Vipi ofisi ya makamu wa Rais imehamishiwa kwenye mbuga za wanyama serengeti?

Keynes

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
533
89
Jamani wana JF na wana jukwaa la siasa naomba kuuliza.
Je ofisi ya makamu wa rais imehamishiwa kwenye mbuga za wanyama siku hizi??...Maana tangu mwezi wa 12 mwaka jana vyombo vya habari vinaripoti yupo ziarani kwenye mbuga za wanyama na wakeze wawili!!
Je hii ndo ilikua sababu ya kugombea umakamu wa raisi? Miaka yote alikua kwenye uongozi hakupata fursa za kutembelea mbuga?? Mzee tunakuhitaji ofisini utatue matatizo ya nchi...loh!!!!
_DSC1066.JPG _DSC1058.JPG
 
Anapumzika mzee baada ya kazi kuzunguka nchi nzima kunadi ilani ya sisiem. Ninachoshangaa mke wake wa tatu kwa nini haendi nae huko!!
 
ahaaa...mkuu kuna mke wa tatu tena!!!
Tunamtaka arudi amshauri mkubwa wake kuhusu mauji ya arusha na mambo mengine waache mambo ya kula bata wakati raia tupo kwenye msiba.
 
Huwezi fanya kazi kila siku, na je ushasikia lini tena alikuwa likizo, serikalini huwa watu wanalimbikiza likizo so inawezekana nae ni miongoni mwao. Pili anatangaza mbuga waswahili nanyi mwende. Ukiuliza ushaona simba? Jibu ndiyo kwenye tv wakati wako hapo pua na mdomo. Go c them live.
 
Jamani wana JF na wana jukwaa la siasa naomba kuuliza.
Je ofisi ya makamu wa rais imehamishiwa kwenye mbuga za wanyama siku hizi??...Maana tangu mwezi wa 12 mwaka jana vyombo vya habari vinaripoti yupo ziarani kwenye mbuga za wanyama na wakeze wawili!!
Je hii ndo ilikua sababu ya kugombea umakamu wa raisi? Miaka yote alikua kwenye uongozi hakupata fursa za kutembelea mbuga?? Mzee tunakuhitaji ofisini utatue matatizo ya nchi...loh!!!!
View attachment 20030View attachment 20031

Upupu huo
 
Hawajali wananchi kwao uongozi ni neeme kwa wao na familia zao..
 
Utalii wa ndani.
Si unajua tena Zenji hakuna mbuga!!
Akimaliza Dr. zamu ya Shamsi Vuai inafuatia.
 
Anapumua huyo bwana na kula pension. Ndo mambo yetu wabongo kazi hatujafanya tunakimbilia kupumzika!
 
Jamani wana JF na wana jukwaa la siasa naomba kuuliza.
Je ofisi ya makamu wa rais imehamishiwa kwenye mbuga za wanyama siku hizi??...Maana tangu mwezi wa 12 mwaka jana vyombo vya habari vinaripoti yupo ziarani kwenye mbuga za wanyama na wakeze wawili!!
Je hii ndo ilikua sababu ya kugombea umakamu wa raisi? Miaka yote alikua kwenye uongozi hakupata fursa za kutembelea mbuga?? Mzee tunakuhitaji ofisini utatue matatizo ya nchi...loh!!!!
View attachment 20030View attachment 20031
Kumbuka ofisi yake inahusika na Mazingira pia, hivyo huko yuko kazini kuhakikisha Mazingira na viumbe walioko huko wanalindwa kwa manufaa ya taifa.
 
Na Familia "zake"!

Kumbe huyu jamaa "ameshaendelea" ndiyo maana na afya inaleta mgogoro - naona hata suruali inalegea!
 
Utalii wa ndani.
Si unajua tena Zenji hakuna mbuga!!
Akimaliza Dr. zamu ya Shamsi Vuai inafuatia.

Si mchezo Pinda alipokwenda kijijini kwake kwa likizo mlimmwagia sifa kibao hapa na haikuwa tatizo yeye kuchukua likizo ile kama ya wiki 2, lakini Bilal kuchukua likizo imekuwa tabu...Kweli hapa JF kunya anye kuku tu akinya bata kahara...nendeni MOI katoe usaha vichwani mwenu
 
Huwezi fanya kazi kila siku, na je ushasikia lini tena alikuwa likizo, serikalini huwa watu wanalimbikiza likizo so inawezekana nae ni miongoni mwao. Pili anatangaza mbuga waswahili nanyi mwende. Ukiuliza ushaona simba? Jibu ndiyo kwenye tv wakati wako hapo pua na mdomo. Go c them live.
Mi nakubali utalii wa ndani muhimu mkuu but kwa yeye kiongozi mwenye majukumu mazito kama yeye nadhani siku 2 au 3 zingemtosha....sasa karibu week 3 hii habari.
 
Huwa ananifurahisha sana na ile miwani yake anywayz apumzike maana umakamu wa rais siku hizi imekuwa ni kukata utepe na kuzindua visima vya maji
 
Back
Top Bottom