Vipi Refa Anapoamua Kukwatua!? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vipi Refa Anapoamua Kukwatua!?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by X-PASTER, Jul 22, 2009.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Jul 22, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Vipi refa anapoamua kukwatua?
  Napenda nami leo nichangie kidogo kile ambacho kinajiri hapa JF. Kwa muda mrefu sana, mambo ya siasa na dini ndio yamekuwa kama ajenda kuu za wadau humu ndani ya forum. Tatizo tu linapokuja watu kuchangia basi tunashuhudia mambo mengi yakijichanganya, kiasi ya kwamba ile radha ya mjadara, na ule ukomavu wa fikra ambao tunatarajia kuoneka humu upotea kama vile mvuke unavyo potea hewani.

  Wako wale ambao hukusudia kusema uongo ili kulinda ufisadi wao na kuwalazimishia maovu watu ambao hawana uovu. Wako pia ambao wanajitahidi kudumu katika kusema ukweli hata kama unawaudhi wakubwa na jamaa zao. Hawa mara nyingi wameitwa kwa majina wasiyostahili kama vile wachochezi, hawakusoma au waliochoka na amani ama waleta vurugu na kadhalika.

  Kwa bahati mbaya uongo unaosemwa mara nyingi ni katika lengo la kuwalazimisha watu maovu, unaelekezwa kwa wale ambao wanaonekana kama kikwazo kwao, waswahili tu hao.

  Mara kadhaa na kwa nyakati tofauti viongozi wa dola wemetoa shutuma za uongo dhidi ya Waswahili hawa tena shutuma za kufanana kwa miaka tofauti. Kwa kweli ukiyatafakari kwa makini utakubaliana nami kuwa shutuma hizo ni za kupangwa na kutolewa kwa makusudi maalumu katika kuficha ufisadi na hujuma juu ya Waswahili hao.

  Alhamdulillah, pamoja na propaganda dhidi ya Uswahili na Waswahili, wako watu ambao bila kuogopa vitisho na shutuma za dola na vyombo vya habari vya mlengo wa kando, wamedumu katika ukweli.

  Kuna wale ambao wao ujiona kuwa si waswahili na wapo karibu sana na serikali, hao lolote watalosema hata kama linakwenda nje ya katiba serikali ulichukua na kulikumbatia.

  Hao wanao itwa waswahili, ambao kwa njia moja ama nyingine wenyewe wanaamini kuwa wamechangia kwa kiwango kikubwa sana katika kuleta amani na uhuru wa nchi hii na uzuri hawakuwa wadini kama watu wanavyo waona, ila uzalendo wao ulikuwa kwanza kisha imani ya dini zao baadae. Ila kwa bahati nzuri ama mbaya wakaja kusahaulika kwenye kula hayo matunda ya uhuru. Kisingizio kilichotolewa ni kuwa ‘Hawa Waswahili hawakusoma' na kwa hali hiyo hawastahili kabisa kuwepo kwenye taasisi za serikali, ila wale wachache ambao walionekana kuwa ni watiifu kwao.

  Propaganda hii ikaenezwa kisiri siri kila kukicha kiasi ya kwamba ikaja kuonekana kama vile kweli miongoni mwa jamii ya Watanzania.

  Wale ambao walijitokeza kutetea haki za kimsingi za kila raia, wakaitwa wachochezi na waliochoshwa na amani. Na wakashughulikiwa ipaswavyo. Maana wengine hata maiti zao hazijulikani zimestiriwa ardhi gani, kama hazikuwa chakula cha samaki baharini.

  Ebu basi tuangalie hii nadharia ya hawa waswahili ambao tunaambiwa kuwa hawakusoma dhidi ya wale waliosoma....!(?)

  Miaka ile ya uhuru mpaka kipindi kile kabla ya Azimio la Arusha na vita vya kagera, nchi ilikuwa katika neema fulani, japokuwa si kulinganisha na nchi zingine zilizokuwa zishaendelea, lakini afadhali tulikuwa kwenye amani ya kweli. Japokuwa kulikuwa na ufisadi wa kuwakumbatia wakurugenzi na mameneja wa makampuni na mashirika yaliokuwa hayafanyi vizuri, hata ivyo hatukusikia sana malalamiko kutoka kwa wananchi, labda kwa kuwa vyombo vya habari vya wakati ule vilikuwa vinamilikiwa na wenye nchi. Na pia hakukuwa na uhuru wa habari kama sasa.

  Kosa lilifanyika tena kubwa sana la kutaifisha makampuni na mashamba ambayo wasomi wetu walidai kuwa hayo makampuni yameanzishwa kwa jasho la kina baba kabwela, tutakapoweza kuyamiliki hapo ndipo tutaweza kufaidi vizuri matunda ya uhuru wa nchi hii. Na kweli kabisa makampuni, mashamba na hata majumba yalichukuliwa kinguvu bila ya kuwapatia wenyewe fidia kwa zile mali zao. Tukasahau kuwa hayo mashamba na hayo makampuni, soko la bidhaa zake uko nje linamilikiwa na hao tulio amua kuwanyang'anya leo. Kesho yake tunawapelekea hao hao kuwauzia kile tulicho wapora jana.

  Tulishuhudia sana walafi (wasomi) jinsi walivyokuwa wakihamishwa kutoka kampuni au shirika ili kuelekea lile na hali ya kuwa wanajulikana wazi kabisa kuwa utendaji wao haukuwa na tija zuri. Yapo wapi yale mashamba makubwa ya katani, miwa, Pamba na menginewe? Makampuni ambayo yaliweza kuhimili mikiki mikiki ya urafi wa wasomi ni yale tu ambayo kwa njia moja ama nyingine yalikuwa bado yapo indirect kwa wenyewe.

  Hali ilikuja kuwa na mbaya zaidi pale tulipoamua kuivamia nchi huru, kwa kisingizio kuwa tumevamiwa na joka kuu. Kwa hali hiyo basi sababu tushaipata kwa kuwa tushakuwa na chuki tayari, kisha nia tulishakuwa nayo na vile vile uwezo tunao. Watanzania watafunga mikanda tu, hawana tatizo watafumilia.

  Baada ya vita tukashurutishwa kuifunga hiyo mikanda kwa ahadi ya miezi kumi na minane mambo yatakuwa tu mazuri. Ni kweli mambo yalikuwa mazuri, maana mpaka leo hii ile laana bado inatula na kutumaliza, miezi kumi na minane zimegeuka karne kumi na nane. Wachilia mbali hao ndugu zetu ambao walijitolea kwenda kufa nchi zingine ambazo ziliamua kutumia mtutu wa bunduki kujipatia uhuru wa nchi zao.

  Miaka ile mwanzoni mwa miaka ya themanini, nchi iliingia kwenye balaa kubwa la njaa na ukame wa bidhaa adimu, ikawa haitoshi, serikali hiyo hiyo ya wasomi ikaamua kutaifisha kile kidogo kilichokuwa kinapatika kwa wale wananchi ambao kwa jitihada zao binafsi waliamua kuleta bidhaa kutoka nchi za jirani.

  Tukaingizwa kwenye maduka ya kaya, kula na kununua kwa vidaftari, nunua sukari na unga wa muhogo, au kile chakula ambacho baadae ilikuja kujulikana ni chakula cha farasi kule Marikani (Unga wa manjano).

  Ufisadi huu unaopigiwa kelele leo ni zao la utawala m-bovu uliokuwepo tangia awamu ya kwanza. Refa tuliyekuwa naye alikuwa refa mchezaji, refa ambaye akuchelewa kumshika mtu jezi pale anapoona wale wasomi wameelemewa. Mapenzi yake yalikuwa wazi dhahiri shahiri. Tusishangae hizi dua zinazo ombwa na hao wazulumiwa, M'Mungu anapozijibu matokeo yake uwakumba waliokuwemo na wasio kuwemo. Hali hii ya refa mchezaji imerithiwa miaka na miaka, kwa kuwapata wale ambao watahakikisha kuwa wanawashughulikia waswahili kila wanapokuja juu, au kuulizia haki zao za kimsingi.

  Mijadala mingi inapoletwa humu ndani ya forum, mara zote kama si mara nyingi imejaa ushabiki wa kisiasa na udini zaidi ya uzalendo. Tumeshuhudia miswada ikipelekwa kombo kwa maksudi kabisa ili ionekane kuwa ni hatari kwa usalama wa taifa letu kwa kuwa tu imeletwa na waswahili ambao wanaonekana kuwa ni walalamishi tena ni wadini. Lakini je unapo lalamika na usipo sikilizwa ndio unyamaze? au mpaka pale utakapo popolewa na jiwe ndio utajuwa kuwa hawa jamaa wamechoka?. Nilikuwa nategemea sehemu kama hii hapa ndani ya forum, watu wangekuwa wazalendo zaidi kuliko kukumbatia vyama vyao vya siasa na udini.

  Tuchukulie suala limeletwa na Muislam au Mkristo, kwenye kulijadili kama tutaondoa udini na kuona yale mazuri yaliyomo kwenye hiyo ajenda basi lichukuliwe na kufanyiwa kazi, na yale mapungufu yarekebishwe na kama hayawezekani yaondolewe ili lionekane kuwa ni suwala la kitaifa zaidi.

  Kwa jinsi hiyo hiyo hata kwenye vyama vya kisiasa. Ikiwa chama cha CUF, CHADEMA, CCM, TLP, JAHAZI na vinginevyo, vimeleta hoja ambayo inaonekana kuwa ni nzuri na ina faida kwa jamii nzima basi yachukuliwe yale mazuri na kufanyiwa kazi ili kweli JF ionekane kuwa ni sehemu ya great thinkers, lakini wapi, propaganda za usomi zimewakaa, kila jambo linachukuliwa ni la kidini zaidi kuliko hali halisi ilivyo.

  Lakini hayo ya kujiita kuwa The Home Of Great Thinkers hayapatikani humu, jinsi ilivyo hao wasomi ndio hao hao ambao wamo humu, ambao tunaweza kuwaita ni mamluki, wapo kupinga kila jambo, hata liwe zuri vipi kwao ni baya tu, maana wapo hapa kulinda maslahi ya mabwana zao, na uzalendo kwao ni msamiati tu uliopitwa na wakati. Yaani hauna maana yeyote.

  Hao wasomi wamelewa propaganda kiasi ya kwamba hawaoni mazuri ya upande wa pili. Ushabiki umekuwa mkubwa kiasi ya kwamba JF imekosa radha, ile changamoto ambayo ilitegemewa iwepo kutoka kwa wasomi ambao wenyewe wanajiita The Great Thinkers haipo na wala hakuna dalili za kuwepo.

  Serikali haijali matatizo yetu. Serikali ndiyo baba na haina budi kulea watoto wake. Sisi ndio watoto na hatuangaliwi. Hii ni serikali ya CCM na wanatuangamiza.

  Hivi karibuni Maaskofu wa kikatoliki walikuja na waraka wao na wamekusudia kuwafundisha waumini wao jinsi ya kuwachagua viongozi watakao waona kuwa wanafaa. Ili suala ukiliangalia juu juu, linaonekana kama ni zuri sana. Lakini je limezingatia utaifa?. Je hili suwala lilipoletwa humu ndani ya forum lilijadiliwa kwa kuzingatia uzalendo au tuliruhusu imani zetu zitawale kwanza kabla ya kuchaguwa yale mazuri yaliyomo kwanza.

  JF inasemekana ina ushawishi mkubwa sana huko kwenye jamii ya watanzania, je wachangiaji walishindwa nini kuwashauri hao maaskofu na waraka wao kuwa kwa kuwa hili suala linahusu nchi ambayo wakazi wake wana imani tofauti tofauti, je wameshirikishwa hao wote ili kujenga uzalendo wa kitaifa?.

  Kwani kulikuwa na ubaya gani kwa hao wasomi wa kikatoliki kuwaalika wenzao wa imani zingine na wale ambao hawana imani za kidini wakakaa pamoja na kushauriana kisha wakatoa tamko la pamoja? Sasa ikitokea kila dini kuamua kuwaelimisha wafuasi wao jinsi ya kuchaguwa kiongozi wanaye muona anafaa je tutafika?.

  Lilipokuja suwala la OIC, kwanini hayakuangaliwa yale mazuri yalio kuwemo ndani ya OIC kisha kukatolewa mapendekezo kutoka kwa wale ambao wanaona kuwa ni muhimu sana kwao kama Watanzania kuondoa kile ambacho kina watia wasiwasi juu ya icho kinachoitwa OIC?
  Najuwa kuwa mjadala kuhusu OIC bado unajadiliwa na serikali na bado kutoa maamuzi yake, kwani haujatupwa bado, vile vile hata waraka wa kanisa, bado haujawa adopted na serikali, bado unajadiliwa na kuna challenges toka kwa watu mbalimbali ingawa kuna baadhi ya watu wanasupport tu kwa sababu wao ni Wakatoliki, sio kwa sababu wanaunga mkoni hoja zilizomo. Pengine hata hawajausoma waraka wenyewe

  Kwa ujumla wanayosema Waislamu, wanayosema Maaskofu hawa, na walichosema Waheshimiwa wengine ni ukweli ambao kuupinga ni kuonyesha jinsi gani wewe unayepinga ulivyo kinyume na ukweli. Tunachotaka kukumbusha hapa ni kuwa kupingwa kwa wasema kweli na watendaji kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania sio jambo geni..

  Kilichokosewa tu hapa ni kuwa waliokua wakila na kipofu safari hii wamemshika kipofu mkono naye kapiga kelele sasa lazima nyama ndani ya bakuli zihesabiwe.

  Nakumbuka kisa kimoja, nilipokuwa napita kwenye viwanja vya kuchezea mpira, hususani watoto, nikakuta kuna mkusanyiko wa chama maarufu cha si-hasa... Mtoto mmoja mdogo, aliyekuwa amekasirika kwa sababu eneo lao la kuchezea mpira wao wa makaratasi (ndio) lilikuwa limeingiliwa, alichekesha watu. Mgombea aliposimama alisema: "CC motooo!!!" yule mtoto akajibu "Utatuunguzaaa!!" Watu walicheka, lakini mimi nilishituka. Kwa nini mtoto huyu hana hofu? Analeta utani kwenye siasa, tena anatania chama cha dola! Kwa vile watu walikuwa wachache kisauti chake kikali kilisikika mno.

  Cha kushangaza ni kwamba, hata wale walinzi wa dola na wale wengine waliokuwa ndani ya yunifomu za kijani na njano pia walivunjika mbavu. Japokuwa huo moto unawaunguza, lakini je wafanyeje na wao ndio taifa la kesho?

  Kumbukeni kwamba hata watu waovu hujiona wanayo haki ya kufanya maovu. Mwizi huona anayo haki ya kuchukua cha mtu mwingine. Mharibifu huona anayo haki ya kuharibu mali ya mwingine, vivyo hivyo mchokozi hujiona anayo haki ya kuchokoza. Fisadi hujiona ana haki ya kufanya ufisadi wake.

  Subirini tu tuone, maana panapofuka moshi pana moto. Panapo kusanyika Tai ujue kuna Mzoga. Lakini tena refa anapogeuka kuwa mchezaji, tena akakamata jezi ya mchezaji wa timu moja asipige bao, au refa anapoamua kukwatua hivi hivi wazi wazi, ujue maji yamezidi unga.

  Hivyo haki mnayoipigania ninyi wasomi ni hatari tupu.
  Kwa maana mmesahau kuwa kusema kweli ni sehemu ya uadilifu
   
  Last edited: Jul 26, 2009
 2. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #2
  Jul 22, 2009
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Huo mpango wenu wa kuigeuza Tanzania iwe Tanzanistan uishie huko huko kwenye mpaka wa Somalia na Kenya.
   
