Vipi magereza wameita professional kwa ajili ya interview?|

Magereza kuna professionals?.,
kwani kazi ya kulinda wafungwa na mahabusu inahitaji digrii.,cha muhimu ujue tu kupozi kama komando Joni kwenye yale magari yao.
 
Katika wakati huu wa "TEHAMA" mambo mengi yanaitajika kubadilika, majeshi yetu pia yanaitaji kubadilika.
Magereza pia limeamua kutangaza nafasi za watu watakomba kazi kuna na Profession mbalimbali ili kuleta mabadiliko kwenye jeshi hili.
 
Magereza kazi yake kubwa sio kulinda wafungwa, kazi kubwa ya magereza ni kubadili tabia za wafungwa ili wakitoka huko waje huku kuwa raia wema. hivyo basi wanahitajika professionals kwaajili ya kuendesha gereza kisasa na kufanya hiyo kazi ya kubadili tabia pamoja na kuwapatia wafungwa stadi za maisha ili wakitoka waje wawe raia wema. Na lingine ni kuwa sasa hivi inatakiwa magereza yajiendesha kwa kuzalisha chakula chao. So kilimo cha kisasa kitawezekana bila professional wa kilimo? Jadili
 
Back
Top Bottom