Vipindi vya dini katika shule za msingi na Sekondari za Serikali vifutwe

Wale waliofanikiwa kupata elimu ya darasani angalau ya darasa la saba na kuendelea watakumbuka vipindi vya dini ambavyo vilitengwa rasmi kulingana na madhehebu mbalimbali na wanafunzi wote ni lazima kuhudhuria katika vipindi hivyo.

Mara nyingi vipindi hivi huwa Ijumaa kuanzia muda wa saa nne ili kuwapa fursa waislamu kwenda msikitini kwa sababu mara nyingi wao huwa hawatumii madarasa kuswali katika vipindi vya dini kama wenzao Wakristo.

Wakati mjadala wa tija elimu yetu ukiwa mkali bungeni na mtaani ipo haja ya kuliangazia pia jambo hili na kuona kama kuna tija yeyote kuwa na hivi vipindi.

Ukiangalia kwa makini utagundua vipindi hivi vya dini havina tija yoyote kwa wanafunzi zaidi ya kuwachukulia muda wao ambao ungweza kutumika katika mambo mengine muhimu kama sanaa za uchoraji, uchongaji, kuimba, kuogelea, ushonaji n.k

Ni wakati sasa mamlaka zinazohusika na elimu zitoe muongozo wa vipindi hivi kufutwa na kuongeza mambo mengine secular au kupunguza muda wa wanafunzi kukaa darasani.

Kizazi cha ibilisi alie laaniwa
 
Sijasema dini ifutwe katika taifa, nimesema vipindi vya dini viondolewe katika shule za serikali. Mbona hakuna vipindi vya dini katika ofisi nyingine za serikali na tunaishi vizuri tu.
Vipindi vya dini mashuleni vinakukwaza nini wewe?

Umeshupalia tu vifutwe vifutwe! ili iweje?

We MCHAWI nini?
 
Maadili mazuri uanzia utotoni.
ni vizuri watoto wakamjua mungu tangu wakiwa wadogo.
Na mashuleni NI SEHEMU sahihi ya kumjua mungu.
Sijasema dini ifutwe katika taifa, nimesema vipindi vya dini viondolewe katika shule za serikali. Mbona hakuna vipindi vya dini katika ofisi nyingine za serikali na tunaishi vizuri tu.
 
Hivi kwa nini serikali haiwapi fursa waganga wa kienyeji pia kutoa elimu yao mashuleni?
Inabidi na wao wadai vipindi vyao mashuleni.
Vipindi vya dini mashuleni vinakukwaza nini wewe?

Umeshupalia tu vifutwe vifutwe! ili iweje?

We MCHAWI nini?
 
Hivi kwa nini serikali haiwapi fursa waganga wa kienyeji pia kutoa elimu yao mashuleni?
Inabidi na wao wadai vipindi vyao mashuleni.
Shetani hawezi kupewa fursa yoyote.

Kama unapenda sana uchawi kawafundishe mama zako huko!

Eboo!
 
Sayansi inavyozidi ku expand, taratibu tu uzito wa haya masomo ya dini yanazidi kupungua

Vipindi vya dini miaka ya nyuma ni tofauti na sasa, sio tu shuleni hata makanisani. Na ndio maana unakuta mchungaji anahubiri kuhusu udangaji kanisani, au siasa kwa maana ndizo mada ambazo anaweza kushawishi watu wamsikilize kuliko habari za mungu

Ni system moja ya kiupigaji hivi iliyozalisha wapambanaji waliopewa jina la watumishi wa mungu ila mimi nawaita wajasiliamali maana wengi wana products zao kabisa wamezi brand mafuta ya upako, maji nk.
 
Watu badala ya kujibu hii mada kwa hoja wanaanza kuleta nonsense na personal attacks.

Alafu hawa wanaopiga promo hapa tabia zao na dini ni tofauti trust me asilimia 90 ya wote waliocomment kuhusu vipindi vya dini vimewasaidia na blahblah wapo kwenye ule uzi wa kula tunda kimasihara.
Na wao ndio walikuwa wakitongozana na kufanya ngono hukohuko shule baada ya kutoka kwenye hivyo vipindi vya dini.

Wewe unayesoma hapa na mfuasi wa dini nafsi yako yenyewe inakwambia ukweli.

Haya ndio mazao ya dini Unafiki na Uvivu wa kufikiri hata uwe na PhD.

hivi vipindi havina faida wala impact yoyote kwa wanafunzi tabia chafu, uhuni, ngono zembe, mimba za utotoni, uvutaji bangi na ujeuri uko palepale.
Mojawapo wa faida za vipindi vya dini katika shule za msingi na sekondari ni kuwajengea utamaduni wa kutambua na kuvumilia itikadi za dini/imani zingine. Ndiyo maana tunaweza kuwa na staha dhidi ya imani ya mwingine.
 
Taifa au familia yoyote bila misingi ya dini (haijalishi Ni dini ipi)

Iyo familia itageuka familia ya hovyo Sana.
- Kuua
-kubaka
-wizi
-Chuki
-unafiki
-mapenz na Ndugu
-mapenz ya jinsia moja
-mapenz kinyume na maumbile
-mapenz na wanyama
-ukatili
- ulevi na madawA
-ushirikina
-umalaya na ukahaba
-Nidhamu mbovu
-uzalendo sifuri
-utii hamna

Ndo maana serikali
imeruhusu na inazilea taasisi za kidini (hazilipi Kodi) ili kuisaidia serkali kujenga mshikamano, Aman, utulivu na kutunza ustaarabu wa wananchi wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
Naona apo kwenye mapenzi no reference ya uzi wetu uleee
 
Freedom of Religions, as long as hakuna mwanafunzi anatakaye lazimishwa kuhudhuria kipindi cha dini....
Na kwa wanafunzi ambao hawato hudhuria kipindi chochote cha Dini wawe na kipindi chao husika
 
Shule zote nilizosoma ilikuwa ni lazima kuhudhuria vipindi vya dini, na viranja walikuwa wanawawinda wanafunzi waliokuwa hawaendi kwenye hivyo vipindi. Pia walimu walikuwa wanacharaza sana bakora wakikuta nje ya kipindi wakati wenzako wakiwa wanaendelea na kipindi.

Kwa wanafunzi wasiotaka kwenda kwenye hivyo vipindi waachwe wajisomee au wakacheze uwanjani.
Freedom of Religions, as long as hakuna mwanafunzi anatakaye lazimishwa kuhudhuria kipindi cha dini....
Na kwa wanafunzi ambao hawato hudhuria kipindi chochote cha Dini wawe na kipindi chao husika
 
Kwa hiyo watu ambao hawajasoma kabisa au wamesoma shule zenye wanafunzi wa dini moja tu hawana staha wala hawawezi kuvumilia dini nyingine?
Mojawapo wa faida za vipindi vya dini katika shule za msingi na sekondari ni kuwajengea utamaduni wa kutambua na kuvumilia itikadi za dini/imani zingine. Ndiyo maana tunaweza kuwa na staha dhidi ya imani ya mwingine.
 
Shule zote nilizosoma ilikuwa ni lazima kuhudhuria vipindi vya dini, na viranja walikuwa wanawawinda wanafunzi waliokuwa hawaendi kwenye hivyo vipindi. Pia walimu walikuwa wanacharaza sana bakora wakikuta nje ya kipindi wakati wenzako wakiwa wanaendelea na kipindi.

Kwa wanafunzi wasiotaka kwenda kwenye hivyo vipindi waachwe wajisomee au wakacheze uwanjani.
Hizo ni sheria na lazima kuzifwata.
Huwezi jifanyia mambo unavyotaka wewe,
Ndiyo maana kuna kanuni na taratibu za shule,ukiona huwezi kuzifuata basi hama..
Siyo muda wa michezo wewe upo kulala,muda wa dini wewe unaenda kucheza,muda wa kusoma wewe uende kwenye dini.
Kila jambo lina wakati wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wale waliofanikiwa kupata elimu ya darasani angalau ya darasa la saba na kuendelea watakumbuka vipindi vya dini ambavyo vilitengwa rasmi kulingana na madhehebu mbalimbali na wanafunzi wote ni lazima kuhudhuria katika vipindi hivyo.

Mara nyingi vipindi hivi huwa Ijumaa kuanzia muda wa saa nne ili kuwapa fursa waislamu kwenda msikitini kwa sababu mara nyingi wao huwa hawatumii madarasa kuswali katika vipindi vya dini kama wenzao Wakristo.

Wakati mjadala wa tija elimu yetu ukiwa mkali bungeni na mtaani ipo haja ya kuliangazia pia jambo hili na kuona kama kuna tija yeyote kuwa na hivi vipindi.

Ukiangalia kwa makini utagundua vipindi hivi vya dini havina tija yoyote kwa wanafunzi zaidi ya kuwachukulia muda wao ambao ungweza kutumika katika mambo mengine muhimu kama sanaa za uchoraji, uchongaji, kuimba, kuogelea, ushonaji n.k

Ni wakati sasa mamlaka zinazohusika na elimu zitoe muongozo wa vipindi hivi kufutwa na kuongeza mambo mengine secular au kupunguza muda wa wanafunzi kukaa darasani.
Yoda toka uache skul ambapo vipindi vya dini vilikuwepo umekuwa huru na muda mwingi tuu umegundua nn cha maana ambacho wasoma bible na quruan hawajakigundua??
 
Back
Top Bottom