 3. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #3
  Jul 22, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Yale yale ya kutotaka kutumia neema ya akili aliyokupa Mola wako!
   
 4. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #4
  Jul 22, 2009
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Neema ya akili yangu inanisukuma kukataa kwa nguvu zote mpango wa baadhi ya waislam Tanzania wa kutaka kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya kidini (ya kiislam).

  Ninakuhakikishia kuwa mimi sitakuwa mmoja wa wale watakaokaa kimya na kuona nchi yetu ikigeuzwa kuwa Tanzanistani. Hayo mambo ya utawala wa kidini yaishie huko huko Afghanistan, somalistan, tukristani na kwingineko.

  Tanzania hii, tusio waislam tutaendelea kuishi pwani, tutakula kile roho inapenda, tuta - party till 6 in the morning, wadada zetu watavaa nguo zile wanazotaka, na watoto wetu watasoma kokote kule roho zao zinapenda. Wanawake watakuwa na haki sawa na wanaume. Wanawake wataruhusiwa kufanya kazi na kuendesha magari. Kila kitu kitaendelea kuwa cha uhuru na haki kwa kila mtu kama ilivyo sasa hivi.

  Udini wenu huu hautakaa ufanikiwe hata kama Kikwete akilikalia kimya hili jambo.
   
 5. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #5
  Jul 22, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kwani ukizungumza bila kutoa povu unahisi hutaeleweka!?

  Una ushahidi wowote ule, uliokupelekea kusema kuwa nchi inatakiwa kugeuzwa kuwa ivyo unavyo dai? Maana nimeona thread zako nyingi umeling'ang'ania sana ilo suala, au ndio upo kwenye campain + propaganda za kisomi?

  Ili tusikuwekwe kwenye kapu la kupuuzwa unaweza kuthibitisha hao?

  Na hizi nchi zipo bara lipi ndugu "somalistan, tukristani" Mini binafsi sijawahi kuzisikia, may be kwa kuwa si msomi kama wewe.
   
 6. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #6
  Jul 22, 2009
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Njia yoyote ile mtakayojaribu kuja nayo hapa - iwe ni kupitia OIC, mahakama ya kadhi, MoU, emancipation, nk; ukweli utabaki wazi kuwa Tanzania haitakuja kubadilishwa na kuwa nchi ya kiislam. Kituo kikubwa.

  Hayo mengine ya mapovu nadhani yanalenga zaidi kwako kuliko kwangu. Hapa ni msimamo mmoja. Tanzania haitakuwa nchi ya kiislam na kuwa chini ya sheria au mila za waarabu.

  Watu wenye udini kama wewe na mwenzako Game Theory mnaweza kuniweka kokote kule mnakotaka.

  Weka kikombe cha kahawa karibu na pua lako unuse harufu ya kahawa (smell the coffee). Mbinu zenu zimegundulika na sasa mtaishia kutapatapa tu mara ohhh CHADEMA watoe tamko .... ne mengine mengi.
   
 7. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #7
  Jul 22, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mkuu X-P,

  Naomba kukuuliza swali. Definition haswa ya Mswahili ni nini? Maana wengine tumezoea kusikia mtu akiwa tapeli au ana chelewa kwenye appointment kila wakati basi anaitwa Mswahili. So kwa ninvyo jua mimi mtu Mswahili kila siku anakua projeted as a negative person. Kwa hiyo labda wewe mkuu unaweza kusaidia katika kutu fafanulia wengine hilo.
   
 8. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #8
  Jul 22, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  asante kwa post yako, wote humu tuna haki ya kusema dukuku zetu kwa namna yoyote ile ya amani nadhani ndio maana hata wamiliki wa site uacha mjadala uendelee regardless of the controveries it may raise.

  mi nimeanza kukuelewa angle yako lakini pia we mwenyewe una raise unwanted attention kwa upande wako that is you send a little of negative vibes upon urself. kwa mfano kuna mtu hapo juu tayari kashaita unataka kuifanya tanzania iwe tanzanistan wakati hiyo post has nothing to do with religion(nilivyo elewa mimi) bali asking about our patriotism that is ni jinsi gani tunajiona watanzania kabla ya dini zetu. but kwa nini umuingize mungu kwa jina 'Allah' ukati kwenye huo utanzania unao utaka wewe na kwa maandishi yako wewe kwamba sisi tuwe wa tanzania kwanza kabla ya dini zetu uoni unawakera wengine kabla hata ya kusooma mada yenyewe vizuri. sisi wote tuna dini zetu lakini iwe imani zetu si vibaya kusimamia na kupigania dini yako mkuu hila kila kina mahala pake na kwa upande wangu nadhani kabla sijaingia kwenye post hii, before i got to this post i had to go through Jukwaa la Siasa haya niambie Mh, kuna Allah kweli kwenye uzalendo au kuna mungu ibariki Tanzania ni vizuri kuipenda na kuitetea dini yako lakini basi ziwe mahala na sehemu zinapo husika.
   
  Last edited: Jul 22, 2009
 9. J

  JokaKuu Platinum Member

  #9
  Jul 22, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,794
  Likes Received: 5,062
  Trophy Points: 280
  X-PASTER,

  ..hata mimi naona jina lako "x-paster" linaweza kuwa-distract watu wengine ktk kusoma hoja zako.

  ..halafu unajiita natural born extremist, kwanini usijiite natural born moderate?

