Vipi nimkatalie?

mahirtwahir

JF-Expert Member
Jan 12, 2013
613
311
Alinizani bandia,ndani ya maisha yake
Wala sikufikiria ,kma ntarudi kwake
Sitorudi abadani,sitorudi abadan
ni kheri niazirike

Lakini leo karudi,kama jambo halikua
Na macho yake shahidi,kaja kuniangukia
Kajaniomba nirudi mapenzi kuyarudia aaaa
Kaja omba samahani,vipi nimkatalie
Vipi nimkataliee?

Vikuba vya asumini,kaniletea tamasha
Mapenzi ya utotoni,leo kaja yakumbusha
Yanamwenda midomoni,kwa furaha na bashashaa
Kaja omba samahani,vipi nimkatalie.
Vipi nimkatalie?

Sikoai kunahibika,niko mwake mikononi
Uso nimeuvubika,fudi fudi kifuani
Kama mwana amefika,kwa mama mwenye imaniii
Kaja omba smahani,vipi nimkatalie
Vipi nimkatalie?


$ U r My Number 1 $
 
Malenga umebutua, ingawa unayo hoja,
shairi na mizania, wala hauwi kioja,
vina wewe zingatia, wapige chenga wakuja,
ndo zimwi likujualo, halikuli likakwisha!!!!!

kalamu menigomea, shairi nakata tama,
mengi ningeongelea, sikie mpaka kahama,
ngekuwa wayasomea, ungepata diploma,
mapenzi hayana fundi, ukifeli ndo umefeli.
 
Alinizani bandia,ndani ya maisha yake
Wala sikufikiria ,kma ntarudi kwake
Sitorudi abadani,sitorudi abadan
ni kheri niazirike

Lakini leo karudi,kama jambo halikua
Na macho yake shahidi,kaja kuniangukia
Kajaniomba nirudi mapenzi kuyarudia aaaa
Kaja omba samahani,vipi nimkatalie
Vipi nimkataliee?

Vikuba vya asumini,kaniletea tamasha
Mapenzi ya utotoni,leo kaja yakumbusha
Yanamwenda midomoni,kwa furaha na bashashaa
Kaja omba samahani,vipi nimkatalie.
Vipi nimkatalie?

Sikoai kunahibika,niko mwake mikononi
Uso nimeuvubika,fudi fudi kifuani
Kama mwana amefika,kwa mama mwenye imaniii
Kaja omba smahani,vipi nimkatalie
Vipi nimkatalie?


$ U r My Number 1 $

hee kumbe ngojera sijui shairi aisee hii tabia ya kukariri sio kabisa..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom