vipindi vya ITV na mustakabali wa taifa la Tanzania! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

vipindi vya ITV na mustakabali wa taifa la Tanzania!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by RC., Jul 15, 2012.

 1. R

  RC. JF-Expert Member

  #1
  Jul 15, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 446
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sisi watanzania tunaoitakia mema taaluma ya uandishi wa habari na utangazaji,tunashindwa kuamini kuwa haya yanayofanyika ITV hayajaonwa na mmiliki na watangazaji wa kituo hiki!kwani kuna vipindi hivi,sport kizaazaa!dk 45,na malumbano ya hoja,ni vipindi vinavyolenga kutafiti na kuibua hoja juu ya mikwamo mbalimbali ambayo taifa letu linatafuta njia mbadala ya kujikwamua kutoka kwenye mikwamo hiyo,lkn sijaelewa nini madhumuni ya vipindi hivi,kwani vipindi hivi vimekuwa BIAS sana kwani kwa muda sasa vpindi hivi vinaendelea kukosa mvuto kutoka kwa wananchi na wadau mbalimbali wa ITV.

  Nitajaribu kuchambua kipindi kimoja baada ya kingine,nikianza na kipindi cha sport kizaazaa!kipindi hiki ni kizuri sana hususani kwenye maswala ya michezo hasa kipindi hiki ambacho taifa letu liko kwenye mkwamo wa kupata timu mbalimbali za kuliwakilisha taifa kwenye mashindano ya aina mbalimbali,lkn kipindi hiki kimekuwa kinawaalika watu walewale,mawazo yaleyale sura zilezile kujadili soka na michezo mingine utafikiri wadau wa soka la Tanzania ndiyo hao tu,kwanini wasialike na wengine ambao wanaujuzi na uelewa mpana kwenye soka la ndani na la kimataifa kama SHAFFII DAUDA,EDO KUMWEMBE Na wengine ili kunogesha kipindi?badala yake ni walewale akina HOZA,Na wapiga soga wengine wengi,,ushauri,,naomba muandaaji wa kipindi hiki abadili mfumo mzima wa uendeshaji wa kipindi hicho ili kuipa changamoto jamii alikwa kwenye kipindi;

  kipindi cha dk45,ndugu semunyu namshangaa sana kipindi chake ni kizuri sana kwa mustakabali wa taifa letu,lkn jamaa huyu amekuwa BIAS sana kwenye swala zima la uteuzi wake wa watu wa kuwahoji kwani kila kukicha utasikia leo tutakuwa na wasira,samwel sitta,benard membe,mary nagu,...kwa kutaja wachache.hivi viongozi ni hao tu? jaribu kualika na viongozi wa vyama vingine ambavyo navyo vinamajembe ya kufafanua mada kwa mfano,CUF(LIPUMBA NA WENGINE),TLP(LYATONGA NA WENGINE),CHADEMA(Dr W.SLAA NA WENGINE) kwa kutaja vichache....

  ushauri kwakuwa kipindi hiki kimepoteza mvuto wake ni bora ukakiboresha kwa;1;kuuliza maswali magumu kwa viongozi hawa ili tuwe tunapata kujua uwezo wao wa kujenga hoja juu ya mambo mbalimbali yanayohusu jamii,.;2;kuruhusu maswali kwa wasikilizaji ili tujiridhishe kwa mambo mbalimbali ambayo yanaongelewa hapo na kuwafanya wahojiwa kuwa wakweli kwenye mada husika;3;na mwisho jaribu kuuliza maswali mengi ili muhojiwa asipate nafasi ya kupiga porojo za kisiasa...

  Kipindi cha malumbano yahoja;kipindi hiki pia kinagusa hisia za watanzania wengi haswa wale ambao wanaitakia mema nchi hii;lkn kipind hiki kwa muda sasa kimekuwa kikialika watu hususani wachangiaji wengi wao ni wanafunzi wa Elimu ya juu,na wadau wa siasa walewale mara chache sana utaona sura ngeni humo,sasa nauliza hivi wachangiaji hao ndiyo wenyewe wanaojua kujenga hoja?,,,ushauri.,,jitahidini kualika wachangiaji wengine ili tuone utofauti wa mawazo chanya yanayoletwa na wachangiaji hao ili tuondoe shaka kuwa mnatumika kuwaandaa watu hapo kushika madaraka hapo baadaye.