  ..hoja yako nitaichangia baada ya kuitafakari.
   
 10. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #10
  Jul 22, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Wakiristo wanajifanya wajinga na hawayaelewi mambo na hujifanya hivyo pale wanapoona labda kwa fikra zao waislamu watafaidika ,hii kusema kweli kwa wale Wakristo wenye tabia hii ,hao wanakuwa na roho mbaya na pia wanakuwa na choyo ,ukiona mtu ana weka mguu katika jambo ambalo labda kwa fikra zake litawaneemesha wengine basi mtu huyo muweke kwenye kundi la watu wenye choyo na ni watu wabaya sana ,awe Muislamu au Mkiristu na hili sio analifanya kwenye mambo makubwa yahusuyo Taifa ,hata nyumbani kwake,au ndani ya mjumuiko wa wenzake ,akili yake ni ya uchoyo na huwa hataki mwengine apate.Watu wa aina hii inabidi muwaelewe na mapema ni watu ambao roho zao ni dhaifu na mara nyingi hujifanya wao ndio wao tu ,hakuna mwengine ,watu wa aina hii ni hatari katika maendeleo ya nchi na jamii kwa ujumla.
  Hivi Tanzania kujiunga na IOC wakiristu mtapata hasara gani ? Waislamu kuwana na sehemu ya kujiamulia baadhi ya mambo yao yanayohusu sheria zao pakiwepo na nguvu ya serikali kuitambua hali hiyo ,Wakiristu mtapata mkosi gani ? Mlete jawabu tu ambalo litaonyesha kuwa mtakuwa waathirika ,vinginevyo ni choyo tu ,na huo ndio ukweli ,sababu ya msingi hakuna ,mnadai Katiba inavunjwa ,hapo penye hicho kifungu hakuna uhusiano kabisa na suala hili,ila mawazo yenu finyu yamewapelekea baadhi yenu kupitisha roho mbaya kwa vile wanavyoona na kutafsiri wanavyotaka wao.
  Wakiristu wana mashule na mahospitali kibao,lakini wakisikia Waislamu wanataka kujenga shule au zahanati ,utawaona mabega yamewatoka na ushingo kuunyoosha juu ,wakichunguza ilikuwaje kuwaje serikali ikawaruhusu kupata msaada mkubwa huo,msaada huo wameupata vipi ,nani amewapa yaani wanakwenda kwenda mpaka wanahakikisha hakuna wanachokipata waislamu ,wanachotaka hawa ni watu wote waelekee kwenye mashule na mazahanati wanayoyamili wao.Wakiwa na tamaa labda waislamu watabadili dini na kuingia kwenye ukiristo ,mtafundisha mpaka mtachoka lakini kwa hilo halina nafasi kabisa ,maana hakuna mtoto wa kiislamu anaefundishwa ulevi ni haramu ila kila anaeinukia anajua kuwa jambo hilo limekatazwa ndani ya dini automatic analifahamu hilo ,kufuata au kutofuata ni suala jingine ,kwa tamaa hiyo mliyonayo watu wataitafuna feza na hakuna atakae ingia kwenye ukafiri.
   
 11. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #11
  Jul 22, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kwani mpaka leo Watanzania hususan JF members tunazijadili mada zetu kutokana na majina...!?
  Kwani kuwa natural born extremist ni jinai? Nakumbuka enzi ya vita vya kagera, tuliwahi kuambiwa kuwa rais wa Uganda enzi hizo ni jokakuu, vipi hapo ndugu joka kuu, kuna uhusiano wowote na yule wa Uganda enzi zile? (samahani lakini)
  Natarajia busara toka kwako... JokaKuu.
   
 12. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #12
  Jul 22, 2009
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Mkuu X Pastor mimi la kwangu ni swali dogo,ninaomba unifahamishe hivi opposite ya neno 'msomi' ni 'mswahili'? nauliza swali hili baada ya kunukuu maneno yako hapo juu na yameonyesha hivyo.
   
 13. M

  MgonjwaUkimwi JF-Expert Member

  #13
  Jul 22, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 1,288
  Likes Received: 521
  Trophy Points: 280
  Maswali mazito haya! Kama kawaida hautajibiwa unachouliza, bali utapata jibu la ukiukwaji wa katiba.
   
 14. K

  Kinte Member

  #14
  Jul 22, 2009
  Joined: Jun 27, 2009
  Messages: 74
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Ni vyema ukaanza kwa kutupa faida kabla hujaanza kutuuliza kuhusu hasara.
   
 15. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #15
  Jul 22, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  X-Paster,
  Umesema kweli.
  Umenikumbusha msemo wa waswahili(sijuwi kama ndo hao wanaoitwa si wasomi au wadini) wanasema "...hasidi hana sababu.." Wewe utawaona tu watakavyo kuja hapa badala ya kutafakari na kutoa hoja au mchango wa ulichokieleza hapo, wao watakuja na kauli paraganyifu na kejeli bas.
   
 16. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #16
  Jul 22, 2009
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Acha kulialia basi
   
 17. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #17
  Jul 22, 2009
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Sana sana utakachoambiwa ni kuwa Tanzania itapata misaada toka nchi za kiarabu na/au za kiislam. Yaani mpaka leo hii watu wanadhani kuwa nchi yetu itaendelezwa na umatonya?!?!
   
 18. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #18
  Jul 22, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Do I have to?
   
 19. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #19
  Jul 22, 2009
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Absolutely
   
 20. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #20
  Jul 26, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Habri zenu wakuu, hii ni ile thread iliyonyofolewa, bahati nzuri katika kutafuta tafuta nikaikuta tena, na hapa nimeiwakilisha kwa mara nyingine.

  Shukran
  _____________________

  Vipi Refa Anapoamua Kukwatua?

  Napenda nami leo nichangie kidogo kile ambacho kinajiri hapa JF. Kwa muda mrefu sana, mambo ya siasa na dini ndio yamekuwa kama ajenda kuu za wadau humu ndani ya forum. Tatizo tu linapokuja watu kuchangia basi tunashuhudia mambo mengi yakijichanganya, kiasi ya kwamba ile radha ya mjadara, na ule ukomavu wa fikra ambao tunatarajia kuoneka humu upotea kama vile mvuke unavyo potea hewani.

  Wako wale ambao hukusudia kusema uongo ili kulinda ufisadi wao na kuwalazimishia maovu watu ambao hawana uovu. Wako pia ambao wanajitahidi kudumu katika kusema ukweli hata kama unawaudhi wakubwa na jamaa zao. Hawa mara nyingi wameitwa kwa majina wasiyostahili kama vile wachochezi, hawakusoma au waliochoka na amani ama waleta vurugu na kadhalika.

  Kwa bahati mbaya uongo unaosemwa mara nyingi ni katika lengo la kuwalazimisha watu maovu, unaelekezwa kwa wale ambao wanaonekana kama kikwazo kwao, waswahili tu hao.

  Mara kadhaa na kwa nyakati tofauti viongozi wa dola wemetoa shutuma za uongo dhidi ya Waswahili hawa tena shutuma za kufanana kwa miaka tofauti. Kwa kweli ukiyatafakari kwa makini utakubaliana nami kuwa shutuma hizo ni za kupangwa na kutolewa kwa makusudi maalumu katika kuficha ufisadi na hujuma juu ya Waswahili hao.

  Alhamdulillah, pamoja na propaganda dhidi ya Uswahili na Waswahili, wako watu ambao bila kuogopa vitisho na shutuma za dola na vyombo vya habari vya mlengo wa kando, wamedumu katika ukweli.

  Kuna wale ambao wao ujiona kuwa si waswahili na wapo karibu sana na serikali, hao lolote watalosema hata kama linakwenda nje ya katiba serikali ulichukua na kulikumbatia.

  Hao wanao itwa waswahili, ambao kwa njia moja ama nyingine wenyewe wanaamini kuwa wamechangia kwa kiwango kikubwa sana katika kuleta amani na uhuru wa nchi hii na uzuri hawakuwa wadini kama watu wanavyo waona, ila uzalendo wao ulikuwa kwanza kisha imani ya dini zao baadae. Ila kwa bahati nzuri ama mbaya wakaja kusahaulika kwenye kula hayo matunda ya uhuru. Kisingizio kilichotolewa ni kuwa ‘Hawa Waswahili hawakusoma’ na kwa hali hiyo hawastahili kabisa kuwepo kwenye taasisi za serikali, ila wale wachache ambao walionekana kuwa ni watiifu kwao.

  Propaganda hii ikaenezwa kisiri siri kila kukicha kiasi ya kwamba ikaja kuonekana kama vile kweli miongoni mwa jamii ya Watanzania.

  Wale ambao walijitokeza kutetea haki za kimsingi za kila raia, wakaitwa wachochezi na waliochoshwa na amani. Na wakashughulikiwa ipaswavyo. Maana wengine hata maiti zao hazijulikani zimestiriwa ardhi gani, kama hazikuwa chakula cha samaki baharini.

  Ebu basi tuangalie hii nadharia ya hawa waswahili ambao tunaambiwa kuwa hawakusoma dhidi ya wale waliosoma....!(?)

  Miaka ile ya uhuru mpaka kipindi kile kabla ya Azimio la Arusha na vita vya kagera, nchi ilikuwa katika neema fulani, japokuwa si kulinganisha na nchi zingine zilizokuwa zishaendelea, lakini afadhali tulikuwa kwenye amani ya kweli. Japokuwa kulikuwa na ufisadi wa kuwakumbatia wakurugenzi na mameneja wa makampuni na mashirika yaliokuwa hayafanyi vizuri, hata ivyo hatukusikia sana malalamiko kutoka kwa wananchi, labda kwa kuwa vyombo vya habari vya wakati ule vilikuwa vinamilikiwa na wenye nchi. Na pia hakukuwa na uhuru wa habari kama sasa.

  Kosa lilifanyika tena kubwa sana la kutaifisha makampuni na mashamba ambayo wasomi wetu walidai kuwa hayo makampuni yameanzishwa kwa jasho la kina baba kabwela, tutakapoweza kuyamiliki hapo ndipo tutaweza kufaidi vizuri matunda ya uhuru wa nchi hii. Na kweli kabisa makampuni, mashamba na hata majumba yalichukuliwa kinguvu bila ya kuwapatia wenyewe fidia kwa zile mali zao. Tukasahau kuwa hayo mashamba na hayo makampuni, soko la bidhaa zake uko nje linamilikiwa na hao tulio amua kuwanyang’anya leo. Kesho yake tunawapelekea hao hao kuwauzia kile tulicho wapora jana.

  Tulishuhudia sana walafi (wasomi) jinsi walivyokuwa wakihamishwa kutoka kampuni au shirika ili kuelekea lile na hali ya kuwa wanajulikana wazi kabisa kuwa utendaji wao haukuwa na tija zuri. Yapo wapi yale mashamba makubwa ya katani, miwa, Pamba na menginewe? Makampuni ambayo yaliweza kuhimili mikiki mikiki ya urafi wa wasomi ni yale tu ambayo kwa njia moja ama nyingine yalikuwa bado yapo indirect kwa wenyewe.

  Hali ilikuja kuwa na mbaya zaidi pale tulipoamua kuivamia nchi huru, kwa kisingizio kuwa tumevamiwa na joka kuu. Kwa hali hiyo basi sababu tushaipata kwa kuwa tushakuwa na chuki tayari, kisha nia tulishakuwa nayo na vile vile uwezo tunao. Watanzania watafunga mikanda tu, hawana tatizo watafumilia.

  Baada ya vita tukashurutishwa kuifunga hiyo mikanda kwa ahadi ya miezi kumi na minane mambo yatakuwa tu mazuri. Ni kweli mambo yalikuwa mazuri, maana mpaka leo hii ile laana bado inatula na kutumaliza, miezi kumi na minane zimegeuka karne kumi na nane. Wachilia mbali hao ndugu zetu ambao walijitolea kwenda kufa nchi zingine ambazo ziliamua kutumia mtutu wa bunduki kujipatia uhuru wa nchi zao.

  Miaka ile mwanzoni mwa miaka ya themanini, nchi iliingia kwenye balaa kubwa la njaa na ukame wa bidhaa adimu, ikawa haitoshi, serikali hiyo hiyo ya wasomi ikaamua kutaifisha kile kidogo kilichokuwa kinapatika kwa wale wananchi ambao kwa jitihada zao binafsi waliamua kuleta bidhaa kutoka nchi za jirani.

  Tukaingizwa kwenye maduka ya kaya, kula na kununua kwa vidaftari, nunua sukari na unga wa muhogo, au kile chakula ambacho baadae ilikuja kujulikana ni chakula cha farasi kule Marikani (Unga wa manjano).

  Ufisadi huu unaopigiwa kelele leo ni zao la utawala m-bovu uliokuwepo tangia awamu ya kwanza. Refa tuliyekuwa naye alikuwa refa mchezaji, refa ambaye akuchelewa kumshika mtu jezi pale anapoona wale wasomi wameelemewa. Mapenzi yake yalikuwa wazi dhahiri shahiri. Tusishangae hizi dua zinazo ombwa na hao wazulumiwa, M’Mungu anapozijibu matokeo yake uwakumba waliokuwemo na wasio kuwemo. Hali hii ya refa mchezaji imerithiwa miaka na miaka, kwa kuwapata wale ambao watahakikisha kuwa wanawashughulikia waswahili kila wanapokuja juu, au kuulizia haki zao za kimsingi.

  Mijadala mingi inapoletwa humu ndani ya forum, mara zote kama si mara nyingi imejaa ushabiki wa kisiasa na udini zaidi ya uzalendo. Tumeshuhudia miswada ikipelekwa kombo kwa maksudi kabisa ili ionekane kuwa ni hatari kwa usalama wa taifa letu kwa kuwa tu imeletwa na waswahili ambao wanaonekana kuwa ni walalamishi tena ni wadini. Lakini je unapo lalamika na usipo sikilizwa ndio unyamaze? au mpaka pale utakapo popolewa na jiwe ndio utajuwa kuwa hawa jamaa wamechoka?. Nilikuwa nategemea sehemu kama hii hapa ndani ya forum, watu wangekuwa wazalendo zaidi kuliko kukumbatia vyama vyao vya siasa na udini.

  Tuchukulie suala limeletwa na Muislam au Mkristo, kwenye kulijadili kama tutaondoa udini na kuona yale mazuri yaliyomo kwenye hiyo ajenda basi lichukuliwe na kufanyiwa kazi, na yale mapungufu yarekebishwe na kama hayawezekani yaondolewe ili lionekane kuwa ni suwala la kitaifa zaidi.

  Kwa jinsi hiyo hiyo hata kwenye vyama vya kisiasa. Ikiwa chama cha CUF, CHADEMA, CCM, TLP, JAHAZI na vinginevyo, vimeleta hoja ambayo inaonekana kuwa ni nzuri na ina faida kwa jamii nzima basi yachukuliwe yale mazuri na kufanyiwa kazi ili kweli JF ionekane kuwa ni sehemu ya great thinkers, lakini wapi, propaganda za usomi zimewakaa, kila jambo linachukuliwa ni la kidini zaidi kuliko hali halisi ilivyo.

  Lakini hayo ya kujiita kuwa The Home Of Great Thinkers hayapatikani humu, jinsi ilivyo hao wasomi ndio hao hao ambao wamo humu, ambao tunaweza kuwaita ni mamluki, wapo kupinga kila jambo, hata liwe zuri vipi kwao ni baya tu, maana wapo hapa kulinda maslahi ya mabwana zao, na uzalendo kwao ni msamiati tu uliopitwa na wakati. Yaani hauna maana yeyote.

