wakati.
Alhamisi wiki hii, kiongozi wa wa Afrika CDC Dkt John Nkengasong alisema Tanzania bado haijawasilisha taarifa kwa kituo hicho ingawa mawasiliano yanaendelea.

Takwimu rasmi za mwisho za Tanzania zilitangazwa 29 Aprili na waziri mkuu ambapo wagonjwa walikuwa 480, na waliokuwa wamefariki kutokana na ugonjwa huo walikuwa 21.

Zanzibar baadaye ilitangaza ongezeko la wagonjwa mara moja, mnamo 7 Mei walipotangaza wagonjwa 29 wapya. Hiyo ilifikisha idadi ya wagonjwa Tanzania hadi 509.

Rais Magufuli - hapa akionekana Desemba 2019 - amekosolewa kwa kutotoa takwimu kuhusu maambukizi
Rais Magufuli Jumapili iliyopita alitoa takwimu kiasi kuhusu wagonjwa wa Covid-19 waliokuwa wamelazwa katika hospitali na vituo mbalimbali nchini humo.

Alisema idadi ya wagonjwa katika hospitali mbili kubwa jijini Dar es Salaam ilikuwa imeshuka kutoka 228 hadi 18, na kutoa pia takwimu za hospitali nyingine nchini humo. Hata hivyo, hakusema idadi hiyo imeshuka kutoka lini hadi lini.

Ni vigumu kuthibitisha takwimu hizo, na pia ni vigumu kupata takwimu za kiwango cha maambukizi na idadi ya vifo kwa sasa nchini humo.

"Tanzania kwa muda mrefu imekuwa na sheria kali zinazominya uhuru wa kujieleza na uhuru wa wanahabari," anasema Roland Ebole, ambaye ni mtafiti wa kanda katika shirika la Amnesty International.

"Sasa, tunashuhudia sheria hizo zikitumiwa katika njia kubwa zaidi kuwalenga wale wanaozungumza, hasa kuhusu Covid-19," anasema Bw Ebole.
 
Hapa jf pekee inaweza kukusaidia kujua takwimu iwapo membaz watakuwa wakweli katika majibu yao; nani miongoni mwetu ana ndugu au jamaa yake ambaye yuko hospital kwa ajili ya Covid19, au amepoteza ndugu au jamaa yake kwa Covid19?

Utajua kama imepungua au hali ni mbaya kama tunavyodhani.
 
Back
Top Bottom