Mabibi na mabwana tunapo tapatapa na pumzi kuweza kupumua, kumejitokeza mielekeo chanya sana katika kuwasaidia TRA kubaini vyanzo zaidi vya mapato yasiyokuwa na utata wowote.
Ni vizuri kila aitwaye mtu na hasa aliye mzalendo wa kweli akalipa kodi kwa kila aina ya pato alipatalo. Huo ndiyo ulio utaratibu katika dunia yote iliyostaarabika.
Unajiita vipi mzalendo au hata kuthubutu kujiita mzalendo hali wewe hulipi kodi?
Kama tumefika kudai kodi hata kwenye shughuli zozote zimhusishayo marehemu, kwa nini mtu yeyote na awaye yote asilipe kodi kwa pato lake lote alipatalo?
Tuanze sasa na waheshimiwa marais wetu wa nchi na bila kuwasahau wale waheshimiwa wabunge. Akina askofu Rashidi.
Iwe ni mshahara, posho, allowance, takrima nk. Hebu kila mtu na alipe kodi. Oneni hata aibu basi nyie kuachana na ubinafsi wenu usiokuwa na maana.
Mnaowakamua kodi kila uchao hali zao ni duni mno kuliko viongozi nyie mnaojilimbikizia marupurupu kila iitwayo leo. Mtoze kodi shughuli za misiba, harusi, Idd, Christmas nk huku kuna midume na mijike hailipi kodi? Wapi na wapi?
Misamaha yote ya kodi na ifutwe kwa watu na taasisi zote ziwe za serikali au vinginevyo.
Mnahamasisha wengine vipi kulipa kodi hali ninyi hamlipi kodi? Mtajuwa vipi kodi zilizopo kama ni kandamizi hali ninyi haziwahusu?
Au nasema uongo ndugu zangu?