  Hao wasomi wamelewa propaganda kiasi ya kwamba hawaoni mazuri ya upande wa pili. Ushabiki umekuwa mkubwa kiasi ya kwamba JF imekosa radha, ile changamoto ambayo ilitegemewa iwepo kutoka kwa wasomi ambao wenyewe wanajiita The Great Thinkers haipo na wala hakuna dalili za kuwepo.

  Serikali haijali matatizo yetu. Serikali ndiyo baba na haina budi kulea watoto wake. Sisi ndio watoto na hatuangaliwi. Hii ni serikali ya CCM na wanatuangamiza.

  Hivi karibuni Maaskofu wa kikatoliki walikuja na waraka wao na wamekusudia kuwafundisha waumini wao jinsi ya kuwachagua viongozi watakao waona kuwa wanafaa. Ili suala ukiliangalia juu juu, linaonekana kama ni zuri sana. Lakini je limezingatia utaifa?. Je hili suwala lilipoletwa humu ndani ya forum lilijadiliwa kwa kuzingatia uzalendo au tuliruhusu imani zetu zitawale kwanza kabla ya kuchaguwa yale mazuri yaliyomo kwanza.

  JF inasemekana ina ushawishi mkubwa sana huko kwenye jamii ya watanzania, je wachangiaji walishindwa nini kuwashauri hao maaskofu na waraka wao kuwa kwa kuwa hili suala linahusu nchi ambayo wakazi wake wana imani tofauti tofauti, je wameshirikishwa hao wote ili kujenga uzalendo wa kitaifa?.

  Kwani kulikuwa na ubaya gani kwa hao wasomi wa kikatoliki kuwaalika wenzao wa imani zingine na wale ambao hawana imani za kidini wakakaa pamoja na kushauriana kisha wakatoa tamko la pamoja? Sasa ikitokea kila dini kuamua kuwaelimisha wafuasi wao jinsi ya kuchaguwa kiongozi wanaye muona anafaa je tutafika?.

  Lilipokuja suwala la OIC, kwanini hayakuangaliwa yale mazuri yalio kuwemo ndani ya OIC kisha kukatolewa mapendekezo kutoka kwa wale ambao wanaona kuwa ni muhimu sana kwao kama Watanzania kuondoa kile ambacho kina watia wasiwasi juu ya icho kinachoitwa OIC?
  Najuwa kuwa mjadala kuhusu OIC bado unajadiliwa na serikali na bado kutoa maamuzi yake, kwani haujatupwa bado, vile vile hata waraka wa kanisa, bado haujawa adopted na serikali, bado unajadiliwa na kuna challenges toka kwa watu mbalimbali ingawa kuna baadhi ya watu wanasupport tu kwa sababu wao ni Wakatoliki, sio kwa sababu wanaunga mkoni hoja zilizomo. Pengine hata hawajausoma waraka wenyewe

  Kwa ujumla wanayosema Waislamu, wanayosema Maaskofu hawa, na walichosema Waheshimiwa wengine ni ukweli ambao kuupinga ni kuonyesha jinsi gani wewe unayepinga ulivyo kinyume na ukweli. Tunachotaka kukumbusha hapa ni kuwa kupingwa kwa wasema kweli na watendaji kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania sio jambo geni..

  Kilichokosewa tu hapa ni kuwa waliokua wakila na kipofu safari hii wamemshika kipofu mkono naye kapiga kelele sasa lazima nyama ndani ya bakuli zihesabiwe.

  Nakumbuka kisa kimoja, nilipokuwa napita kwenye viwanja vya kuchezea mpira, hususani watoto, nikakuta kuna mkusanyiko wa chama maarufu cha si-hasa... Mtoto mmoja mdogo, aliyekuwa amekasirika kwa sababu eneo lao la kuchezea mpira wao wa makaratasi (ndio) lilikuwa limeingiliwa, alichekesha watu. Mgombea aliposimama alisema: "CC motooo!!!" yule mtoto akajibu "Utatuunguzaaa!!" Watu walicheka, lakini mimi nilishituka. Kwa nini mtoto huyu hana hofu? Analeta utani kwenye siasa, tena anatania chama cha dola! Kwa vile watu walikuwa wachache kisauti chake kikali kilisikika mno.

  Cha kushangaza ni kwamba, hata wale walinzi wa dola na wale wengine waliokuwa ndani ya yunifomu za kijani na njano pia walivunjika mbavu. Japokuwa huo moto unawaunguza, lakini je wafanyeje na wao ndio taifa la kesho?

  Kumbukeni kwamba hata watu waovu hujiona wanayo haki ya kufanya maovu. Mwizi huona anayo haki ya kuchukua cha mtu mwingine. Mharibifu huona anayo haki ya kuharibu mali ya mwingine, vivyo hivyo mchokozi hujiona anayo haki ya kuchokoza. Fisadi hujiona ana haki ya kufanya ufisadi wake.

  Subirini tu tuone, maana panapofuka moshi pana moto. Panapo kusanyika Tai ujue kuna Mzoga. Lakini tena refa anapogeuka kuwa mchezaji, tena akakamata jezi ya mchezaji wa timu moja asipige bao, au refa anapoamua kukwatua hivi hivi wazi wazi, ujue maji yamezidi unga.

  Hivyo haki mnayoipigania ninyi wasomi ni hatari tupu.
  Kwa maana mmesahau kuwa kusema kweli ni sehemu ya uadilifu.
   
Loading...