Vipi mnahamasisha wengine kulipa kodi ikiwa ninyi hamlipi kodi? Mtajua vipi kodi zilizopo ni kandamizi ilihali ninyi haziwahusu?

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
7,676
2,000
Mabibi na mabwana tunapo tapatapa na pumzi kuweza kupumua, kumejitokeza mielekeo chanya sana katika kuwasaidia TRA kubaini vyanzo zaidi vya mapato yasiyokuwa na utata wowote.

Ni vizuri kila aitwaye mtu na hasa aliye mzalendo wa kweli akalipa kodi kwa kila aina ya pato alipatalo. Huo ndiyo ulio utaratibu katika dunia yote iliyostaarabika.

Unajiita vipi mzalendo au hata kuthubutu kujiita mzalendo hali wewe hulipi kodi?

Kama tumefika kudai kodi hata kwenye shughuli zozote zimhusishayo marehemu, kwa nini mtu yeyote na awaye yote asilipe kodi kwa pato lake lote alipatalo?

Tuanze sasa na waheshimiwa marais wetu wa nchi na bila kuwasahau wale waheshimiwa wabunge. Akina askofu Rashidi.

Iwe ni mshahara, posho, allowance, takrima nk. Hebu kila mtu na alipe kodi. Oneni hata aibu basi nyie kuachana na ubinafsi wenu usiokuwa na maana.

Mnaowakamua kodi kila uchao hali zao ni duni mno kuliko viongozi nyie mnaojilimbikizia marupurupu kila iitwayo leo. Mtoze kodi shughuli za misiba, harusi, Idd, Christmas nk huku kuna midume na mijike hailipi kodi? Wapi na wapi?

Misamaha yote ya kodi na ifutwe kwa watu na taasisi zote ziwe za serikali au vinginevyo.

Mnahamasisha wengine vipi kulipa kodi hali ninyi hamlipi kodi? Mtajuwa vipi kodi zilizopo kama ni kandamizi hali ninyi haziwahusu?

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Rebeca 83

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
12,816
2,000
Mimi nashangaa sana Tanzania kodi kila mahali watu wanabanwa halafu zinaenda wapi Chato! Nchi nyingine ukilipa kodi nyingine inarudishwa na iliyotumika kila mwananchi anapaswa kujua kodi yake imetumika vipi?

Any misuse of tax payer’s money is enough to take you out of office, only in Africa hakuna Rais anawajibishwa ndio maana wana make irrational decisions.
 
Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
13,329
2,000
Wanasema aliye nacho huongezewa na asiye nacho hunyang'anywa hata na kile kidogo alicho nacho
 
Benzodiazepine

JF-Expert Member
Oct 18, 2018
648
1,000
Wabunge wa Chama Tawala (Ruling Party), na pia Wabunge wa Vyama Visivyotawala (Opposition Party) wote hao hawawezi kujitungia Sheria za Kujikata KODI katika mishahara yao.

Akili za wabunge asilimia kubwa ni zile zile tu haijalishi yupo chama gani.
AISEEEH! PESA NI TAMU, KILA MTU ANAENDA BUNGENI KWA MASLAHI YAKE BINAFSI KWANZA.

Jamani eeeh tujitahidi kugombea nafasi za uongozi.
 
Scaramanga

Member
Aug 19, 2020
20
45
TRA watatunyonya mpaka tunyonyoke. Kodi ya kitanda, Kodi ya birthday, Kodi ya mpishi n.k
Sijawahi sikia hii ndg Alexander hapa TRA tutakuwa tunawaonea kabisa.Kodi nazojua wanatoza kwa mujibu wa sheria ni kodi ya mapato,VAT,liseni ya udereva,ya mshahara na sdl sasa hii ya birthday umetoa wapi. Tusichanganye ushuru wa Manispaa na Kodi za TRA
 
katitu

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
864

Hata ushuru nao ni Kodi ni tofauti tu ya majina.Mamc hawalipi Kodi.ushuru siyo Kodi na unatozwaje.si umepitishwa na madiwani ambao pia ni wabunge kupitia by-laws ambazo ziko kisheria pia.Mbona TRA wanalipwa etraduty ya 600,000/= na haikatwi Kodi kwa Nini?
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
7,676
2,000
Wabunge wa Chama Tawala (Ruling Party), na pia Wabunge wa Vyama Visivyotawala (Opposition Party) wote hao hawawezi kujitungia Sheria za Kujikata KODI katika mishahara yao.

Akili za wabunge asilimia kubwa ni zile zile tu haijalishi yupo chama gani.
AISEEEH! PESA NI TAMU, KILA MTU ANAENDA BUNGENI KWA MASLAHI YAKE BINAFSI KWANZA.