  Jambo jingine tunaomba kituo hiki kiwe kinarusha vipindi vya Bunge ili watanzania wengi waweze kuona LIVE nini wawakilishi wao wanafanya bungeni badala ya kurusha bongo fleva wakati wanapambana kuokoa taifa letu,jipambanueni kama star tv,.mwisho niko mbali sana na Tanzania hivyo basi mkimuona MENGI na HAO WALENGWA muwafikishie ujumbe huu kwa manufaa ya taifa letu MUNGU MBARIKI R.C Aendelee kuelimisha umma.

  MUNGU IBARIKI NCHI YANGU TANZANIA Asanteni..
   
 2. T

  TATOO Senior Member

  #2
  Jul 15, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 113
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Acha majungu yako wewe kama umetumwa na CCM n TBC yake umefulia mbaya sana ....unachitakiwa kuweka kichwani mwako ni kwamba nchi hii hakuna TV ambayo inatoa taarifa za usawa na haki bila kuficha kama ITV na yenye vipindi vya maana kama ITV....so unataka na wao waanze kuficha matatizo ya wananchi kama ya chama cha majizi???CCM.......ITV kula mzigo na kwa taarifa yako hadi wewe na tbc yenu mtakosa wa kuliza km hyo tbc yenu ipo.....na hata matangazo mtakosa na itafikia mda mtajinyima kazi wenyewe....
   
 3. R

  RC. JF-Expert Member

  #3
  Jul 15, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 446
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  changia hoja acha kubwabwaja najua watu kama ninyi ni wavivu wa kusoma usifikiri na kuona ndani ya box kama hivi!
   
 4. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #4
  Jul 15, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,016
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  ITV shida inaajiri watangazaji wasio na uwezo.
  TBCccm wala sio hedek kwetu
  Chanel ten star tv kidogo hawajawa infiltrated kiivo
   
 5. R

  RC. JF-Expert Member

  #5
  Jul 15, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 446
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni kweli wangebadilika sasa wawe kama wenzao mlimani TV,AU CITIZEN.
   
 6. M

  Mngendalyasota Senior Member

  #6
  Jul 16, 2012
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Au kama STAR TV.Nawapenda sana wazee wa Rocky City na taarifa zao ambazo ni well balanced.
   
 7. n

  nyangasese Senior Member

  #7
  Jul 16, 2012
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Star tv inakuja kasi, itv kaeni chonjo mtakua kama tbc
   
 8. W

  WaMzizima Senior Member

  #8
  Jul 16, 2012
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Usisahau vilevile kwenye ITV ni lazima waseme kiongozi wao Reginald Mengi oopsss!! sorry Dr Reginald mengi anafanya nini hata kama haina maana yeyote, mfano; leo hii dr mengi alikuwa nyumbani tu amepumzikaa au Leo hii Dr Mengi kakutana na blaa blaa blaa...who cares...gosh!!

  vilevile wanakera na tabia yao ya kuonyesha nusu ya taarifa ya habari kucover whatever Mengi anachofanya hata kama ni pumba...gosh the guy has a really big ego.
   
 9. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #9
  Jul 16, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,149
  Likes Received: 10,500
  Trophy Points: 280
  Nachelea kukubaliana na wewe.
   
 10. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #10
  Jul 16, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280
  Kama kile kipindi cha sport ni fujo tu huwezi kujifunza kitu.
   
 11. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #11
  Jul 16, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Shafi Dauda na Eddo Kumwembe wana upeo wa michezo wale? This must be a joke!
   
 12. N

  NG'ONGOVE Senior Member

  #12
  Jul 16, 2012
  Joined: Apr 28, 2012
  Messages: 151
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mimi nakubaliana na wewe hasa kwenye redi kijani na bluu. p'se ITV chukueni ushauri muufanyie kazi
   
 13. M

  MUNYAMAKWA Member

  #13
  Jul 16, 2012
  Joined: Jun 15, 2012
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuwa biased? Mbona hili liko wazi, tena kuna kitu kinaitwa 'kipima joto' ambacho kinaendeshwa sio kitaalam ,mfano unatupatia asilimia ya matokeo bila kutuambia idadi ya watu waliopigia kura hoja hiyo. Statistically kuna idadi inayotakiwa kufikiwa ili matokeo yawe yanawakilisha jamii iliyokusudiwa.Hebu imagine kama watu 6 ndo waliojotokeza kuchangia kwenye hicho kipima joto chao ,je hapa utapata uhalisia wa jambo lililokusudiwa kuifikia jamii.Msifiche elezeni total number of respondents acheni ubabaishaji na kuendesha vipindi as if mko kwenye old stone age.
   
 14. Ungana

  Ungana JF-Expert Member

  #14
  Jul 16, 2012
  Joined: Jul 16, 2011
  Messages: 358
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dk.45 za next week ni lile lile JOKA LA MDIMU bado...hivi vipindi ni MZAHA,period!
   
 15. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #15
  Jul 16, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kweli kipindi hicho kinachosha sana ,kwa upande wangu nakiona hakina tofauti na zecomedy ,tena zecomedy wanabadilisha mada ,ila hawa sport kizaazaa habari ni zile kwa zile wakiwalaumu walewale.

  Tatizo hawa ITV na TBC wanaidumaza Tanzania kwa kuifanya ni ndogo sana na habari zao zote ni kwa waishio hapo Dsm tu ,ukienda kwenye vipindi vya shule basi ni shule za DSM tu ,yaani kila kitu ni kutuonyesha wachovu wa DSM ,wamechoooka !
   
 16. L

  Lugeye JF-Expert Member

  #16
  Jul 16, 2012
  Joined: Apr 18, 2011
  Messages: 1,074
  Likes Received: 1,375
  Trophy Points: 280
  itv wale wemebadilika sana nahisi magamba wameshajipenyeza pale kuna mkona wao sasa hivi STAR TV inafanya vizuri mno huwezi kuamini
   
 17. daniel don

  daniel don Member

  #17
  Jul 16, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kaka umeonyesha ni jinsi gani umekuwa mfuatiliaji mzuri wa vipindi mbalimbali vya Luninga nchini, vipindi ambavyo umevitaji na kufanunua ni kweli kabisa kuna kila sababu wahusika wafanye mabadiliko ya washiriki. Imefika hatua mshiriki mmoja anapokosekana watazamaji wanatambua kuwa fulani leo hayupo..Ni vipindi vizuri vimekosa mawazo mapya, vile vile waongeze washiriki wengi wa njia ya simu..Hakuna cha majungu kaka huo ni mtazamo wako kama wanavyosema wachangiaji wengine!:second:
   
 18. Mandingo

  Mandingo JF-Expert Member

  #18
  Jul 16, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 3,380
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  Nakubaliana na wewe 100%!
  ITV mbadilike yaani mnaboa sana utakuta kutwa nzima wanashinda na bbc,cnn,dw... lakini jioni angalia internatonal news!hamna kitu kabisa sasa badala ya kushinda na hayo ma bbc + ccn + dw basi kipindi hiki mtuonyeshe bunge!
  Ukija kwenye habari za A.mashariki ndio sifuri kabisa!yaani habari 2 mmemaliza
  kama hamjajipanga kutoa habari za A.Mashariki muache kuliko huu usanii mnao fanya...
  PONGEZI ZA DHATI KWAO STAR TV
  JAMAA WANAPIGA KAZI!
   
 19. Mandingo

  Mandingo JF-Expert Member

  #19
  Jul 16, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 3,380
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  Nakubaliana na wewe 100%!
  ITV mbadilike yaani mnaboa sana utakuta kutwa nzima wanashinda na bbc,cnn,dw... lakini jioni angalia internatonal news!hamna kitu kabisa sasa badala ya kushinda na hayo ma bbc + ccn + dw basi kipindi hiki mtuonyeshe bunge!
  Ukija kwenye habari za A.mashariki ndio sifuri kabisa!yaani habari 2 mmemaliza
  kama hamjajipanga kutoa habari za A.Mashariki muache kuliko huu usanii mnao fanya...
  PONGEZI ZA DHATI KWAO STAR TV
  JAMAA WANAPIGA KAZI!
   
 20. kadoda11

  kadoda11 JF-Expert Member

  #20
  Jul 16, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 16,293
  Likes Received: 8,388
  Trophy Points: 280
  hivi kumbe bado wanaendela kurusha kile kipindi!.niko mbali na bongoland,nimemiss zile porojo mkuu.....wale wachangiaji kila mtu anataka kuonyesha uwezo wake wa kupiga porojo za soka fitna.ni porojo tupu.
   
Loading...