Vipi nijikwamue | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vipi nijikwamue

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Mama, Nov 27, 2008.

 1. M

  Mama JF-Expert Member

  #1
  Nov 27, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Nawauliza malenga, wa bara na visiwani,
  Kwa tungo mnazotunga, majibu nipatieni,
  Mwenzenu ninatanga, moyo wangu pepeeni,
  Ulimboni ninanasa, ni vipi nijikwamue.

  Nanasa nikijiona, niokoe nisizame,
  Naogopa hiki kina, cha ulimbo nikiseme,
  Nakihisi ni kirefu, msitake nijipime,
  Ulimboni ninanasa, ni vipi nijikwamue.

  Ulimbo wanivutia, unang'ara rangi yake,
  Jasmini wanukia, si haba harufu yake,
  Zeze unanipigia, napenda sauti yake,
  Ulimboni ninanasa, ni vipi nijikwamue.

  Nikipima kwa mizani, niko fifti fifti
  Wajuzi jibu nipeni, ulimbo wajizatiti
  Ulimbo kwangu mwilini, nitoeje watafiti
  Ulimboni ninanasa, ni vipi nijikwamue.
   
Loading...