Jamani eeeh tujitahidi kugombea nafasi za uongozi.

Pana haja ya kuukataa unyonyaji wao huu usiokuwa na chembe ya huruma hata kwa wale walio wanyonge kweri kweri.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Kamakabuzi

JF-Expert Member
Dec 3, 2007
2,034
2,000
W
Mimi nashangaa sana Tanzania kodi kila mahali watu wanabanwa halafu zinaenda wapi Chato! Nchi nyingine ukilipa kodi nyingine inarudishwa na iliyotumika kila mwananchi anapaswa kujua kodi yake imetumika vipi?

Any misuse of tax payer’s money is enough to take you out of office, only in Africa hakuna Rais anawajibishwa ndio maana wana make irrational decisions.
Wabunge wanakuwakilisha - kama una swali, waulize
 
vvm

JF-Expert Member
Jul 18, 2014
3,949
2,000
Haiwezekani serikali hii ya wanyonge kuwa kuna watu wanalipwa kwa ela za wanyonge lakini hawalipi kodi hayo yalifanyika zamani enzi za upigaji na ubabaishaji tofauti na hapo ni UNAFIKI
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
7,676
2,000
W

Wabunge wanakuwakilisha - kama una swali, waulize

Wewe ni mbunge jombi? Au mnufaika wa hizi janja janja zao?

Kwamba hawa wanaweza kweli ghafla wakaokoka wakautambua mzigo wa kodi wanaotubebesha hali wao hawalipi? Aaaah Wapi! Thubutu!

Muda wa kuwashurutisha unazidi kujongea.

Au niko mbali na ukweli ndugu zangu?
 
Kamakabuzi

JF-Expert Member
Dec 3, 2007
2,034
2,000
Wabunge wa Chama Tawala (Ruling Party), na pia Wabunge wa Vyama Visivyotawala (Opposition Party) wote hao hawawezi kujitungia Sheria za Kujikata KODI katika mishahara yao.

Akili za wabunge asilimia kubwa ni zile zile tu haijalishi yupo chama gani.
AISEEEH! PESA NI TAMU, KILA MTU ANAENDA BUNGENI KWA MASLAHI YAKE BINAFSI KWANZA.

Jamani eeeh tujitahidi kugombea nafasi za uongozi.
Jikumbushe hoja za kwanza na Msukuma kwenye bunge hili akimhoji mgombea unaibu spika- hapo ndipo mawazo yalipo
 
Mtambwe

JF-Expert Member
Apr 14, 2014
704
1,000
Mabibi na mabwana tunapo tapatapa na pumzi kuweza kupumua, kumejitokeza mielekeo chanya sana katika kuwasaidia TRA kubaini vyanzo zaidi vya mapato yasiyokuwa na utata wowote.

Ni vizuri kila aitwaye mtu na hasa aliye mzalendo wa kweli akalipa kodi kwa kila aina ya pato alipatalo. Huo ndiyo ulio utaratibu katika dunia yote iliyostaarabika.

Unajiita vipi mzalendo au hata kuthubutu kujiita mzalendo hali wewe hulipi kodi?

Kama tumefika kudai kodi hata kwenye shughuli zozote zimhusishayo marehemu, kwa nini mtu yeyote na awaye yote asilipe kodi kwa pato lake lote alipatalo?

Tuanze sasa na waheshimiwa marais wetu wa nchi na bila kuwasahau wale waheshimiwa wabunge. Akina askofu Rashidi.

Iwe ni mshahara, posho, allowance, takrima nk. Hebu kila mtu na alipe kodi. Oneni hata aibu basi nyie kuachana na ubinafsi wenu usiokuwa na maana.

Mnaowakamua kodi kila uchao hali zao ni duni mno kuliko viongozi nyie mnaojilimbikizia marupurupu kila iitwayo leo. Mtoze kodi shughuli za misiba, harusi, Idd, Christmas nk huku kuna midume na mijike hailipi kodi? Wapi na wapi?

Misamaha yote ya kodi na ifutwe kwa watu na taasisi zote ziwe za serikali au vinginevyo.

Mnahamasisha wengine vipi kulipa kodi hali ninyi hamlipi kodi? Mtajuwa vipi kodi zilizopo kama ni kandamizi hali ninyi haziwahusu?

Au nasema uongo ndugu zangu?
Kweli kulipa Kodi ni Uzalendo, lakini tegemeo Langu ni kuwa wale wenye vipato vikubwa ndio walipe kubwa Zaidi, kwa mfanoo Raisi, mawaziri, wabunge Spika n.k. Lakini kuna wenge anbao hawalipi Kodi halafu wanalipwa marupu rupu hata hayahesabiki, uzalendo gani munaotaka tuonyesha maskini wa Mungu?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom